Monday, October 27, 2008

Ligi Kuu ya Vodacom

Msimamo wa ligi
Mwaka huu tunapaa kweli kweli si mchezo. Kuna timu moja hivi inashika nafasi ya tatu kwa wingi wa magoli ya kufungwa.

10 comments:

Anonymous said...

Viongozi wa Yanga watoe maelezo ni kwa nini waliweka aya za kidini kwenye muhuri. Ni vema maelezo hayo yawekwe pia hapa. Vinginevyo tunakosesha watu raha,

Anonymous said...

Ni hoja ya msingi kwa upande mmoja kwani inaweza kutafsiriwa na baadhi ya watu katika namna ambayo sio sawa kwani watu wanaweza kuihusisha na mambo fulani fulani, Lakini kwa upande wa pili inawezekana walifanya bila kufahamu au kutarajia mwitikio hasi kutoka kwa jamii hivyo ni vyema wakaweka wazi ili watu watokwe na wasiwasi badala ya kuacha hali hii iendelee na kuongeza maswali kuliko majibu.
YANGA ALUTA KONTINUA.

Anonymous said...

hivi mpaka leo mnaamini ushirikina kwenye soka? hivi Brazil, Italy, Ujerumani ni wachawi saana ? HAYO MANENO YAMEWEKWA ILI KUWATISHA TU WASIOKWENDA SHULE AKIKA DALALI. hakuna chochoteee

Anonymous said...

Wakati mwingine huwa sielewi ni nini hasa lengo la dini ya kiislamu. Mechi ijayo wekeni maandiko ya biblia uone kama kuna mtu mkristo yoyote atakayelalamika ila nakuhakikishia waislamu wataandamana na kuzuia hiyo mechi isichezwe kwa sababu tiketi zina maandiko ya biblia na watawaambia waislamu wote wasinunue hizo tiketi.
Uchawi kwenye mpira ni tishia toto tu hebu waiteni wachawi wote mnaowajua waipe uchawi timu ya taifa ichezi na Brazil.

Anonymous said...

aibu kubwa sana kwa wote wanaoamini uchawi ,ndio maana malbino wanauawawa kila siku ,jamaani sasa wakati wa kuamka .

Anonymous said...

Jamani huu mjadala unatusaidia nini.Mwanzo nilifikiri hayo maneno labda yalikuwa yakashifa fulani, lakini tafsri yake inaonyesha ni maneno ambayo hayana shida yoyote kwangu kama mkristu sijui kama yanawakwaza wenzetu waislam.Uchawi katika soka hakuna acheni umbumbumbu.Simba wametufunga miaka nane hao wachawi walikuwa wapi wasitusaidie.Chambueni mambo kitaalam zaidi si kienyeji hivyo.Nisaidie tu kusema kwamba uchawi wa Yanga ulianzia wakati wa usajili,kila mwenye akilianafahamu kuwa yanga wametumia fedha nying kupata timu bora,kulipa mishahara,kuandaa timu,wengine walidharau, haya ndiyo matokeo yake tunayo yaona. Timu imefungwa mechi moja tu katika 10,unahitaji kutafuta mchawi katika hili? Niwakumbushe simba kwamba maandalizi wanayafanya kwa ajili ya kuifunga yanga na sivinginevyo.Matokeo yake wana pointi 13 katika michezo kumi, hata kama wangeifunga yanga ingewasaidia nini kwa nafasi walipo. Hii ni nchi ya wajinga wanaoheshimu uchawi utawaletea maendeleo katika karne hii ambayo sayansi imeonyesha uwezo mkubwa.Watanzania tuamke, tusome, dunia inakimbia kwa kasi kubwa.Mtamaliza maalbino,mtageukia watoto wenu na mtaendelea kuwa masikini milele.TUNATIA AIBU KUKUMBATIA UCHAWI WAKATI TUNA UMASIKINI UNAOPINDUKIA.Hizi ndizo gharama za ujinga.Timu yoyote duniani iliiweze kufanya vizuri inahitaji kuwa na fedha za kutosha,kwa hiyo utasajili wachezaji wazuri,kocha mzuri, mishahara mizuri,vifaa vya mazoezi vya kutosha nk.Historia inaonyesha kuwa hata huko ulaya timu zote zenye majina makubwa zina fedha za kutosha ilikuleta mafanikio na si uhodari wa kubeba hirizi. NIMESEMA SANA LAKINI INANIUMA KUONA NCHI YANGU KATIKA KARNE HII AMBAYO DUNIA IKO MIKONONI MWA KILA MTU SISI TUNAIBUA MIJADALA YA USHIRIKINA. TAFADHALI TUJIFUNZE KWA WALIO TUTANGULIA.

Anonymous said...

Sasa hivi kwa Yanga pa kurekebisha ni pale katikati yaani anatakiwa beki wa kati wa kusaidiana na Nadir, huyu Owino anabutua saana ni rahisi kumtoka. Tuna wakati mzuri wa kujipanga kujiandaa na mabingwa wa africa, na naomba wasishiriki Kagame ili wapumzike na waanze mazoezi wakiwa wako safi, hili kombe halisaidii chochote ni kupoteza pesa tu.

Anonymous said...

Kombe la Kagame (au mashindano yayote yale) ni muhimu kama sehemu ya mazoezi ktk kujipima -match fitness.

*samahani wandugu: hivi tulishaondolewa adhabu ya cecafa miaka 3? nauliza maana mdau hapo juu amegusia kagame!

Anonymous said...

MSIKIENI HASSAN DALALI ANAVYOTAPATAPA KOCHA WAKE AMBAYE NI MTALAAM WA SOA KAKUBALI GOLI LA YANGA LILIKUA SAFI NA KADI YA HARUNA MOSHI ILIKUA SAFI HAINA MATATIZO YEYE ANABWABWAJA HAPA CHINI" hebu msikieni........
"Dalali pia alisema mfungaji wa bao la Yanga Mwalala na hata Boniface Ambani aliyetoa krosi iliyozaa bao hilo alikuwa tayari amekwishaotea lakini waamuzi walifumbia macho jambo hilo. Kutokana na mlolongo huo wa ufisadi wa waamuzi , Simba imesema haitokuwa tayari kucheza na Yanga kama waamuzi wa aina hiyo ya Mwandike wataendelea kupangwa na kuitaka TFF kutafuta waamuzi kutoka nje ya nchi ambao hawatakuwa na mapenzi na timu hizo mbili na kuondoa harufu ya ufisadi".
“Kuanzia Kamisaa wa mchezo, mwamuzi wa kati, wasaidizi wake na wa mezani wote ni Yanga na hii kuhakikisha hata kama mwamuzi ataharibu mchezo analindwa kwa kuandikiwa ripoti nzuri,” Dalali alisema. Aidha, Dalali amehoji kwa nini kila mechi ya Simba na Yanga kamisaa wa mchezo ni lazima awe Alfred Luiza jambo ambalo linaashiria kuwapo na ajenda ya ufisadi wa kuihujumu klabu yake"
source HABARI LEO @http//habarileo.co.tz/michezoburudani

Anonymous said...

Akaandae timu jumamosi wanakutana na Minziro atawaua tena.Hii imepita waache longolongo wako pabaya,jumamosi haiko mbali