Saturday, January 31, 2009

Yanga kuua leo?
Yanga leo inaanza kampeni ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika kwa kuivaa Etoile d’or de Mirontsy ya Comorro katika mchezo wa kwanza wa raundi ya mtoano utakaochezwa Uwanja wa Taifa, jijini, Dar es Salaam.

Inatakiwa kuibuka na ushindi mkubwa ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele, kabla ya mchezo wa marudiano utakaofanyika Moroni, Comorro katika wiki mbili zijazo na kuingia katika raundi ya kwanza, ambapo watakutana na bingwa mtetezi, Al-Ahly ya Misri.

Hata hivyo Yanga inapewa nafasi ya kuibuka na ushindi mkubwa kutokana na rekodi mbovu walio nayo Wacomorro katika michezo ya Afrika. Ila cha kuzingatia kwa Yanga leo ni kutodharau mechi hiyo kwani ikumbukwe kwamba mpira unadunda.

Tusubiri dakika 90 za mpambano huo, kila la heri Yanga ya Tanzania.

35 comments:

Anonymous said...

Tunaongoza bao 1

Anonymous said...

thanks, mdau kwa kutpatia matokeo kwa muda unaofaa kabisa,endelea kutufahamisha jinsi game itakavyokwenda.thanks

Anonymous said...

Wamerudisha ktk dk 20.

Bao ni 1-1

Anonymous said...

lete muda, dk ngapi? matokeo?

Anonymous said...

matokeo vipi? bado dk ngapi?

Anonymous said...

bado dk 15.bado ngoma 1-1.wacomoro ni wazuri n wanajihami

Anonymous said...

matokeo vipi mkuu?dk ngapi bado?

Anonymous said...

Mpira umekwisha Yanga 8 wa-Comoro 1. Wafungaji wa magoli ya Yanga:
1.Boniface Ambani
2.Jeryson Tegete
3.Ambani
4.Ndhlovu
5.Tegete
6.Ambani
7.Mrisho NGASSA
8.Ambani

Anonymous said...

ahsante mkuu hii ndio habari ya ukweli yulikuwa tunaingoja hongera wana yanga uzi huo huo mwaka huu hata ahliy tunataka afungwe

Anonymous said...

Hongera Yanga,wachezaji,viongozi,na wafadhili,na wapenzi wote,
sasa matayarisho yaanze kwa Al Ahli,hapa tayari tunapita,huyu mnyama al ahli anatusumbua sana kila tukikutana nae,yaani hatujawahi hata mara moja kumfunga,sasa ni zamu yetu kuanza kujipanga hivi sasa ili tuweze kumbamiza ,commoro hio mechi iliyobakia ya marudiano tunakwenda kucheza friendly game kwaajili ya kujitayarisha na kukutana na al ahli,matayarisho yaanze mapema kwa kumuua huyu mnyama,na mashindano ya chan yatasaidia wachezaji wetu watakao kenda huko kuzidi kuwiva kwa mechi za kimataifa na kumsubiri al ahli,
hongera sana dar yanga

Anonymous said...

CM lete matokeo rasmi mzee!

Mdau, M.E., UK

Anonymous said...

Tatizo lililopo ni kwamba mechi ya ahliy imekaa vibaya sana. Sisi tuna wachezaji wengi timu ya taifa na mechi hiyo itapigwa siku tatu baada ya mashindano ya Ivory Cost kuisha. Kama tukitolewa mampema basi tutakuwa na wiki nzima. Advantage moja tuliyokuwa nayo ni kwamba tunaanza kwao.
Pamoja na mafanikio yote tuliyoyapata miaka miwili iliyopita bado kuna watu wanaamini kocha hafai. Sasa sijui wanataka tupate kocha ambaye atatufanya tufungwe. Ubingwa wa Afrika ni wetu tu.

Anonymous said...

Naona mtambo wa magoli Ambani umepona sasa.

Anonymous said...

ambani anaongoza kwa ufungaji african champions league, sio tu ligi ya hapo nyumbani,na atazidi kuwakimbia wafungaji wote wa africa ktk mechi ya marejeano.

ambani best striker african

Anonymous said...

Hawa wa-Ngazija walishauriwa wakubali tu tucheze mchezo mmoja Dar yaishe, wakajifanya wanakomaa eti lazima turudiane. Wametumia haki yao ila wanajitia gharama bure, wangefanya tu kama wenzao AGSM waliokubali wakafungwa 5-1 yakaishia Dar kimya kimya. Kile kisingizio cha kukosa uwanja wenye hadhi ya kimataifa Comoro nafikiri bado kipo kama wangetaka kukitumia. Ila Yanga waanze kufanya mazoezi kwenye mahandaki maana hawa jamaa uwanja wao nasikia...

Anonymous said...

timu ilikuwaje

Anonymous said...

du hii kali sana hongera sana wana wa jangwani kwani mmenipa raha sana wembe huohuo mpaka watu wanywe sumu mwaka huu duu hii safi sana mdau cuba

Anonymous said...

Hawa wanataka watupotezee muda tu waombe yaishe kwani wataingia gharama za bure.

Anonymous said...

we wacha tu,hii sio kutupotezea muda,hii ni kupeleka kikosi cha pili ili kizowee mechi za nje,wakirejea wale wa chan,watakuwa hawa nao wamepata mazoezi ya kuondoa woga,hii safi sana, yanga sasa ni timu kubwa,inafaa mazoezi yao wakajipime nguvu sasa na timu za europer,au timu kubwa za asia,ili kuiweka kimataifa,
vipi mkuu jengo letu linaendeleaje?na uwanja unaweza kututumia picha kwa hapa ili tujisikia na sisi tulio mbali,thanks
yanga-damu-EU

Anonymous said...

Wadau mliopo Bongo tupeni ripoti kamili ya mchezo ilikuwaje pamoja na kikosi kilichotoa dozi hiyo kama vile dawa mseto ya malaria...lol. Mechi ya marudio bi kushusha kikosi cha pili cha kina mwaikimba, n.k nao wamalizie hiyo asusa waliyoianza wenzao.
mfurukutwa wa Yanga, USA

Anonymous said...

Halafu kuna watu wengine akili zao zinawatuma eti tumuuze Ngassa wa millioni 60. Mpira wa Ngassa amemzidi Nani wa Man Utd kwa hiyo bei yake ni zaidi ya Nani.
Halafu watu lazima waelewe Yanga siyo kituo cha kukuza vipaji, tunafanya biashara kwa hiyo kama kuna mtu anamtaka Ngassa lazima atoe hela inakayorudisha hela yote ya usajiri na ujenzi wa uwanja. Uwanja umetugharimu zaidi ya millioni 800 na hiyo ndiyo iwe bei ya Ngassa.

Anonymous said...

mnyama mbadoo leo kabanwa 1-1 na JKT Ruvu

Anonymous said...

kuna matokeo yoyote ya mechi ya leo?mkuu tupatie habari za huko tz

Anonymous said...

kuna matokeo yoyote ya mechi ya leo?mkuu tupatie habari za huko tz

Anonymous said...

yanga imeshinda goli moja mfungaji tegete soma ktk mwananchi

Anonymous said...

MATOKEO YA LEO HAYA HAPA
http://mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=9770
Ni kama tushakua mabingwa hatuwezi kukosa pointi 6 katika michezo saba hayo yatakua maajabu ya 9 ya dunia.
Mfurukutwa wa Yanga USA

Anonymous said...

sasa huu ubingwa uonekane kwa kuwa moja ya timu kali africa,sio kila siku tunakuwa bingwa baadae africa siku zote tunakuwa ni kama timu ya commorro, timu zote africa zipo fiti, hata vinchi vidogo vya ruanda,burundi ,uganda,na nyinginezo wanakuwa wamekomaa ktk mashindano ya nje,sisi mpaka sasa hatujui kama ni wakongwe wa mashindano,inabidi timu yetu ielewe na kuwakomalia timu za huko juu ya africa,sisi ni wakongwe kama wao, sasa wacha tuone mwaka huu,naamini tutabadilika,hasa baada ya wachezaji wetu wengi kuwa wameonyesha kukomaa kiasi na timu ya taifa, nadhani safari hii hatutokuwa kama timu ya mchangani tukikutana na ahlali ya misri

Anonymous said...

YANGA BINGWA 2008-2050

Anonymous said...

kwa msimamo wa ligi kongoa hapa
http://www.fifa.com/associations/association=tan/nationalleague/standings.html

Anonymous said...

Aisee nimegundua haya magazeti yanataka mgogoro uanze jangwani. someni hii, eti sisi hatupo kwenye timu zenye mpira wa kuvutia sasa sijui tunashindaje. Na magori yote bora kwenye ligi tumefunga sisi.


Simba sasa kama Arsenal
Na Saleh Ally
UKITAKA kuona mchezo wa kuvutia na kukufurahisha, hakuna shaka kuwa unatakiwa kuangalia jinsi Simba wanavyocheza mechi zao za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kama ulizoea kuiona timu ya taifa ya Zambia, ikicheza mpira wa kuvutia na samba la uhakika, sasa kocha Patrick Phiri maarufu kama 'piriton' ameleta soka hilo Msimbazi. Tena, beki wa kati Juma Nyoso amekuwa ni kivutio kikubwa huku akiwa anatuliza mpira, kupiga chenga na kupanda kana kwamba ni kiungo wakati ni beki wa kati.

Lakini la muhimu zaidi ni kwamba mechi nne za Simba katika Ligi Kuu Bara chini ya Mzambia Patrick Phiri zimetosha kumaliza kazi aliyoifanya kocha wa Bulgaria, Krasmir Bezinski aliyetimuliwa.

Katika mechi 11 za mzunguko wa kwanza, Simba ilishinda mechi nne tu, ikafungwa tano na kupata sare mbili ikiwa imepata mabao 11 ya kufunga na kufungwa mabao 13 hali ambayo ilionyesha safu ya ushambuliaji ilikuwa butu na ile ya ulinzi ilikuwa nyanya.

Lakini tangu kocha wa Zambia atue na kuiongoza timu hiyo kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, Simba imeshinda mechi tatu kati ya nne za ligi na kutoka sare moja, pia imetoka sare nyingine katika mechi ya kirafiki dhidi Zesco ya Zambia.

Katika mechi hizo, Simba imeshinda dhidi ya Villa Squad mabao 2-0, Polisi Morogoro (3-2), Prisons (3-1) na mwisho sare ya mabao 1-1 dhidi ya JKT Ruvu. Sare nyingine ni ya bao 1-1 dhidi ya Zesco ya Zambia. Takwimu zinaonyesha, katika mechi hizo tano ikiwamo ya Zesco, Msimbazi wameshinda mechi tatu na kutoka sare mbili huku washambuliaji wake wakiwa wameweka rekodi ya kutotoka bila bao katika mechi zote.

Simba imefunga mabao 10, imefungwa matano hali inayoonyesha kasi ya wafungaji ni nzuri huku safu ya ulinzi ikiwa inahitaji marekebisho na kocha huyo ameliona hilo.

Phiri raia wa Zambia, amefanya mabadiliko makubwa haraka katika kikosi hicho wiki zisizozidi sita tangu akichukue kikosi hicho hasa katika uchezaji, kuanzia beki, kiungo na ushambuliaji safu ambayo tangu ametua nchini.

"Kweli safu ya ulinzi bado, ni kazi ya kurudia na kukumbushana najua baada ya muda fulani wataelewa. Watacheza vizuri na imani tufanya vizuri tu," alisema Phiri, ambaye amewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Zambia, 'Chipolopolo' aliyofanikiwa kuivusha hadi Kombe la Mataifa Afrika nchini Ghana.

Kocha huyo aliyewahi kuinoa Simba kwa vipindi viwili tofauti na kuifanya kuwa tishio Afrika Mashariki na Kati amesema anataka kuendelea kuiunganisha timu hiyo kwa uhakika zaidi ingawa anapata wakati mgumu kufanya hivyo huku wakiendelea na ligi.

Aliiambia Mwanaspoti kuwa, katika kipindi ambacho ligi imesimama kupisha maandalizi ya Taifa Stars kwenda CHAN, ataendelea kufanya maandalizi na wachezaji wake waliobaki.

Kiuchezaji, hasa kutumia idara zote kwa pasi nyingi za uhakika zaidi, [b]Simba inaweza kuwa inaongoza kwa pasi na mpira wa kuvutia ikifuatiwa na JKT Ruvu na Moro United.[/b]

Anonymous said...

waseme watakayo bingwa ndie atawakilisha nchi msijiumize vichwa na hao wanga

Anonymous said...

Waache wachonge tuu. Msimamo ndio huo. Mkuu CM naomba utuwekee front page kama utaweza. Huyo Allu Saleh ameamua kuandika kwa unazi bila facts!


Rnk Team MP W D L GF GA +/- Pts
1 Young Africans 15 14 0 1 31 5 26 42
2 Kagera Sugar 15 8 2 5 15 12 3 26
3 Simba SC 15 7 3 5 20 17 3 24
4 Prisons 15 6 4 5 15 19 -4 22
5 Mtibwa Sugar 15 6 3 6 20 14 6 21
6 JKT Ruvu 15 5 6 4 20 19 1 21
7 Toto African 15 6 3 6 15 17 -2 21
8 Azzam United 15 5 3 7 17 19 -2 18
9 Moro United 15 3 6 6 22 20 2 15
10 Polisi Morogoro 15 3 6 6 15 19 -4 15
11 Villa Squad 15 4 2 9 12 30 -18 14
12 Polisi Dodoma 15 0 8 7 8 19 -11 8

Anonymous said...

simba hamuoni aibu kusoma na kuweka comment zenu kwenye blogu hii iliyoandikwa kwa rangi za njano na kijani?
CM nakuomba uweke msimamo wa ligi juu kabisa na iwe kila mtu anapokuja bloguni aione kwanza kabla ya kuweka comment

Anonymous said...

Mmeona Nipashe ya leo tena? Lazima wana yanga tuwe makini na hawa wachonganishi.
http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2009/02/09/131304.html

Wanataka sasa wawagombanishe wachezaji na viongozi halafu tuanze kufungwa. Mwaka huu mlie tu hata mseme nini sisi wana yanga tunauamini uongozi wetu mpaka uchaguzi mwingine utakapofanyika. Wapumbavu kweli hawa wahandishi wa habari. Na wewe Mengi itabidi tukufikirie kwenye uwanachama wa klabu yetu yaani mwanayanga mwenzetu lakini unakubali habari za uchanganishi ziweke kwenye vyombo vyako vya habari!!!! Hata kama ni ugomvi wako na Manji ni hukohuko mmanilzani msiihusishe klabu yetu ilikuwepo kabla ya hata nyie kuzaliwa.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___