Tuesday, March 10, 2009

Ambani arejea kuikabili Al Ahly
Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Boniface Ambani amerejea nchini tayari kwa maandalizi ya kuikabili Al Ahly ya Misri katika pambano la ligi ya Mabingwa ya Afrika iatakayopigwa Jumapili ijayo huko Cairo Misri.

Ambani aliruhusiwa na uongozi wa klabu ya Yanga kwenda kufanya majaribio kwa siku sita katika klabu ya Zhejiang Greentown ambayo inashiriki katika ligi kuu ya China.

Mchezaji huyo aliyesajiliwa na Yanga msimu huu, amefunga mabao matano katika Ligi ya Mabingwa Afrika na ni tegemeo kubwa kwa timu hiyo ya Jangwani katika mechi dhidi ya Al Ahly.

No comments: