Saturday, January 24, 2009

Ngassa akosa ulaji Norway
Mchezaji tegemeo wa Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania Mrisho Ngassa (19) amekosa ulaji katika klabu ya Lov- Ham ya Norway baada ya dau dogo lililotolewa na timu hiyo kukataliwa na Yanga.

Baada ya klabu ya Yanga kukataa kumruhusu mchezaji Ngassa kwenda Norway kwenye klabu ya Lov-Ham Football kuwahi usajili wa dirisha dogo, uongozi wa Lov-ham Football uliamua kuachana na Ngassa na kumchukua Mcameroon a mbaye ndiye atakayewahi ulaji huo uliokuwa dhahiri kwa Ngassa.

Lakini juhudi za wakala wa Ngassa kuwashawishi Lov-Ham wawe na subira na waongeze pesa zaidi ya kiasi walichokubali awali cha Dola 50,000 za malipo kwa Yanga. Lov-Ham wamekubali kuwa na subira lakini wamekataa kuongeza pesa kwani wanaamini 50,000 USD ni nyingi kwa mchezaji wa Kitanzania kutokana na ukweli kwamba hapajawahi kutokea mchezaji wa Kitanzania kufanikiwa katika mpira wa kulipwa Ulaya hivyo basi kumchukua Ngassa ni kama kucheza mchezo wa bahati nasibu.

Lov-Ham wamekubali kwa sharti jipya kwamba laziwa iwe mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao na safari hii atalazimika kafanyiwa majiribio kwani hakuna tena ulazima na uharaka wa kuwahi dirisha dogo kutokana na Mcameroon kuchukua nafasi ya Ngassa

Tayari Lov-Ham wameuandikia uongozi wa Yanga kama walivyoelekezwa na wakala wa Mrisho Ngasa anayetambuliwa na FIFA Yusuf Bakhresa


SOURCE: Mtibwa Website

11 comments:

Anonymous said...

Viongozi wamwache Ngassa akajaribu bahati yake. Hela sio kila kitu, ni bora akacheza Norway kwa hela ndogo kuliko Sudan hata kama wanatoa hela nyingi.

Anonymous said...

Kumbukeni kwa Ngassa mpira ni ajira yake. Sasa wewe hapo juu unaweza kufanya kazi bila malipo? HIvi ukimuweka Nani wa Man na Ngassa nani ana kiwango kikubwa? Ngassa lazima aende timu kubwa kwa hela nyingi.

Anonymous said...

someni hii habari hapo chini eti atalipwa millioni 144 kwa mwaka. Wanapokuambia millioni 144 hapo hawajatoa tax, insurance etc. hela atakayochukua ni chini ya millioni 50 kwa mwaka. Dili ya Sudan ni bora zaidi.
-----------------------------------
Saleh Ally
IWAPO uongozi wa Yanga ungetoa ruhusa kwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Mrisho Ngassa angefanikiwa kujipatia kitita cha zaidi ya Sh milioni 432 katika kipindi cha miaka mitatu.

Klabu ya Ligi Daraja la Pili ya Lov-Ham ya Norway iko tayari kumlipa mshahara wa dola 10,000 (shilingi milioni 12) kwa mwezi kwa kipindi cha miaka mitatu na huenda ingeongeza kiwango kama angepata mafanikio.

Iwapo Ngassa angepata ruhusa kujiunga na timu hiyo, bila ya marupurupu angekuwa anapata kitita cha shilingi milioni 144 kwa mwaka hiyo inamaanisha kwamba kwa miaka mitatu alikuwa na uhakika wa kitita cha shilingi milioni 432 au zaidi.

Ilielezwa kwamba baada ya wakala huyo kuwasiliana na uongozi kulieleza suala hilo mwamuzi wa mwisho ni mfadhili wao mkuu, Yusuf Manji kwa kuwa ndiye anayesajili wachezaji.

Mwanaspoti ilifanya juhudi za kumpata Manji aliyerejea nchini hivi karibuni kutoka Marekani lakini simu yake ilikuwa imezimwa.

Hadi jana mchana tiketi ya Ngassa ya kuondoka kwenda Norway ilikuwa katika ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam lakini imeelezwa hakukuwa na maelewano mazuri kati ya uongozi wa Yanga na wakala wake, Yusuf Bakhresa.

Habari za uhakika zimeeleza kwamba, klabu ya Lov-Ham ilikuwa tayari kutoa kitita cha dola 50,000 (zaidi ya sh milioni 60) kwa Yanga ili imuachie mchezaji huyo kwenda Norway.

Mchana kutwa Mwanaspoti ilimsaka Ngassa bila ya mafanikio kutokana na simu yake kuwa imezimwa, ila ilifanikiwa kumpata Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega aliyekiri kupokea taarifa za mshambuliaji huyo chipukizi kutakiwa na klabu ya Norway lakini akasisitiza suala la kufuatwa kwa utaratibu.

"Kweli niliwasiliana na wakala na akaniambia kwamba Ngassa anatakiwa Norway na tayari tiketi iko ubalozini. Lakini hivi tunaweza kufanya biashara ya mchezaji haraka bila ya kufuata taratibu namna hiyo?," alihoji Madega jana kutoka Nairobi, Kenya.

"Nimemwambia tunataka tukutane na klabu hiyo, tufanye amzungumzo kuhusu suala la Ngassa na baada ya hapo tutamuachia, sisi hatuna tatizo, mbona Ivo Mapunda na Said Maulid wameuzwa kwa kufuata utaratibu. Sidhani kama njia ya kumuuza mchezaji kupitia wakala bila ya viongozi wa klabu kuwa ni sahihi.

"Hapo hatujajua iwapo Ngassa atakuwa anauzwa klabu nyingine, Yanga itafaidika vipi. Hilo ni suala la kufuata utaratibu na kuwa na mikataba ya uhakika badala ya kufanya mambo kwa haraka tu," alisema Madega.

"Hatuna kinyongo, wala msituhukumu, tuko tayari kumuuza mchezaji yeyote lakini utaratibu ufuatwe na wanaotaka mchezaji wa Yanga basi wawasiliane na kukutana na viongozi wa Yanga ili tumalizane kiutaratibu jamani," alisisitiza Madega.

Habari zimeeleza kwamba, Lov-Ham ilikuwa tayari kutoa kitita hicho cha dola 50,000 kwa kuwa wachezaji wengi wa Afrika iliowachukua hawana mafanikio.

Lakini uongozi wa klabu hiyo ukasisitiza kwamba uko tayari kuweka kipengele ambacho kitatoa nafasi ya kuongeza kiwango cha malipo ya mchezaji huyo.

Wiki iliyopita, Mwanaspoti ilifanya mawasiliano na Kharthoum, Sudan na kupata taarifa namna ambavyo Ngassa ni lulu nchini humo huku klabu kubwa za Al Hilal na El Merreikh zikionyesha nia ya kutaka kumnasa katika dirisha la usajili la mwezi Juni.

Klabu hizo zimeonyesha nia ya kumchukua kwa dau kubwa zaidi kuanzia dola 160,000 kutoka kwa Al Hilal huku El Merreikh wakiwa tayari kutoa kitita cha kuanzia dola 400,000 (zaidi ya Sh milioni 450).

Mshambuliajia huyo, ambaye ni mtoto wa zamani wa mchezaji wa Simba, Khalfan Ngassa na Pamba ya Mwanza �TP Lindanda� ameonyesha kuwa lulu kubwa kutokana na uwezo wake uwanjani anapokuwa na Yanga pia timu ya taifa, Taifa Stars.

Ngassa ni tegemeo kubwa la Taifa Stars katika michuano ya Kombe la CHAN itakayoanza mwezi Februali nchini Ivory Coast.

Anonymous said...

mwacheni ngasa akajaribu bahati norway,hizo habari za timu za sudan ni za magazeti tu,kama kweri wanamwitaji kwa 160,000usd mbona hatujawaona kuja kwa uongozi wa yanga au tff ?zaidi ni uzushi tu wa magazeti,ila hao wanorway wameonyesha niha hasa,kwa akili za kawaida tu hakuna timu dunia hii inaweza kutoa kiwango hicho kwa mchezaji wa kitanzania ,nchi ambayo aina hata mchezaji wa daraja la 4 ulaya,tunajidanganya tu ,ngasa aende norway afungue milango kwa wengine ,sudan ni kupoteza muda wake tu na uwezo wa kununua mchezaji kwa pesa hizo hawana wakijitaidi mno ni usd 10,000

Anonymous said...

Mzee CM, Naona umejisahau tena habari ni zile zile za Simba na Villa? Chemka baba.
Ndugu wana Yanga wenzangu kwa nini tunakuwa na haraka na mambo hivi? Mimi inanishangaza kidogo kuona jinsi tunavyo yachukulia mambo. Kwa nini swala la kuuza mchezaji linakuwa ni issue hata kutaka kulifanya kwa namna ya zima moto? Mimi ninavyo jua timu ina taka kununua mchezaji kutokana na uwezo wake binafsi na si swala la kuwahi au kuchelewa. Mchezaji yeyote mwenye uwezo atanunuliwa na timu yoyote si kwa kuwahi wala kuchelwa. Ikiwa mchezaji hana uwezo hatakama mtamuuza haraka haraka kama wengi wanavyo dhania ataenda kushindwa na kurudi. Mifano ipo mingi ya waliofikiri wamefanikiwa kumbe viwango vilikuwa chini. Kama kweli Ngasa anakiwango kinacho kubalika hajanyimwa ulaji kama ambavyo wengi wemeanza kusema ulajiwake upo pale pale, tena kwa timu kubwa kuliko hata hizo zinazotajwa. Kwamba mchezaji wa Tanzania hawezi kuuzwa kwa $400,000 inaweza kuwa kweli na pia isiwe kweli kwani hilo linategemea mambo mengi, kwa hiyo jibu lake siyo rahisi hivyo. Mimi nafikiri Ngasa aongeze bidii katika kazi yake atapata mafanikio makubwa.Hawa wanaotaka mambo ya zima moto sidhani kama wanamsaidia huyu kijana, msingi ni uwezo wake tu ndio utamsaidia. Inaonekana Tanzania tunajirahisi mno katika kile kinachoitwa kuuza wachezaji ndio maana wanakwenda jioni kesho asubuhi wamerudi. We are also expensive,uwezo wetu utuonyeshe kwamba nasi ni wa gharama na si mitumba.

Anonymous said...

Kinachotokea ni kutaka kumvuruga kijana na timu kwa ujumla , mashabiki wa AC Millan juzi juzi waliandamana kupinga kuondika mchezaji wao KAKA si bure kwa kuwa wanaamini kuwa ndio chachu ya ushindi kwenye timu , sio siri kwamba Ngassa ni chachu ya ushindi kwa sasa sio Yanga tu hata kwa Taifa ( simaanishi kwamba azuiwe moja kwa moja ), tukumbuke kwamba mwezi ujao tunakwenda Ivory Coast dunia nzima itatupia jicho pale kwa mtazamo wangu ni mahala muafaka kwake na wachezaji wengine kuonyesha uwezo wao ambao utawafanya wapate mikataba ya uhakika moja kwa moja badala ya hii ya kwenda kufanya majaribio kwanza na dau pia linaweza kuwa zaidi ya hilo la Norway
halafu na tujiulize Henry Joseph tunaambiwa naye amepata timu huko huko lakini yeye taratibu zote zimefuatwa na ataenda huko mwezi ujao iweje Ngassa atakiwe kwa spidi ya haraka kiasi hicho
Namshauri kijana atulie afanye kazi nyota yake iko juu akafanye mavituz yenye akili Ivory Coast matunda atayaona KAMA IPO IPO TU

Anonymous said...

kweli mzee,KAMA IPO IPO TU,klabu na klabu ndio zinafanya mawasiliano,sio wakala anakurupuka tu kuja kumtaka mchezaji akitumia here says.Haikubaliki duniani kote hii.NGASA na uongozi wa YANGA wawe makini sana na hili muda huu na hasa timu inapoelekea kwenye mashindano makubwa ya klabu bingwa afrika.

Anonymous said...

kweli mzee,KAMA IPO IPO TU,klabu na klabu ndio zinafanya mawasiliano,sio wakala anakurupuka tu kuja kumtaka mchezaji akitumia here says.Haikubaliki duniani kote hii.NGASA na uongozi wa YANGA wawe makini sana na hili muda huu na hasa timu inapoelekea kwenye mashindano makubwa ya klabu bingwa afrika.

Anonymous said...

Wana yanga tuwe makini sana akati huu ambapo adui yetu hana mbinu nyingine zaidi ya kutuvuruga kwa njia yoyote ile ili tuanze kuvutana na kuvuruga mipango yetu , walianzia kwa makocha na wachezaji mara makocha na viongozi ili mradi tu watimize lengo lao na mbinu kubwa wanayotumia ni waandishi wao hasa wa magazeti ambao sio siri ni wengi

Anonymous said...

Mechi ya leo vipi matokeo?

Anonymous said...

yanga oyeeeeeeee