Thursday, August 28, 2008

Ligi Kuu ya Vodacom
Yanga vs JKT Ruvu ........2-1
Mabao ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Wakenya - Boniface Ambani na Ben Mwalala jioni hii yametosha kuirejesha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa JKT Ruvu 2-1.

8 comments:

Anonymous said...

NGOMA INANOGA.ASANTE KAKA.

Anonymous said...

lEO SIJARIDHIKA NA STANDARD YA MPIRA TULIONYESHA.BUTUA BUTUA NYINGI SANA HATUCHEZI MPIRA WA KUPANGA.

Juma said...

Leo nilikwenda kushuhudia mechi, tumeshinda lakini hatukucheza mpira kabisa...hakuna uelewano na sijaridhika na uwezo wa Kondic...Tunayo safari sana kufika uwezo wa kutandaza mpira wa kufundishwa...

Anonymous said...

Jamani suala la kocha linanitia wasiwasi.Jana tumeshinda lakini timu haikucheza kitimu.Kama sio uamuzi wa Othman Kazi hata kushinda tusingeshinda.Owino alimkwatua mchezaji wa Ruvu lakini haikupigwa penelti.Tunamshukuru lakini tunahitaji marekebisho.Timu ilichoka sana kipindi cha pili na kutawaliwa na Ruvu.

Anonymous said...

mbona uliruhusu matokeo feki ya 2-2 jana? mimi nilienda kulala nikijua ni sare. usiwaruhusu wababaishaji wachafue site ya wapenzi wa Yanga.
-mpenzi wa Yanga, berks, UK

Anonymous said...

Suala la kocha: hivi uwezo wa kocha unapimwa kwa mechi moja? Mbona timu ilipocheza vizuri dhidi ya Prisons hatukusikia hizi lawama?

Hata timu kama ManU inaweza kucheza vibaya dhidi ya Bolton au timu ingine ndogo, lakini si sababu ya kocha. Inawezakana ni hali tuu ya mchezo. Tukumbuke, kinachotakiwa kwanza ni ushindi; kuremba baadaye. Hao waliocheza vizuri imewasaidia nini kama hawakufunga magoli?

Anonymous said...

'Anybody can have a bad day in office'
-Arsene Wenger after a Fulham match, which Fulham won 1-0!

Timu yoyote inaweza kucheza ovyo mpaka ukashangaa hata iwe Chelsea, Man U au L/pool!!

Hata jana Man U walichezewa na Zenit St Petersburg na kila mtu alikubali matokeo.

Yanga wako OK; usisahau ndio msimu umeanza bado wachezaji wana kutu-kutu kidogo baada ya muda kandanda litakuwa swafiiii!

-mpenzi wa Yanga. Berks, UK

Anonymous said...

asante Bwana Berks kwa koment iliyokwenda shule.
labda niulize leo nimesoma moja ya gazeti lenye ubia mkubwa na Yanga linasema Micho anarejea Yanga.

jee wadau hii ni kweli?

halafu lakini mimi naungana na wenzangu kuwa huyu mserbia "Mhaya" atazamwe upya nilitishwa na wachezaji kuchoka na nikafikiri atatumia muda huu wa wiki mbili kuimarisha hilo, tena nasoma gazeti la Kulikoni la leo eti kaenda likizo wiki mbili!!!!!!!!!!!!.

likizo mwanzo wa msimu!!!!!!!!