Tuesday, September 16, 2008

Ivo Mapunda kutimkia Ethiopia?


Kipa wa Yanga na Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Ivo Mapunda huenda akatimkia nchini Ethiopia muda wowote wiki hii kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa.

Ivo anatarajiwa kwenda kufanya majaribio katika kikosi cha timu ya St. George ya huko ambayo inanolewa na kocha wa zamani wa Yanga Sredovedic Milutin 'Micho'.

Viongozi wa Yanga bado wapo gizani kuhusu suala zima la Ivo kuondoka kwenda Ethiopia kwani timu hiyo haijawasiliana na uongozi wa klabu hiyo kuhusu masuala ya uhamisho.

Ivo kwa sasa amekosa namba ya uhakika katika kikosi cha kwanza cha Yanga kufuatia kusajiliwa kwa Juma Kaseja ambaye ndiye anliyedaka katika mechi zote tatu za ligi ambazo Yanga imecheza hadi sasa.

Kama atafanikiwa kucheza soka nchini humo, Ivo hataweza kushiriki katika timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambayo inajiandaa na michuano ya wachezaji wa ndani ya nchi (CHAN) ambayo Stars inakabiliwa na kibarua kigumu dhidi ya Sudan mwezi Novemba.

4 comments:

Anonymous said...

Tumeacha mbachao kwa msala upitao.Kaseja ni mwanachama wa Simba na sasa wamepata udhamini atarudi Simba ama sivyo itabidi tumpe pesa nyingi zaidi kwani mkataba wake ni wa mwaka mmoja na alifanya hivyo ili arudi Simba.Kumtupa na kumdhalilisha Ivo kutatutokea puani.Ni suala la muda tu.

Anonymous said...

Kweli kabisa, Kaseja mwakani anarudi Simba, na hiyo mechi na Mnyama oktoba 26 atadaka nani???Kaseja hakai golini na huyo mserbia mhh...naonoa utejaa utaendelea tuu...

Anonymous said...

Kwa nini Asikae Golini?... Lazima ni mchezaji halali na anachezea Yanga sio simba mpira ni ajira jamani pamoja na upenzi ajira inabaki pale pale ila Yanga nao inabidi wafanye-rotation kwa makipa wao kucheza sio kila siku Kaseja tuuuuu!.
Simba hapajatulia Wako dhaifu mwaka huu...

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___