Friday, January 16, 2009

Ligi Kuu ya Vodacom kuendelea "rasmi" kesho

Mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom ulioanza mwishoni mwa wiki iliyopita, unatarajiwa kuendelea "rasmi" kesho kwa mabingwa watetezi Yanga kupambana na wanajeshi wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa zamani wa Taifa Jijini Dar.

Yanga hadi ilimaliza mzunguko wa kwanza ikiwa kileleni mwa ligi hiyo baada ya kujikusanyia pointi 30 ikiwa imepoteza mchezo mmoja tu.

Michezo mingine iliyochezwa katikati ya wiki:

10 Jan. Polisi Dom vs Mtibwa Sugar........1 -1
Polisi Moro vs Kagera Sugar........3-0
11 Jan. JKT Ruvu vs Toto Africa........1-0
12 Jan. Moro Utd vs Azam FC................2-2
16 Jan. Villa Squad vs Prisons .............. 2-0

Kesho
Yanga vs JKT Ruvu 1-0
Mtibwa Sugar vs Kagera Sugar 2-1

Jumapili
Simba vs Polisi Moro

12 comments:

Anonymous said...

vipi huko mambo hayajaanza

Anonymous said...

Mpira ni mapumziko, bado 0-0

Anonymous said...

Timu yetu imepangwaje leo

Anonymous said...

Tunaongoza 1-0. Mfungaji Shamte Ally

Anonymous said...

Mpira umekwisha, tumeshinda bao 1

Anonymous said...

sasa mbona hamsemi timu ilikuwaje

Anonymous said...

ok man asante kwa matokeo na hongera vijana wa jangwani kwa ushindi ila ninaomba analisis ya mchezo kwa waliouona Mdau Cuba

CM said...

timu ilikuwa
1.Kaseja
2.Nsajigwa
3.Maftah
4.Ndhlovu
5.Nadir
6.Bonny
7.Ngassa
8.Chuji
9.Ambani/Shamte
10.Tegete/Mumbara
11.Makassy/Nurdin

Timu ilikosa utulivu katika umaliziaji kwani walikosa magoli mengi ya wazi.

CM said...

Katiks mchezo mwingine wa ligi uliopigwa leo, Mtibwa Sugar imeifunga Kagera Sugar 2-1.

Anonymous said...

Bwana CM Tunaomba utupatie msimamo ukoje kwa sasa,baada ya mechi hizi.

Anonymous said...

vipi Mnyama kafufuka leo?

CM said...

Simba leo imeshinda 3-2