Tuesday, January 27, 2009

Yanga uwanjani leo

Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu ya Yanga leo inashuka dimbani kuikaribisha Mtibwa Sugar ya Turiani, mechi itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi hiyo ya raundi ya 14 tangu kuanza kwa Ligi Kuu Agosti 22 mwaka jana, inatarajia kuwa na upinzani wa hali ya juu huku kila timu ikitaka kuibuka na ushindi. Yanga inaongoza ligi kwa kufikisha pointi 36 baada ya kushinda mechi 12, kufungwa mchezo mmoja, huku ikiwa haijatoka sare.

14 comments:

Anonymous said...

Tumeshinda 1-0

CM

Anonymous said...

iingize hii blog yako kwa issa michuzi blog sports, kwani ndio blog inayotumiwa na mamilioni ya wa TZ waliopo nje na ndani ya nchi, sio wengi wanao itambua hii blog yako, watambulishe wale wapenzi wa Yanga wanaoishi nje kufatilia habari za Yanga kuto blog hii,
mimi nimeiiona kwa bahati tu hii blog hata ilikuwa haifahamiki kabisa ktk jamii ya wa tz waliopo nje.
mdau-Holland

Anonymous said...

Asante sana kwa kutupa matokeo kwa haraka,CM! Yanga ni mwendo mdundo.
Mdau,Italia.

Anonymous said...

we mdau wa holland siku zote hizo ulikuwa wapi? labda siyo yanga. wenzio matokeo yote ni hapa. hata huyo michuzi siku hizi kazidiwa na biashara hata stori zake zinachelewa. na hata haya matokeo ya yanga sijui kama utayaona huko.
wana yanga tunaifahamu blog hii. hata kama hatufiki milioni

Anonymous said...

wewe hii blog imeanza 2007 leo 2009 ndiyo unaijua. Ukiiweka kwa michuzi watu watatuvamia hapa kama umeijua kaa kimya au mtonye mwanayanga mwenzako.

Anonymous said...

kweli wazee hakuna haja ya kuiweka kwa michuzi hii ni blog ya wana yanga na kwakua tunajuana huwa tunajulishana, ukiiweka kwa michuzi itageuka kuwa kama ze utamu na kutuletea uchaafu humu ndani hasa mashabiki wa simba kwani wengi wao ni kina kayumba shule hakuna kazi kutukana tu.
HONGERA YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO

Anonymous said...

Hongera wachezaji , makocha na uongozi kwa ujmla kwa kuendeleza vipigo hakuna kuchafua rekodi mwaka huu hata kama wale jamaa zetu wameshatangaza kunawa mikono kuhusu ubingwa . Pongezi za binafsi kwa bwana mdogo Ngassa kwa kuwafikishia ujumbe murua kwamba upo na utaendelea kuwanyanyasa maana walishatangaza ooohh katoroka hajulikani aliko mara aichefua Yanga n.k Kwa ujumla dogo umewashika

Masebe said...

Huyu mtu wa Holland siyo mwana yanga, hii blog imejieleza wazi ni kwa ajili ya wanayanga kupashana habari halafu anataka ipelekwe wapi tena, sisi wenye nayo tunaifahamu vizuri wa ndani na nje na tuna itumia sana.Tunakuomba bwana CM usikubali mawazo hayo.Nafikiri hatuhitaji mamilioni ya watanzania bali maelfu ya wanayanga wenye nia moja na nguvu moja.

Anonymous said...

Ubingwa wanukia Yanga

BAO pekee lililofungwa na winga machachari wa Yanga, Mrisho Ngassa lilitosha kuipa timu yake ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.

Kwa ushindi huo, Yanga imefikisha pointi 39 na kuzidi kuukaribia ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.

Mpira ulianza kwa Mtibwa kucheza kwa utulivu huku wakifanya mashambulizi yenye mpangilio.

Dakika ya pili, Uhuru Selemani wa Mtibwa aliingia na mpira katika eneo la hatari na kumpasia Zahoro Pazi ambaye, akiwa yeye na kipa Obren Cirkovic, alipiga shuti lililombabatiza kipa huyo na kuwa kona butu.

Yanga walijibu shambulizi hilo mnamo dakika ya nane na kupata bao pekee lililofungwa na Ngassa baada ya kupokea pasi ya Ben Mwalala.

Mwalala alipiga mpira mrefu kutoka winga ya kulia na mabeki wa Mtibwa kuzubaa, wakidhani kipa wao Shaban Kado angeutokea mpira huo na ndipo Ngassa akauwahi na kufunga.

Baada ya bao hilo, Yanga waliendelea kucheza kwa nguvu huku Mtibwa wakionyesha kupoteza uelewano walioanza nao.

Mwalala alipata nafasi ya kufunga dakika ya 44, lakini kabla hajafunga aliunawa mpira huo na mwamuzi Methew Akrama wa Mwanza kumpa kadi ya njano.

Kipindi cha kwanza Mtibwa walifanya mabadiliko kwa kumtoa David Mwantobe na nafasi yake kuchukuliwa na Yusuph Mgwao.

Yanga walikwenda mapumziko wakiongoza kwa bao hilo moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya shambulizi kali, lakini beki wa Mtibwa Chacha Marwa alikuwa imara na kuokoa.

Yanga waliwatoa Athuman Iddi na Mwalala na nafasi zao kuchukuliwa na Mkenya Mike Baraza na Abdi Kassim.

Dakika ya 62, kona ya Abdi Kassim iliunganishwa kwa kichwa na Nadir Haroub lakini mpira uligonga mwamba wa juu na kuokolewa na mabeki wa Mtibwa.

Mtibwa walipata kona dakika ya 67 iliyopigwa na Yusuph Mgwao na kuunganishwa na Abdalah Juma, lakini mpira ukiwa ukielekea nyavuni, kipa Obren akaokoa.

Mtibwa nao walifanya mabadiliko mengine kwa kuwatoa Pazi na Abdalah Juma na nafasi zao kuchukuliwa na Omari Matuta na Salum Ussi.

Yanga walilisakama lango la Mtibwa na mnamo dakika ya 73 Baraza alipewa mpira mrefu na Shadrack Nsajigwa na kumpiga chenga Salum Swed na kupiga shuti lililomgonga kipa Kado na kuokolewa na mabeki wa Mtibwa.

Dakika ya 81, Shamte Ally aliipasua ngome ya Mtibwa na kuingia ndani ya eneo la hatari na kufumua shuti lililopaa juu.

Dakika nne baadaye, Mtibwa walijibu shambulizi, lakini Omari matuta akipewa pasi na Salum Swed kufunga akapaisha juu.

Kocha wa Mtibwa Sugar Salum Mayanga aliyapokea matokeo hayo kwa masikitiko huku akiwabebesha lawama washambuliaji wake kwa kushindwa kuzitumia vema nafasi walizopata.

Kwa upande wa kocha wa Yanga Dusan Kondic, alimlaumu mwamuzi Akrama na kumwita mmoja wa waamuzi wanaoua soka hapa nchini.

Vikosi

Yanga: Obren Cirkovic, Shadrack Nsajigwa, Nurdin Bakari, Wisdom Ndlovu, Nadir Haroub, Godfrey Bonny, Mrisho Ngassa, Athuman Iddi/Mike Baraza, Boniface Ambani, Ben Mwalala/Abdi Kassim na Shamte Ally.

Mtibwa Sugar: Shaban Kado, Meck Maxime, Idrisa Rajab, Chacha Marwa, Salum Swed, Shaban Nditi, Zahoro Pazi/Omari Matuta, Rashid Gumbo, Abdallah Juma, Uhuru Seleman na David Mwantobe/Yusuph Mgwao

Anonymous said...

Wembe huo huo, hongereni wachezaji na benchi zima la ufundi, mmeonesha consistency ya kueleweka.

Golini siku hizi akisimama JKJ au Obren hamna tofauti, saafi saana.

Kuhusu Ngassa, namshari kama itawezekana asubiri finals za CHAN kabla ya kwenda kufanya majaribio. Akipata performance nzuri CHAN, anaweza kupata timu ya ligi kuu ulaya bila hata kujaribiwa.

Namtakia mafanikio mema.

Anonymous said...

Jamani vp mnyma leo??

Anonymous said...

Wakuu mnyama vipi? Katoka kweli leo? Na bado hukumu yao nyingine Jumapili kwa JKT Ruvu lazima wachumbiwe tu, si mnajua kocha Kilinda ni mnazi wa Yanga kuliko hata Imman Madega lazima awape moto wachezaji wamchinje mnyama.... hehehehe

Anonymous said...

WAMEWAOTEA WAFUNGWA WAKASHINDA 3-1

Anonymous said...

Mimi niko UK na naifahamu hii blog kwa muda mrefu sasa. Pia huwa natuma maoni yangu mara kwa mara.

Kwa hiyo sio kweli kuwa walioko nje ya nchi hawaifahamu hii blog! Na hakuna haja kuipachika kwa Michuzi. Tujitangaze wenyewe kama mtandao wa wana Yanga.

Vipi kuhusu hatma ya kipa m-Serbia kucheza ligi ya mabingwa Afrika jamani?