Friday, December 26, 2008

CHAN 2009

Stars kundi moja na wenyeji

KUNDI A
IVORY COAST
ZAMBIA
TANZANIA
SENEGAL

KUNDI B
GHANA
DR CONGO
LIBYA
ZIMBABWE

14 comments:

Anonymous said...

Kwa maoni yangu kwa ujumla siyo mbaya sana. Kama tukipita kwenye makundi basi kuna uwezekano mkubwa tukacheza fainali kwa kundi B timu zote siyo tishio kwetu. Tunatakiwa tujiandae kwa mahesabu makubwa. Hata hawa Ivory Coast wachezaji wao wengi wanacheza nje kwa hiyo hawataweza kucheza mashindano haya na Senegal vile vile. Hapa ubingwa ni wetu na wenye wivu wajinyonge.

Anonymous said...

tusijiamini sana tuchukulie kila mchezo ni wa maaana.

Anonymous said...

Kundi gumu, lakini nadhani advantage kwetu ni kuwa tumeisha kutana na timu karibu zote, tumecheza na Senegal, Zambia, labda huyo Ivory Cost, kwangu mimi nadhani maandalizi ni kitu muhimu sana.

Anonymous said...

Kundi sio baya sana kwa tathimini ya haraka hasa ukizingatia kwamba wachezaji wote ni wa ndani kwa hiyo hakuna mjanja wa kumtisha mwenzake kwa u-professional wake, na pia sisi tuna faida kwani wachezaji wetu wamecheza pamoja muda mrefu kwa sababu hatuna professionals tofauti na wenzetu ambao kuna wachezaji wao ambao hawana uzoefu katika timu zao za taifa kutokana na kufunikwa na professionals kwa muda mrefu. Maandalizi yakiwa ya kutosha basi tunaweza kufanya vyema.


KILA LA KHERI TAIFA STARS ASANTE BLOG MANAGER KWA TAARIFA

Anonymous said...

Imekula kwetu

Anonymous said...

Wajameni,
Aliyeaga kwa mkwaju na aliyeaga kwa kura yupi ana unafuu??

Anonymous said...

ndugu mwenye blog hii tunakuomba waminye hawa wanaouliza maswali ya kitoto hii ni n blog ya wana yanga

Anonymous said...

Talib: Simba hawafundishiki
Clara Alphonce
ALIYEKUWA Kocha wa muda wa Simba, Talib Hilal amemaliza kwa malalamiko aliyeyaacha aliyekuwa kocha wa Simba Kasmir Benzinsk kuwa wachezaji wa Simba hawafundishiki.

Kocha huyo aliyasema hayo juzi baada ya Simba kutoka uwanjani na ushindi wa bao 3-2 dhidi ya timu ya Tusker ya Kenya katika mashindano ya Tusker ambayo fainali zake zilikuwa jana.

Talib alisema wachezaji hao wamekuwa wagumu sana kufuata wanayofundishwa na kocha wao wakiwa mazoezini na kucheza mchezo wanaoujua wao.

'' Wachezaji hao uwanjani wanacheza vizuri kwa muda mfupi muda mrefu wanacheza wanavyojua wao ndiyo maana unakuta kila mchezaji anacheza anavyojua yeye,'' alisema.

Pia, alisema wachezaji hao wanapokuwa mazoezini wanafanya vizuri mpaka wanampa matumaini ya kuwa wameiva lakini wakifika uwanjani hawachezi kama walivyofundishwa.

Aliongeza kuwa Simba ina wakati mgumu sana na aliwashauri viongozi wanapotafuta kocha wa kuinoa timu hiyo waakikishe wanatafuta kocha mzuri ambaye ataweza kuinoa Simba iliiweze kufanya vizuri.

Alisema timu hiyo siyo mbaya bali kuna makosa madogo madogo ambayo yanaweza kulekebishika kama wakimpata kocha mzuri ambaye atawanoa kwa muda mrefu.

Aliongeza kuwa wachezaji wengi wa Simba hasa wale waliopo kwenye timu ya taifa walikuwa wanalalamikia sana muda wa mapumziko na hicho anadhani ni tatizo ya timu za Simba na Yanga kufanya vibaya katika mashindano hayo ya Tusker.

Amewashauri TFF, kuzingatia muda wa wachezaji na mashindano yanayoendelea ili kuwapa muda wachezaji waweze kupata muda wa kupumzika na kujiandaa na mashindano mengine.

Anonymous said...

Hizo habari za SIMBA hapa za nini leta habari za Taifa Stars na Yanga Simba tafuteni blog yenu CM hebu ondoa hii takataka ..., kwanza wana bahati tumetolewa kwa shilingi ...
Leteni Habari za maendelea ya Klabu yetu simba wanafundishika au la pelekeni Msimbazi sisi hazituhusu wala hazitusaidii

Anonymous said...

habari za simba ni kama ushuzi hapa. anzisheni blogu yenu muiite Shimba shipoti.

Anonymous said...

Jamani tunaomba muweke picha ya Jengo letu tuone maendeleo ya Jengo and kiwanja. Nilikuwa Dar mwezi wa nane likizo, tuwekeeni picha ya Jengo letu tuone...

Jim
Canada

Anonymous said...

Wameanza kutimuana teana. Soma hii..
Gabriel atimuliwa, Obina asimamishwa Simba SC
Clara Alphonce

UONGOZI wa Klabu ya Simba umemsimamisha mshambuliaji wake wa kulipwa kutoka Nigeria, Orji Obina na kumtupia virago mkongwe, Emannuel Gabriel.


Habari za uhakika kutoka katika vyanzo vyetu na ambazo zilithibitishwa jana na uongozi wa klabu hiyo zilieleza kuwa uongozi wa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi umemsimamisha mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu.


Chanzo kimoja kilieleza kuwa mchezaji huyo amekuwa ni mtovu wa nidhamu, kitu ambacho kimewakela sana viongozi hao na kuchukua jukumu la kumsimamisha kwa muda usiojulikana.


Mnigeria huyo aliwahi kudaiwa kumshambulia aliyekuwa kocha wa klabu hiyo, Krasimir Bezinski katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa Ligi Kuu kwa amdai kuwa alikuwa akimnyima nafasi ya kuonyesha uwezo wake.


Hata hivyo, Obina mwaka huu aliripotiwa na gazeti dada la Mwanaspoti kuwa alitoroka kambini na kwenda kulewa pombe na kurejea akiwa chakari.


Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa uongozi huo umeamua kumtupia virago Gabriel kwa madai kuwa si mchezaji wao kwani tayari alishauzwa katika timu ya Fanja iliyopo Oman.


Hata hivyo, Gabriel ambaye inasemekana uongozi wa Simba umemuza kisirisiri lakini yeye amekataa kuuzwa huko kwa timu hiyo ambayo si chaguo lake.


Chanzo hicho kilieleza kuwa mchezaji huyo ameshauzwa Oman na tayari wameshatoa kibali cha kimataifa cha uhamisho (ITC) huku mchezaji huyo akiwa hajui chochote kinachoendelea.


Mwananchi ilipowatafuta viongozi w Simba kuthibitisha suala hilo ilifanikiwa kumpata mwekahazina msaidizi , Almas Chano ambaye alisema kuwa wa kuulizwa suala hilo ni Katibu Mkuu, Mwina Kaduguda.


Naye alipotafutwa, Kaduguda aliieleza Mwananchi kuwa apigiwe simu baada ya dakika tano na alipotafutwa baadaye alishauri atafutwe Katibu Mwenezi, Said Rubeya.


"Naomba mtafuteni katibu wetu mwenezi, amelitolea ufafanuzi, ataweza kuwaeleza kila kitu kwa uhakika," alieleza Kaduguda. Rubeya hakupatikana licha ya kutafutwa mara kadhaa.


Kwa upande wake, mwenyekiti wa klabu hiyo, Hassan Dalali hakupatikana pia kwenye simu yake.

Anonymous said...

CM tafadhali tunaomba utoe comments kuhusiana na simba hapa si mahali pake...., jamani tuheshimu privace, hapa ni YANGA sasa huyu mnyama anaweka ambayo sisi wana yanga tnajadili mambo habari zao hii sio haki

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___