Sunday, October 26, 2008

Imebaki story! Yanga kidumeBen Mwalala

Bao pekee liliolofungwa na mshambuliaji Ben Mwalala wa Yanga leo limehitimisha unyonge wa miaka 8 wa klabu hiyo kwa mahasimu wao Simba baada ya kushinda 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa kwenye uwanja mkuu wa Taifa.

Mchezo wa leo umeshuhudia kadi tatu nyekundu zikitoka, mbili kwa wachezaji wa Simba Haruna Moshi na Meshack Abel ilihali kwa upande wa Yanga alikuwa Ben Mwalala.

Uimara wa mlinda mlango wa Yanga Obrev Cirkovic leo umechangia kwa kiasi kikubwa kuwakatisha tamaa washambuliaji wa Simba ambao walikuwa wakiliandama lango la Yanga kwa nia ya kusawazisha bao hilo.

Kwa upande wa ulinzi, beki Nadir Haroub leo alikuwa mhimili mkubwa na katika kiungo wa ukabaji kwa kweli kiungo Godfrey Bonny leo alifanikiwa kufanya kazi yake vizuri japokuwa kuna wakati alikuwa ameelemewa kutokana na kiungo wa ushambuliaji Athumani Iddi kutokuwa katika hali nzuri kimchezo. Hata hivyo katika kipindi cha pili Nurdin Bakari aliongeza nguvu katika sehemu hiyo na timu ilionekana kuweza kubana katika sehemu ya kiungo.

Katika ushambuliaji, Boniface Ambani alikuwa amepaniwa sana kiasi kwamba aliumizwa na mabeki wa Simba na akashindwa kuendelea na mchezo. Mchezaji Mrisho Ngassa leo alishindwa kufanya kile ambacho wengi walikitarajia na muda mwingi alikuwa akifanya madhambi.

Hata hivyo Simba leo walionyesha mchezo mzuri licha ya kufungwa na Yanga. Kiungo Haruna Moshi leo aling'ara sana kwa pasi safi za mwisho alizokuwa akizitoa kwa akina Musa Hassan na Emmanuel Gabriel lakini washambuliaji hao walikwamishwa ama na uimara wa kipa au walikuwa wakipiga mipira nje.

Kwa ushindi huo, Yanga imefikisha pointi 27 wakati Simba imebakiwa na pointi 13 kutokana na michezo 10.

Yanga: Circkovic, Nsajigwa, Nurdin, Owino, Nadir, Bonny, Shamte, Chuji/Mumbala, Ambani/Maftah, Mwalala na Ngassa/Makassy.

Simba: Amani, Kanoni, Jabu, Abel, Yondani, Henry, Nyagawa/Kijuso, Banka, Gabriel/Ulimboka, Mgosi na Haruna.

Kwa kweli sasa imebaki story, hatimaye tumewafunga.

20 comments:

Anonymous said...

lete halua ,na sisi tuvinjari asante vingozi na wachezaji wa yanga tumetoka vifua mbele.

Anonymous said...

Great analysis. Muhimu kwanza ushindi. Mechi ya Yanga v Simba huwa iankuwa na pressure kwa wachezaji, hivyo utakuta mchezaji anakuwa off.

Vipi hali mazingira ya red cards?

Anonymous said...

Hata siamini kwani hawa jamaa wametunyanyasa sana HONGERA SANA YANGA, HEBU KULENI HAYO MAMILIONI MLIYOAHIDIWA NA KLABU YENU. MPIRA PESA BWANA ZAMA ZA KUCHEZA KUUZA MAJINA NA UMAARUFU ZIMEPITA. Hao simba waacheni wajisifie na kujifariji kwa kucheza mpira mzuri, sie mabao tu! mpira bila magoli ni sawa na kuwa na mwandiko mzuri halafu unafeli mtihani. YANINI HAYO? YANGA OYEEEEEEEEEEEEEEEE

Anonymous said...

Timu ya Yanga inastahili pongezi kwa kazi nzuri waliyofanya. Hii na dalili njema kwenye safari ya mashindano ya CAF. Kikubwa ni kuanza maandalizi mapema.
HONGERA SANA YANGA KWA KUWANYAMAZISHA MSIMBAZI.

Anonymous said...

Tatizo bado kuna kuelewana kudogo pale kati ya Owino na Nadir. Owino mzito na anakosea saana anyway tumwachie mwalimu yeye ndo anawajua zaidi

Anonymous said...

Hongera yanga na Ahsante blog manager!!!!
OMBI KWA WADAU WA YANGA
Jamani wadau wa ughaibuni atakayekwenda Tanzania karibuni tumtafutie huyu mdau hapa simple digital camera na kama ikiwezekana hata scanner kwani hiyo itamwezesha kuweka picha za matukio moja kwa moja badala ya kusubiria za kwenye magazeti mengine hasa kwa mapambano ya Dar es Salaam. Hili linaweza kufanywa pia na wadau walioko Tanzania kwani kuna watu wenye uwezo wa kufanya haya hata huko nyumbani, YANGA NI TIMU KUBWA SANA SEMA WENYEWE HAWAJUI KUTUMIA FURSA KIUHAKIKA. FREDRICK MWAKALEBELA WA TFF AU SALEH NJAA YUPO CONTRACTORS REGISTRATION BOARD(CRB)ni mwanasheria WANA UWEZO WA KUMSAIDIA MDAU HUYU ANAYEWEZA KUWAONA WATU HAWA BASI AWATAFUTE AWAPE UJUMBE KWANI WOTE HAO NI YANGA DAMU, watamnunulia camera huyu bwana, pia kuna Burton Mahenge mwanasheria wa manispaa ya Kinondoni ni Yanga DAMU kuliko hata Madega.

Anonymous said...

Mdau hapo juu umesahau Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh. Jakaya Kikwete ni yanga damu unaweza kumuona au kumtumia ujumbe mtoto wake Riz 1 akafanya vitu. Kesho lazima apite hapa nitamfikishia ujumbe.

Anonymous said...

Unajua mambo mengine siyo utani, ili simba ichukue ubingwa inabidi tufungwe mechi tano na wao washinde zote. Ningewashauri waanze kuandaa timu ya msimu ujao na waache mtindo wa kuandaa timu kwa ajili ya mechi moja.

Anonymous said...

MDAU HAPO JUU UMENENA HUYU MANAGER KUNA HAJA YA KUMFAHAMU TUMSAIDIE WAZO HILI KANIPA HATA JAMAA YANGU YUKO UK MASOMONI.

HUYO JAMAA MANAGER AWASILIANE NA UONGOZI KWA MSAADA HUO

KUHUSU MECHI YA JANA KWA KWELI BINAFSI NILITOKWA MACHOZI YA FURAHA BAADA YA MECHI KUISHA.

NAMSHUKURU MAULID KITENGE TULIYEKUWA NAYE BROADCASTING ROOM KWA KUNISUPPORT.

SIE TUPO KWENYE MEDIA NIMEMTAJA KITENGE KWA KUWA NI YANGA MWENZANGU
LAKINI KUNA MWANDISHI MWENZETU MPIGAPICHA YEYE NI SIMBA ALITIA AIBU KWA KUBEBA UCHAWI AKITAKA KWENDA KUWEKA LANGONI KWETU
NAWASHUKURU MUHIDIN SUFIANI WA MTANZANI,SELEMAN MPOCHI WA GUARDIAN,MWENDAPOLE WA UHURU NA KISAKA BEN WA MAJIRA KWANI WALIMSHITUKIA NA KUMTIMUA
ILIKUWA KITUKO
TEHETEHE
ASANTE WADAU WANAYANGA

Anonymous said...

JAMANI KUNA HAJA YA KUMCHANGIA HUYU MWENYE BLOG. MIMI NIKO HAPA HAPA NCHINI TANZANIA.ILI HUYU MWENYE BLOG AWEZE KUIBORESHA NA SISI WANANYANGA TUZIDI KUWA NA UWEZO WA KUPATA TAARIFA AMBAZO NI CURRENT. HIVYO NASHAURI HUYU CM AWEKE ACCOUNT NUMBER YAKE LIVE ILI TUMSAPOTI KWA KAZI NZURI.WAKATI ANAENDELEA KUWASILIANA NA VIBOSILE WENGINE ILI WAMPE DIGITAL CAMERA, SISI PIA TUMSAPOTI.

Anonymous said...

JAMANI TUNASHUKURU MEDIA, KWA KUTANGAZA LIGI YA VODACOM. ILA KUNA BAADHI YA WATANGAZAJI WANAWEKA USHABIKI KWENYE KURUSHA MATANGAZO. MFANO JANA BARUANI MHUZA JANA ALIFANYA MAMBO YA AJABU NA KUFANYA UMATI UAMINI KWAMBA REFA KAIBEBA YANGA. PALE AMBANI ALIPOUMIZWA BARUANI AKACHEKA SANA.AKASEMA KAVAMIWA NA MWANAUME MWENYE NGUVU.LAKINI WAO WANAPOCHEZA MADUDU WAKIONYWA ANASEMA REFA ANAPENDELEA. TABIA HII HATA JUMA NKAMIA ANAYO.KWA HABARI ZA CHINI CHINI SIMBA WALIDANGANYWA ETI WATUMIE MBINU YA KAGERA SUGAR YA KUCHEZA KWA FUJO NA NGUVU NYINGI ILI TUSHINDWE KUCHEZA .MATOKEO YAKE WAKAAMBULIA KADI NYEKUNDU KIBAO

Anonymous said...

CM NAOMBA UWEKE SEHEMU YA KUDONATE KWA AJILI YA BLOG YETU. THEN MTU AKIBONYEZA HIYO SEHEMU AKUTE ACCOUNT NUMBER NA JINA LAKO KUSUDI TUCHANGIEEEEEE. SIYO TUNYWE ULABU TUU. PIA NINA FURAHA CHAMA LANGU LIVERPOOL JANA LILISHINDA NA KUONGOZA LIGI YA ENGLAND. NAMPA POLE SANA MDAU WA YANGA ILA MSHABIKI WA CHELSEA KWA LIVERPOOL KUVUNJA MWIKO WA MIAKA MINNE YA CHELSEA KUTOFUNGWA KWAO.KAMA YANGA WALIVYOMFANYIAA MNYAMAA SIMBA!!!

Anonymous said...

POLE SANA NDUGU YANGU MASEBE MSHABIKI WA CHELSEA. ILA KWA YANGA TUKO PAMOJA

Anonymous said...

Ndugu wa media tunashukuru umetoa ufafanuzi mzuri kuhusu hizo ndumba, kwa kadri ya matangazo ilionekana ndumba hizo ni za yanga, huu kumbe ulikuwa upotoshaji wa hali ya juu. asante kwa hilo.

Anonymous said...

kutoka kwa Mdau wa Media

asante mkubwa halafu pia kuna haja ya viongozi wetu kuambiwa, manake sie waandishi tunajuana akina nani yanga na nani simba.
sasa binafsi huwa naumia kukuta mambo ya Yanga viongozi wetu wanakuwa wakiwashobokea waandishi ambao sisi tunawajua ni Simba.
kuhusu Baruhan yeye na wenzake akina Ndimbo.
hata imani za kishirikina walionyesha wazi kuwa ni Yanga waliokuwa wakifanya!!! ilihali ukweli ni kwamba tunguli ziliwekwa na kipa wa simba Amani Simba muda mchache kabla pambano halijaanza, na wakatikipindi cha kwanza kinaisha akasahau kuzitoa ndipo baadaye wao wenyewe wakaanza kung'ang'ana kuzitoa.
ila yote kwa yote tupo makini kwa sasa, wale wababaishaji ambao walikuwa wnajifanya kuwa karibu na timu halafu wanauza siri safari hii tuliwaweka pembeni.
Yanga hoye

Anonymous said...

kutoka kwa Mdau wa Media

asante mkubwa halafu pia kuna haja ya viongozi wetu kuambiwa, manake sie waandishi tunajuana akina nani yanga na nani simba.
sasa binafsi huwa naumia kukuta mambo ya Yanga viongozi wetu wanakuwa wakiwashobokea waandishi ambao sisi tunawajua ni Simba.
kuhusu Baruhan yeye na wenzake akina Ndimbo.
hata imani za kishirikina walionyesha wazi kuwa ni Yanga waliokuwa wakifanya!!! ilihali ukweli ni kwamba tunguli ziliwekwa na kipa wa simba Amani Simba muda mchache kabla pambano halijaanza, na wakatikipindi cha kwanza kinaisha akasahau kuzitoa ndipo baadaye wao wenyewe wakaanza kung'ang'ana kuzitoa.
ila yote kwa yote tupo makini kwa sasa, wale wababaishaji ambao walikuwa wnajifanya kuwa karibu na timu halafu wanauza siri safari hii tuliwaweka pembeni.
Yanga hoye

Anonymous said...

Inasikitisha wenzetu wa simba ushirikina wameweka mbele kuliko mazoezi.

Anonymous said...

Naungana na Muganyizi kuhusu watangazaji wa tbc Nkamia,Baruan na Ndimbo , hawa jamaa itikadi ya simba imewatawala kupita kiasi mf kwenye mechi ya yanga na mtibwa Morogoro Ndimbo alitamka wazi wazi kwamba hali hapa ni mbaya refa kavurunda mchezo ,Nkamia ndio haisemeki kule kagera kipindi cha kwanza mwenyewe alitamka kwamba mchezo unaochezwa hapa na kagera haufai kuonwa na mtoto mdogo baadae mwisho anasema yanga walibanwa kila idara huku akifurahia , Baruan kwenye mechi ya jana mwishoni akasema refa huyu kavuruga kabisa mchezo mbali na kutaka kufunga goli kwa mdomo,Nkamia kwenye mechi moja ya simba aliwahi kusema kwamba mchezo huu umepooza pamoja na kujitahidi kwangu kuufanya uonekane umechangamka(inaashiria kwamba huwa anaongeza chumvi kwenye mechi za simba )Mapenzi ya kutupwa ya Nkamia ndiyo yaliyopelekea kumtangaza Haruna Moshi kuwa ndio mfungaji wa bao la stars kule Burkinafaso ,hayo ni kwa uchache tu.Binafsi sidhani kwamba mtangazaji ana nafasi ya kumkosoa mwamuzi hadharani kupitia kipaza sauti kwani kazi yake kubwa ni kutangaza kile kinachotokea mchezoni na si vinginevyo tunaelewa kwamba kila mtu ana itikadi yake lakini mtangazaji anapaswa kuidhibiti hali hiyo kama ilivyokuwa kwa wenzao waliopita .Nadhani bwana Tido Mhando anapaswa kuliangalia hili ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea kama ilivyotokea kwa Dalali ambapo watangazaji kupitia vipaza sauti vyao walikuwa wanatamka kwamba si bure simba kuna kitu wakati wanajua kwamba mpira una kushinda ,kushindwa na droo ingawa niliwahi kumsikia Nkamia kwa ushabiki wake akisema kwamba siku hizi kuna la nne la kukimbia.

Anonymous said...

Ndugu zangu wanayanga hali tunaona ilivyo,wanahabari wa Simba wanakera,jana mimi nililazimika kuachakumalizia dk 20 za mwisho kwa sababu mtangazaji alikuwa ni kero tupu.Alitangaza mpira wa upande mmoja tu kama vile yanga wao hawapo uwanjani. Mimi nishangaa kusikia Canavaro alipigwa na Haruna Moshi,jana sababu za kupewa kadi nyekundu hazikusemwa,hivyo kuonekana kama ameonewa,sitaki kusema chochote kwa Mkamia kwa sababu huyu bado anfanya kazi ya katibu mwenezi wa simba kupitia tbc. Tunaomba waandishi mlio wanayanga mtoe majina yenu tuwafahamu jamani msijifiche,nimefurahi sana kusikia akina Mwakalebela,Ben kisaka kumbe ni wenzetu.Jitajeni jamani mnaogopa nini.

Anonymous said...

Jana Dalali katoa tamko kuhusu kipigo, ni aibu tupu , Talk of the day ya 92.9 magic Fm chini ya Cyprian Musiba wakaitoa na kuijadili lakini walisahau ( kwa yeyote aliye karibu na Musiba amwambie wamuulize Dalali Live yafuatayo )
i. Nini alichokwenda kufanya uwanjani goli la kaskazini yeye na Mgosi kabla ya mechi kuanza na ni kwa mujibu wa kanuni gani ya soka na ni mahala gani pengine duniani amewahi kuona vitu kama hivi vikifanyika hadharani tena kwenye pitch , kwanini Tff isimchukulie hatua ?
ii.Katika orodha ya mechi alizozitaja kwmba wachezaji wao walikuwa wametolewa kwa kadi nyekundu matokeo yalikuwaje?
iii.Kama kucheza pungufu ndio sababu ya timu kufungwa ankumbuka mechi yao na polisi Dodoma mwaka jana wachezaji wangapi wa polisi walitolewa na matokeo yalikuwaje?hakukuwa na ufisadi?
iv.Anakumbuka aliwahi kunukuliwa kwamba wataifunga yanga wakati wowote uwanja wowote hata kama ni Kaunda na waamuzi wakiwa ni Manji akisaidiwa na Madega na Kisasa ? leo anaweweseka nini
v.Anakumbuka kutamka kwamba wana mkata wa kuifunga Yanga kwa miaka kumi na yeye atjiuzulu kuiongoza simba kama ikitokea watafungwa na Yanga kabla ya muda huo kwisha?
vi.Aliangalia mechi ya Arsenal na Hull City?Arsenal ilikosa magoli mangapi ya wazi ambayo mfungaji wake wa kubahatisha Mgosi anaamini hawezi kukosa?
vii.Huyo mchezaji anayemtuhumu ( Mgosi ) ameshafunga magoli mangapi tangu ligi kumalizika kwa Taifa Cup pamoja na kupigiwa debe aitwe Taifa Stars
Mwisho ningependa kuwaambia wana Yanga wenzangu kuwa waswahili wanasema atambuaye ndwele mganga ni yeye na siku zote mwanaume mgoni ankuwa na wivu sana na mkewe na vile vile mwizi ni mwoga mno kuibiwa , inavyoelekea hawa mabwana miaka yote hiyo walikuwa wakitufunga kwa mbinu chafu kwa wafuatiliaji wa mambo nadhani mnafahamu kwa sababu za kuasisiwa kwa kundi la friends of simba ambalo kazi yake ya kwanza ilkuwa ni kukisambaratisha kikosi cha ushindi cha Yanga wakati ule kwa mbinu hizi na kupandikiza watu wao