Monday, August 11, 2008

Yanga huru

Kamati ya Nidhamu ya TFF imewafungulia mabingwa wa soka wa Tanzania, Yanga kutoka katika adhabu iliyokuwa imepewa na TFF kufuatia kutopeleka timu katika mchezo wa kombe la Kagame dhidi ya Simba.

Hata hivyo licha ya kufunguliwa, Yanga imetozwa faini ya dola za Kimarekani 20,000 pamoja na viongozi wake kutakiwa kuomba msamaha kwa TFF kwa kitendo kisichokuwa cha kiuanamichezo cha kutopeleka timu uwanjani.

Mwenyekiti wa Kamati ya nidhamu ya TFF amesema kamati yake imetengua uamuzi huo wa TFF kwa vile hakuna kifungu kinachoeleza adhabu ya miaka 2 kwa timu inayokataa kupeleka timu uwanjani. Kwa hali hiyo, TFF ilitakiwa kutumia kifungu cha FIFA ambacho ni adhabu hiyo iliyotolewa na kamati yake.

.....Duh! usajili wote ule halafu tuishie kucheza na wauza ice cream - Azam FC?

7 comments:

Anonymous said...

Thanks CM. You are so active, man! Keep it up!

Anonymous said...

KWAHIYO ILE DOLA 35OOO. IMEFUTWA AU SASA IMEKUA 55000?

Anonymous said...

Hao nao wasanii wengine walikuwa wasikilize rufaa au watoe adhabu???Nani kawapa powers ya kikanuni kupiga faini???Tanzania hatufiki mbali kwa usanii.Mimi kama mwana Yanga napinga adhabu hiyo ya faini kwani haikufuata kanuni.

Anonymous said...

Anon 7:01:00 PM,

Kamati ya Nidhamu na ile ya juu yake ya Rufaa inapewa mamlaka (powers kama unavyoita) ya kutengua maamuzi ya kamati za mashindano na utendaji za tff na kutoa adhabu inayohusika. Mamlaka hayo yapo kwenye katiba ya tff. Huo ndio utawala wa sheria ndugu yangu.

Sasa wewe ukiwa 'mwanachama wa Yanga', kama hujaridhika ma mmamuzi hayo, unaruhusiwa kupinga kwenye kamati ya rufaa na utasikilizwa tuu kama utakuwa umefuata taratibu.

Pole kwa uchungu ulokupata ...

Anonymous said...

tusherekeeeeeee mamrukuuu na wajinga wajinga wajinyonge

pk-one said...

Pamoja na kwamba Rufani imeshinda kitu ambacho tulikijua ila hii adhabu ya USD 20,000 imetoka wapi? na ni nani anayestahili kulipwa faini hii ni TFF? au waandaaji wa michezo CECAFA ..., hawa jamaa wasilete ubabaishaji .... wasitake kujivunia fedha za bure bure wao sio waandaaaji wa michezo iweje walipwe hizo fedha na CECAFA nao vile vile walipwe hizo 35,000 bado haki haijatendeka hapo....

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___