Wednesday, December 10, 2008

TFF: Yanga tutaonana wabaya
Joseph Shikokoti

Klabu ya Yanga imeingia mkataba na wachezaji wawili wa kimataifa kutoka Kenya kwa ajili ya kukipiga katika klabu hiyo huku TFF ikiweka wazi kwamba muda wa usajili wa wachezaji wapya umekwisha tangu Novemba 30.

Wachezaji hao wawili ambao wameingia mkataba na Yanga ni walinzi Joseph Shikokoti na John Njoroge wote kutoka Tusker ya Kenya.

Hata hivyo wachezaji hao wanaweza kuongezwa katika usajili kwa ajili ya ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Yanga imepeleka majina 27 tu. CAF imeweka tarehe 30 Novemba kuwa siku ya mwisho kwa vyama vya Taifa vya soka kutuma majina kwa njia ya Fax au barua pepe. Na kufikia tarehe 15 Desemba vyama hivyo vinatakiwa kutuma nakala halisi 'Original' ya fomu za usajili za wachezaji wanaoombewa kuchezea vilabu husika katika michuano hiyo.

Je, Shikokoti na Njoroge wataichezea Yanga msimu huu?

5 comments:

Anonymous said...

Viongozi wetu kwa kupimana ubavu na TFF tu, hawajambo

Anonymous said...

kwanini tunakosa umakini kwa tunalolifanya?hizo fedha zimeenda.

Anonymous said...

Hizo fedha ni zako? Hata tukiwakosa kwenye ligi ila tutakuwa nao kwenye mechi za kimataifa. Kwanza kwenye ligi tuna timu ya taifa (taifa stars). Simba mpo?

Anonymous said...

Jamani simba wameshashtukia kuwa hawaingii nusu fainali, simba haiwezi kumfunga prison wala tusker mwaka huu wataacha mpira.

Anonymous said...

hahaa hizo fedha ni zako ok, sisi wanayanga wengine tunashindwa hata kutoa maoni ,tunatahamaki sana.samahani bro.