Sunday, December 21, 2008

Tusker Challenge Cup 2008

Yanga yaaga kwa kura
Mabingwa watetezi wa michuano ya Tusker, Yanga wameaga michuano hiyo baada ya kushindwa katika kura ya kuchagua timu zitakayoingia nusu fainali kutoka kundi A.

Timu za URA na Mtibwa Sugar zimefuzu baada ya wawakilishi wa vilabu hivyo kubahatika kuokota bahasha iliyokuwa na namba 1 na 2. Mwakilishi wa Yanga aliibuka na bahasha iliyoandikwa OUT.

Katika mchezo wa kukamilisha ratiba wa Kundi B uliomalizika jioni hii, Tusker na Simba zimetoka sare ya 0-0. Kwa hali hiyo timu hizo nazo zilikuwa zimelingana kwa pointi na magoli hivyo ilibidi irushwe shilingi ili kupata mshindi wa kwanza ambapo Tusker ilipata kura hiyo ya ushindi wa kwanza.


Inabaki kwamba Yanga OUT mpaka 2009.

19 comments:

Anonymous said...

Tumeaga kwa kujitakia.Tulitakiwa hata sare tukashindwa.Kusingizia kura ni kuficha ukweli.Tutafute kocha mzuri kama tunataka kuitoa Al Ahly ama sivyo tutaangukia pua tena.

Anonymous said...

Jamani mimi naijua Yanga vilivyo ndiyo maana nilishasema toka mwanzo haya mashindano hayatufai mwaka huu yanaweza kuzusha mgogoro mkubwa klabuni na wapumbavu wamshaanza mara mwenyekiti hafai, wengini Manji anafanya nini, na wengine kocha hafai, na upuuzi mwingine. Tusingeshiriki haya maneno yote yasingetokea na klabu ingekuwa tulivyu. Tulikubali kushiriki, tumefungwa, tukae membeni unafiki na makelele ya kijing jinga tuache.

Anonymous said...

Bado tunakazi kubwa mbele yetu yaani mashindano ya Africa, tufanye tathimini kujua udhaifu wa timu yetu na turekebishe ikiwezekana. Tuna ukosefu wa wafungaji ndugu zangu! akina Ambani, Mwalala, Barasa na Sunguti ni watu muhimu sana kama tunataka kutatua tatizo hili. Kazi ya Kocha ni kuongezea ujuzi na kipaji ambacho mchezaji tayari anacho na si vinginevyo! Tuwe wa kweli na tuache kujivunia bahati ambayo leo ipo kesho haipo - mwe macho haambiwi tazama!!!!!

Anonymous said...

Bila Ambani hamna magoli, hakuna kusingizia kula wala nini, jamani uwezo mdogo sana. Haya Kagoda FC

Anonymous said...

Hivi washabiki wa Simba hawana pa kusemea? Mbona wanaingilia uwanja wetu wa wana Jangwani?

Unknown said...

kocha mzuri sana hayo mambo yameisha tugangange yajayo nimeumia sana pole sana ]wana yanga wenzangu

Anonymous said...

Mimi bado nalalamikia soka la bongo kusema kweli hii ndio wanaita kura, hii ni kura au bahati nasibu? (lottary), hivi ni kweli bongo wameshindwa kutafuta creteria nyingine yeyote zaidi ya lottary?, mfano uingereza timu iliyoonyesha nidhani inapata nafasi ya kucheza EUFA cup directly hata ikiwa ya mwisho...? kwa hiyo timu zinajitahidi kutokuwa na kadi nyingi ..., ina maana timu zimefungana hata kadi za njano?..., Mchezo unapendeza ukiisha uwanjani mezani haileti ladha yeyote...., anyway wanaYANGA msife moja huo ndo mpira unadunda tujipange tumalize ligi vizuri na michuano ya Africa

Anonymous said...

tumeshindwa kuua panya sasa tunakwenda kuwinda tembo(ahly) watatukanyaga vibaya sana ,simba wanasifika sana kwa sababu hakuna mchezo wanaouzadharau kama yanga ,sasa mmeona hii ndio fundisho mimi nasema ndege aliye mkononi ni bora kuliko wawili walioko porini.

Anonymous said...

Kushinda na kushindwa yote ni sehemu ya matokeo. Hakuna sababu ya kutafuta mchawi, timu haikuwa na maandalizi ya kutosha, pampja na wacheza wengi walio timu ya taifa kukosa muda wa kupumzika.

Anonymous said...

wajinga nyie kagoda hakuna point mliyotoa ,ovyoooooooo

Anonymous said...

Jamani nasikia Simba kafungwa, je ni Kweli?

Anonymous said...

Wewe achana na Simba, sisi tumetolewa tuandae timu kwa ajili ya 2009...

Anonymous said...

Kagoda FC vipi jamani? mbona boss wenu kimya sana, mara kaumwa, mara nini, sasa jengo lenu ataliacha hivi hivi..... poleni sana wapenda vya bure

Anonymous said...

Simba kweli wameishiwa wanafungwa na timu mbovu namna hiyo tungecheza nao si wanhejinyea.

Anonymous said...

Simba wanatakiwa waandaliwe jeneza tu hawana lolote achana nao palapanda limshalia.

Anonymous said...

Simba wasubiri kipigo kingine toka kwa Tusker labda wasiingize timu uwanjani na baada ya hapo wasubiri kushuka daraja.

Anonymous said...

Ngoja niwaelezeni jinsi simba watakavyoshuka daraja. Kesho watapokea kipigo toka kwa tusker kitu ambacho kitasabisha wagombane kama kawaida yao. Pia kocha wao ingawa alikuwa kwa mwezi mmoja tu lakini inawezekana wakamfukuza jinsi walivyo wapumbavu na washenzi watupu. Wataangaika kutafuta kocha mwingine ambaye watampata chini ya wiki moja kabla ya ligi kuanza na atashindwa kuwaweka wachezaji pamoja kwa sababu magoigoi wao wengine watakuwa wanafundishwa mpira wa wachezaji wetu timu ya taifa. Mechi ya kwanza ya ligi watacheza na timu dhaifu ya Villa lakini watapata kipigo na hapo ndiyo itatangazwa rasmi timu imeshuka daraja kwani huyo kocha mpya atafukuzwa na kocha mkuu atakuwa Dalali. Habari ndiyo hiyo.

Anonymous said...

Talib: Simba hawafundishiki
Clara Alphonce
ALIYEKUWA Kocha wa muda wa Simba, Talib Hilal amemaliza kwa malalamiko aliyeyaacha aliyekuwa kocha wa Simba Kasmir Benzinsk kuwa wachezaji wa Simba hawafundishiki.

Kocha huyo aliyasema hayo juzi baada ya Simba kutoka uwanjani na ushindi wa bao 3-2 dhidi ya timu ya Tusker ya Kenya katika mashindano ya Tusker ambayo fainali zake zilikuwa jana.

Talib alisema wachezaji hao wamekuwa wagumu sana kufuata wanayofundishwa na kocha wao wakiwa mazoezini na kucheza mchezo wanaoujua wao.

'' Wachezaji hao uwanjani wanacheza vizuri kwa muda mfupi muda mrefu wanacheza wanavyojua wao ndiyo maana unakuta kila mchezaji anacheza anavyojua yeye,'' alisema.

Pia, alisema wachezaji hao wanapokuwa mazoezini wanafanya vizuri mpaka wanampa matumaini ya kuwa wameiva lakini wakifika uwanjani hawachezi kama walivyofundishwa.

Aliongeza kuwa Simba ina wakati mgumu sana na aliwashauri viongozi wanapotafuta kocha wa kuinoa timu hiyo waakikishe wanatafuta kocha mzuri ambaye ataweza kuinoa Simba iliiweze kufanya vizuri.

Alisema timu hiyo siyo mbaya bali kuna makosa madogo madogo ambayo yanaweza kulekebishika kama wakimpata kocha mzuri ambaye atawanoa kwa muda mrefu.

Aliongeza kuwa wachezaji wengi wa Simba hasa wale waliopo kwenye timu ya taifa walikuwa wanalalamikia sana muda wa mapumziko na hicho anadhani ni tatizo ya timu za Simba na Yanga kufanya vibaya katika mashindano hayo ya Tusker.

Amewashauri TFF, kuzingatia muda wa wachezaji na mashindano yanayoendelea ili kuwapa muda wachezaji waweze kupata muda wa kupumzika na kujiandaa na mashindano mengine.

Anonymous said...

Kondic na uongozi: Malumbano yenu ni mauti kwa Yanga


BAADA ya kuondolewa katika michuano ya Kombe la Tusker na kuutema ubingwa huo, ndani ya klabu ya Yanga kumetokea upepo mbaya uvumao kuinyemelea klabu hiyo na ambao kimsingi hauna mantiki ikizingatiwa kuwa timu hiyo kwa sasa inakabiliwa na changamoto kubwa mbeleni.
Ni wazi kwa yeyote mwenye akili timamu angefikiria kuwa uongozi na kocha wa Yanga Dusan Kondic wangeelekeza fikra na mawazo yao katika kukabili changamoto zilizo mbele yao.
Changamoto ya kwanza ni kuiandaa timu yao vyema kwa ajili ya michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mzunguko wa pili, uliopangwa kuanza Januari 10 mwakani, huku ikiwa inaongoza katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 30.
changamoto ya pili ni kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika mechi za michuano ya Klabu Bingwa Afrika mwaka huu ambapo wao ni wapeperusha bendera ya Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Yanga imepangwa kuanza na timu ya Etoile d’Or de Mirontsy ya Visiwa vya Comoro.
Mechi ya kwanza baina ya timu hizo itachezwa kati ya Januari 30 au 31 mwaka huu.

Lililo kubwa zaidi ni kwamba, endapo Yanga itafanikiwa kuwa kuwang'oa Wacomoro hao itakutana na kigingi ambacho ni timu ya Al Ahly ya Misri ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo la Klabu Bingwa.

Tofauti na changamoto hizi ambazo ziko wazi kwa mdau wa soka yeyote aliye ndani na nje ya Yanga, kumetokea malumbano ya chini kwa chini ambapo pande mbili yaani kocha Kondic na uongozi.
Kutolewa kwa Yanga Katika michuano ya Tusker na kuvurundwa kwa usajili wa wachezaji wao wa kimataifa John Njoroge na Joseph Shikokoti kunaonekana kuchukuliwa kama kiini cha kamtafaruku hako.
Yanga iliyopangwa katika kundi A na timu nyingine za URA na Mtibwa Sugar katika kipute cha Tusker ilishindwa kuingia hatua ya nusu fainali kwa kupigiwa kura ya 'Out' baada ya timu zote tatu katika kundi hilo kuwa na pointi zinazofanana na mabao ya kufunga na kufungwa.

Michuano hiyo iliisha kwa kwa Mtibwa Sugar ya Morogoro Tanzania,kuibuka mabingwa wapya .
Ni wazi wapo wanayanga walioghadhibishwa na kutofanya vizuri kwa timu yao.
Wegi wao waliwatupia lawama viongozi wao kwa kushindwa kukamilisha usajili wa wachezaji tajwa hapo juu ambao waliamini wangetumika katika michuano hiyo.

Hapa likaongezeka tena suala la mchezaji Mike Baraza ambaye kwa wakati huo alikuwa hajapata hati yake ya uhamisho wa kimataifa (ITC) kutoka timu ya Polisi ya nchini Malaysia.
Kwa sasa ITC ya Baraza imeshatua nchini na ataiwakilisha timu hiyo katika michuano yote iliyo mbeleni mwa Yanga.
Hata hivyo kimsingi hoja ya kukosekana kwa nyota hao haina msingi wowote katika kukosa ubingwa wa Tusker kwani timu hiyo inao nyota wengi wakiwemo wale walio katika kikosi cha timu ya taifa ambao walirejea kuitumikia klabu yao.
Hata hivyo msigano unaoonekana wazi kuwepo baina ya Kondic na uongozi kwa sasa , ni kitendo cha kocha huyo kuingia kichwakichwa kuwasajili Shikokoti na Njoroge ilihali dirisha la usajili lilikuwa limeshafungwa tangu Novemba 30 mwaka jana.
Wachambuzi wa masuala ya michezo wanajiuliza ni namna gani uongozi wa Yanga unafanya kazi na kocha wao na pia mamlaka za soka kama vile Shirikisho la Soka Nchini (TFF).
Kinachojidhihirisha hapa ni kukosekana kwa uwajibikaji na mawasiliano hafifu baina ya uongozi wa Yanga na benchi lake la ufundi.
Inaonekana wazi kocha Kondic anafanya baadhi ya mambo bila kuushirikisha uongozi na pindi yanapokuwa magumu anakimbilia kutoa kasoro za uongozi ambazo pengine si sababu ya kushindwa kwa jamb husika.
Tumeshaona majuzi baada ya kushindwa kuwasajili Njoroge na Shikokoti, kocha huyo ameripotiwa kuuponda uongozi wake kuwa bila ya uwepo wa mfadhili Yanga itakufa.
Hoja zake zina mantiki katika kipengele kimoja kwamba ni ukweli usiopingika kuwa uongozi wake umeshindwa kubuni vyanzo vingine vya mapato ukiacha utegemezi wa mfadhili.
Lakini hili halijaonyesha wazi kuwa ni sababu za msingi za kuwakosa nyota hao.
Ushauri wa bure kwa uongozi wa Yanga na Kondic ni kwamba huu si wakati wa kulumbana badala yake wakae chini na kuzikabili changamoto ikiwemo ya kuhakikisha wanatafuta namna ya kujikwamua kiuchumi kuliko kuendelea na mtindo wa sasa ambao mfadhili asipokuwepo kila kitu kinasimama.

Hawana sababu za kuulizana nani kakosea kwenye suala la wachezaji tajwa, bali waiandae timu vyema kwa ajili ya michuano ijayo.
Mashabiki na wapenzi wa Yanga hawatarajii kuona timu yao inaanza kwa kusuasua katika ligi duru la pili na katika Klabu Bingwa.

Kocha Kondic anatakiwa kusoma alama za nyakati, kwani tayari kuna wanaosema yeye anafundishiwa timu yake na Marcio Maximo kocha wa timu ya Taifa, Taifa Stars.

Hili limetokana na yeye mara zote kusingizia kuwa hawezii nkuweka mipango yake vyema kwani nyota wengi wako katika Stars.

Kondic ajue kwamba mhanga wa kwanza wa Yanga kufanya vibaya atakuwa yeye kisha uongozi.