Friday, November 21, 2008

Yanga kujitoa Tusker?

Mabingwa watetezi wa Kombe la Tusker, Yanga huenda ikajitoa katika michuano hiyo kwa mwaka huu.

Kujitoa huko kunasababishwa na wachezaji wengi wa klabu hiyo kubanwa na ratiba ya michuano ya kimataifa wakiwa katika timu ya taifa - Taifa Stars.

Taifa Stars imeingia kambini kwa ajili ya kupambana na Sudan katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani ya nchi. Mechi ya kwanza itafanyika Dar es Salaam Novemba 29 na ile ya marudiano itapigwa Desemba 13 huko Khartoum.

Ratiba ya michuano ya Tusker inaonyesha kwamba michuano hiyo itaanza Desemba 15, hali itakayoipa Yanga wakati mgumu wa kujiandaa kikamilifu na michuano hiyo hasa ukizingatia kwamba klabu hiyo ina wachezaji 10 katika timu ya taifa.

Wachezaji walio katika kikosi hicho ni Shadrack Nsajigwa, Nadir Haroub, Amir Maftah, Geodfrey Bonny, Nurdin Bakari, Kiggi Makassy, Athumani Iddi, Abdi Kassim, Mrisho Ngassa na Jerry Tegete.

12 comments:

Anonymous said...

Nadhani Yanga inao wachezaji 30. Kwa hiyo kuna wachezaji 20 ambao hawako Taifa Stars.
Mechi ya kwanza timu inaweza kutumia hawa 20, na mechi zitakazofuata wale wa Stars wataongeza nguvu baada ya kumaliza mechi na Sudan (kwanza si wote watakaocheza mechi zote 2 na Sudan kwa hiyo hawatakuwa na uchovu wowote).
Kujitoa Tusker ni kuwavunja nguvu hawa 20 waliopo na pia kutowatendea haki
Kumbuka ktk hawa 20, yumo yule kipa 'Obren cirkovic'(?) wa serbia, Ambani, Mwalala n.k. ambao wana viwango vya kutosha.
Kwa maoni yangu, Yanga inatakiwa ijiandae kushiriki. Hawana sababu ya kujitoa. Hata kama hawatachukua ubingwa timu itakuwa imepata mazoezi muhimu na uzoefu 'fulani' wa mechi za kimataifa.
Wale ambao huwa hawamo ktk 11 watapata nafasi ya kumuonyesha kocha kiwango chao cha soka na mchango wao ktk timu.
Pia kibiashara Yanga inahitaji mapato. Kujitoa ktk mashindano timu itakosa mgawo wa hela na wa viingilio. (Unajua sisi watanzania suala la biashara tuko nyuma kwa vile tumezoea kuomba misaada kwa wafadhili/wahisani.
Yanga inatakiwa kuwa na vyanzo vyake vya fedha, mfadhili wetu ataongezea tulicho nacho -sio tumtegemee kwa 100%. Kushiriki ktk michuano hii ni njia mojawapo ya kujiingizia mapato ndugu zangu).

Shabiki wa Yanga, England.

Anonymous said...

Jamani lazima tuelewe mambo hapa. Kwa mfano mgogoro wa simba unatokana na timu kufanya vibaya kwenye ligi. Kama tukiingiza timu ambayo haiko tayari na kufanya vibaya hiyo inaweza kuleta mgogoro mkubwa sana klabuni. Sasa hivi tuna ushirikiano mzuri sana lazima tuepuke mambo yatakayotuletea migogoro. Kumbukeni timu zilizopo tusker zote ni nzuri na tunaweza kufungwa mechi zote na kombe lenyewe ni hasara tu kama hujachukua ubingwa.
Naunga mkono uongozi,
Shabiki wa Yanga, Mtwara

Anonymous said...

uoga usiokuwa na msingi na kutojiamini.Tumesajili wachezaji 30 wa nini kama hatuwaaamini.Mawazo finyu kwamba kufungwa kutaleta mgogoro!!!Je tujitoe kwenye klabu bingwa ya Afrika kwa sababu kuna hatari ya kufungwa??.Mpira kuna kushinda na kushindwa.Nilitegemea mawazo hayo finyu kutoka kwa wenzetu lakini sio kwa viongozi wetu wanaojifanya wasomi.

Anonymous said...

soka ni biashara sio kuchukua kombe ,kwani kombe ni la nini ?bila hela utaendeleza soka? vingozi wengine ni wabovu tuu hata ufanyeje,kwani huyu madega anakua na uhakika wa kushinda kesi zote anapopata wateja ?

Anonymous said...

Kombe la Tusker halina mpango. PERIOD.

Anonymous said...

Kweli inahitaji kufikiri sana kuhusu hili na tupunguze jaziba tuone ukweli wa mambo. Ni kweli timu imeajili wachezaji 30. Lakini kokote duniani timu inakuwa na kikosi cha kwanza na cha pili.Kwa ujumla ukiondoa wachezaji 10 walio kwenye Timu ya Taifa wale wa kikosi cha kwanza wanabaki ni wale wakigeni tu. Kwa hiyo ni lazima tukubali kuingiza timu ambayo haina maandalizi ya kocha,natukubali matokeo yoyote.Habari kwamba hatuendi kuchukua kombe siyo sawa,nilazima tuendekushindana na siyo kushiriki.Haina maana kwenda kushiriki mashindano ukiwa unajua kabisa kwamba hauko kwenye hali ya kushindana.Pamoja na kupata mazoezi tunahitaji kuonyesha uwezo kama timu.Siungi mkono kujitoa lakini ukweli ni kwamba ratiba hiyo si nzuri na haiwezi kuisaidia timu. Wacha tushiriki kwa sababu ya kushiriki lakini inatakula kwetu.

Anonymous said...

Hivi Yanga wenzangu tukae tufikirie kwa Makini sio kuweka Jazba mbele tu...,
Haya mashindano ni ya kimataifa ni vizuri kama timu itapata mazoezi ..., lakini timu gani? Yanga... ambayo wachezaji 10 kati ya 11 wako ktk timu ya Taifa..., hapa utakuwa unabomoa sio kujenga michezo ya kujipa na kujipa mazoezi inaweza kupangwa ila sio katika Mashindano makubwa namna hii..., hapa wa kulaumiwa ni TFF kwa kuendelea kupanga ratiba mbovu...., timu ya Taifa inacheza tarehe 13 (Tena Sudan sio Dar) halafu mashindano Makubwa namna hii mnapanga yaanze tarehe 15 kweli hapo kuna viongozi? wachezaji wenyewe sasa hivi tunapoongea wako kambini warudi na watakuwa Kambini mpaka watakaporudi toka Sudan..., hawa ni binadamu vile vile wana wake na watoto huwezi kuwatoa sudan moja kwa moja ukawaweka katika mashindano mengine

Anonymous said...

KIngine mi sijawahi kuona Duniani Ligi inakuwa na break zaidi ya miezi Mitatu..., sielewi TFF wana maana gani kupanga ratiba ya namna hii..., kama walikuwa na muda mrefu hivi kwanini basi walichezesha mechi za ligi kila weekend na katikati ya wiki? Viongozi TFF jaribuni kuliangalia sana hili suala la Ratiba maana naona mnavuruga kila kitu....

Anonymous said...

Chunguzeni Timu zilizoendelea kama vile Chelsea, L/pool, Man Utd, Arsenal. Au hata Aston Villa na Tottenham.

Wana michuano ifuatayo karibu kila wiki:
1. Premier League (j'mosi au j'pili)
2.1 Champions leage (j'nne au j'tano)
2.2 Uefa Cup (j'tano au alhamis)

wiki amabzo hakuna champions league au uefa cup kuna michano ya ndani:
3.0 League Cup (Calling Cup) (j'nne, j'tano)
4.0 FA Cup j'mos/j'pili)

5.0 Kuna michuano ya kimataifa timu za taifa pia (euro/world cup) j'tano/j'mos.

Michuano yote hii timu hushiriki na wachezaji hucheza. Ndio maana ya kusajili wachezaji 30.

Yanga hawana sababu au kisingizio cha kujitoa. Mawazo yangu ya awali kabisa hapo juu yanaweza kusaidia jinsi ya kugawanya wachezaji. Naelewa mechi ya kwanza ndio yenye matatizo - wanaweza kuwa wamechoka ila kwa nini wasichanganye wachezaji wazoefu kidogo na wa kawaida wengi? Au waanze wa kawaida halafu kipindi cha pili waingize wazoefu watatu. Mechi ya pili wachezaji wote watakuwa wako fresh. Katika hali kama hii ndio ujuzi na vipaji vya walimu wa soka vinatakiwa waumize vichwa. Achieni makocha majukumu, viongozi kaeni ofisini -utawala. Mambo ya kandanda uwanjani achieni wataalamu wa timu, after all wachezaji wamesajiliwa kucheza na hii ndio kazi yao.

Anonymous said...

Nilisahau kuongeza hii point.

Mara zote washabiki wa Yanga huwa tunapenda mafanikio ya timu uwanjani. Timu imecheza na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa -ubingwa tunao na sasa tunaongoza ligi.

Inabidi tukubali kitu kimoja. Penda ua na boga lake!

Mafanikio huja na mambo kama haya, timu kushiriki michuano mingi. Kwa hiyo tuwe tayari kuendana na 'yanayotokana na mafanikio yetu'.

Mfano: Manchester United kutwaa ubingwa wa Uingereza na Ulaya imejiongezea michuano miwili ambayo timu nyingine za uingereza hazichezi: Super Cup ilichezwa Monaco na World Club Champions itachezwa kule Japan. Kwa hiyo itakuwa nyuma mechi 2 za ligi + mashindano mengine yote ya Uingereza.

Timu ikiwa bora na yenye mafanikio makubwa kama ilivyo Yanga, ni sifa (jambo la kujivunia) na heshima kubwa. Kwa hiyo inabidi sifa na heshima yetu tuiendeleze huko Tusker. Hayo ndio malipo ya mafanikio yetu Yanga -yaani kushiriki ktk michuano mingi!!.

Anonymous said...

Uamuzi wa kijinga wa Madega umebadilishwa.Timu itashiriki.Madega alikwenda kupiga bao na kuanza kutangaza uamuzi bila baraka ya kamati ya utendaji.Maamuzi ya kidikteta.

Anonymous said...

WALA TUSIJITOE WACHA WATOTO WAKACHEZE SOKA UWANJANI KWANI NI KAZI YAO HIYO WACHEZAJI WAPO 30 MAGOLIKIPA WOTE WAPO WASHAMBULIAJI WOTE WAPO

TENA MSISHANGAE TUKACHUKUA NA HILO KOMBE TENA TUKAZIDI KUVIKUSANJA VIKOMBE VINGI KRABUNI SAWA?

WACHENI UTOTO MADEGA KUIJTOA AKUNA MAANA YOYOTE HILE NI SAWA NA MTOTO KUKATAA KUNYWA UJI ETI KWASABABU ALIKUNYWA JANA UJI MWINGI!!!