Tuesday, February 10, 2009

Yanga yaigomea TFF
Wakati TFF inaiandaa Timu ya taifa ya Tanzania - Taifa Stars kwa ajili ya fainali ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN), klabu ya Yanga imekataa kutoa wachezaji wake 10 walio katika timu hiyo mpaka hapo watakapomaliza mchezo wa marudiano wa kombe la klabu bingwa Afrika dhidi ya Etoile ya Comoro.
Yanga ambayo katika mchezo wa kwanza dhidi ya timu hiyo iliiangusha kisago cha mabao 8-1, inatarajiwa kucheza mchezo huo wa marudiano siku ya Jumapili lakini taratibu za usafiri zinaonyesha kwamba ndege ya kurejea nchini itatua siku ya Jumatano.
Awali, TFF iliiomba Yanga isiwapeleke wachezaji wake ambao wapo katika Taifa Stars kwa vile Yanga inaonekana kama vile ipo mguu mmoja ndani ya raundi inayofuata, kwani hata isipokwenda na wachezaji hao haiwezi kupoteza mchezo kwa kufungwa 7-0.
Je, wadau kitendo cha Yanga kuigomea TFF ni sawa?

4 comments:

Anonymous said...

yanga wako sawa kabisa, huwezi kumdharau adui yako ni mwiko

Anonymous said...

Tungewapeleka tu akina Mwaikimba & Co ili nao waweze kuiwakilisha Yanga kwenye michezo ya Kimataifa.

Anonymous said...

Matokeo ya stars na Zimbabwe vipi? Leteni habari hizo!

Anonymous said...

0-0 stars -zimbabwe