Sunday, September 21, 2008

Yanga yaendeleza 100%

Kutoka kushoto waliosimama:Boniface Ambani, George Owino, Abdi Kassim, Juma Kaseja, Wisdom Ndhlovu na Kiggi Makassy. Walioinama kutoka kushoto: Shamte Ally, Mrisho Ngassa, Fred Mbuna, Godfrey Bonny na Nurdin Bakari.


Katika hali inayoonyesha kwamba msimu huu mambo ni moto, Yanga hadi sasa imefanikiwa kushinda mechi zake zote 5 za ligi ilizocheza hadi hivi sasa.

Ushindi huo wa 5 mfululizo umehitimishwa leo kwa ushindi wa 5-0 dhidi ya Villa Squad ya Dar kwenye Uwanja wa zamani wa Taifa Jijini.

Mshambuliaji Boniface Ambani bado anaonekana ni mwiba mchungu kwa nyavu za timu zote pinzani ambazo imekutana na Yanga kwani ndiye mshambuliaji pekee ambaye ameweza kuweka rekodi ya kufunga katika mechi 5 mfululizo.

Hadi hivi sasa Ambani ana mabao 8 ambayo ameyafunga dhidi ya Prisons (2), JKT Ruvu (1), Mtibwa Sugar (1), Moro United (1) na Villa Squad (3).

Mshambuliaji Ben Mwalala naye kutoka Kenya naye msimu huu anaonekana 'kufufuka' baada ya kuziona nyavu mara 4 hdi hivi sasa.

Katika mchezo uliopigwa leo, Yanga ilichezesha kipa wao mzungu kutoka Serbia Obrev Cirkovic ambaye alionyesha umahiri wake pale alipookoa penati iliyotolewa na mwamuzi baada ya mlinzi mmoja wa Yanga kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Tunawatakia kila la heri katika kudumisha 100%

3 comments:

Anonymous said...

naomba ratiba ya yanga tafadhali sana.

Anonymous said...

Kipa mzungu mzima saana, wenye kawafunga midomo

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___