Wednesday, March 25, 2009

Ngassa atacheza West Ham?


Kuna habari kwamba kiungo wa pembeni wa Yanga na timu ya taifa, Mrisho Ngassa atapata kazi kubwa kupata kibali kitakachomwezesha kucheza soka la kulipwa nchini humo.

Ngassa anatarajiwa kuondoka nchini mwanzoni mwa mwezi ujao kwenda kufanya majaribio katika klabu hiyo ambayo hata hivyo kwa sheria za soka la kulipwa la Uingereza, itakuwa vigumu kwake kupata kibali cha kukipiga nchini humo.

Ili mchezaji wa kulipwa aweze kupata kibali cha kucheza huko Uingereza, kama atatoka katika nchi zilizo nje ya Jumuiya ya Ulaya basi nchi yake inatakiwa iwe katika nafasi ya wastani isiyopungua ya 70 katika viwango vya FIFA kwa miaka 2 na anatakiwa ndani ya miaka miwili awe ameshiriki katika kikosi cha kwanza cha timu ya taifa kwa 75%.

Ndugu wadau hebu tusaidiane katika hili, kama kuna mtu mwenye ufahamu kuhusu masuala haya ya work permit za wanasoka katika ligi za UK atufahamishe.

Wakati huo huo, mashabiki wa klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza ya West Ham United wameanza kumzungumzia kiungo wa pembeni wa Yanga - Mrisho Ngassa. KWa habari zaidi hebu cheki hapa

5 comments:

Anonymous said...

Yes, Sheria hiyo hipo, lakini pia mchezaji anaweza kupata kibali hata kama nchi yake haipo katika nchi ya Viwango vya Fifa, kumbe West Ham wanafahamu hilo ndiyo sababu wamemuita kwaajili ya majaribio. Mimi naweza tu kusema kuwa Ngassa akaze buti, nimeona mechi chace akicheza, hapa wanaangalia sana Stamina na uwezo wa kumiliki mpira na maamuzi ya haraka.

Anonymous said...

Tunamtakia Ngasa majaribio mema na afuzu.Kijana an uwezo wa kufanya vizuri, wana Yanga wote tumuombee afanikiwe itakuwa ni kutangaza jina la klabu yetu huko ulaya kama ilivyokuwa kwa Nonda Shaaban.

Anonymous said...

Tunamtakia Ngasa majaribio mema na afuzu.Kijana an uwezo wa kufanya vizuri, wana Yanga wote tumuombee afanikiwe itakuwa ni kutangaza jina la klabu yetu huko ulaya kama ilivyokuwa kwa Nonda Shaaban.

Anonymous said...

Ni kweli kuna masharti kama hayo, ila W/Ham wanaweza kumsajili halafu wakampeleka kucheza (loan) klabu yoyote ya Ulaya kwa mwaka au miwili halafu wakamwombea work permit kucheza premier league.

Mifano; yule mchezaji wa man united kutoka china alipelekwa Royal Antwerp ya ubelgiji(?) kwa miaka 2 halafu akaombewa work permit akapata ila kwa sasa amerejea china.
Manucho wa Man Utd alisajiliwa halafu akapelekwa Panathinaikos ya Ugiriki kwa miezi 6, kisha akaombewa viza.
Kina Rafa na Fabio wa Man Utd walipewa work permit lakini hawajacheza timu ya taifa ya brazil -ila nao walisubiri zaidi ya mwaka mmoja kuweza kupata viza tena timu yao ya Fluminese hawakuwachezesha kipindi chote hicho walichokuwa wanasubiri w/permit.

Wachezaji wengi wa Arsenal kutoka Afrika Magharibi walipitia klabu za ulaya ndipo wakapata nafasi kuombewa w/permit premier league.

Kwa hiyo njia rahisi ya Ngasa kupata w/permit UK, ni kwanza kupelekwa loan ktk klabu za bara la ulaya ndipo itapokuwa rahisi kupewa w/permit baada ya muda mfupi.

nuganyizi said...

MUNGU SAIDIA KIJANA APATE CHANCE.