Thursday, March 19, 2009

Yanga kurejea Ligi Kuu leo
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, timu ya Yanga leo wanarejea kwenye ligi ya nyumbani kwa kukutana na Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Yanga ambao wamerejea mwanzoni mwa wiki hii wakitokea nchini Misri ambako walikwenda kucheza na Al Ahly kwenye mchezo wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kupoteza, wataingia uwanjani leo kwa lengo la kumalizia machungu yao kwa vijana wa Polisi Morogoro katika mchezo huo wa Ligi Kuu.
Mchezo huo wa leo utakuwa ni wa kwanza kwa Yanga baada ya ligi hiyo kusimamishwa kupisha ushiriki wa timu ya taifa kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN) iliyomalizika mjini Abidjan, Ivory Coast hivi karibuni ambao ndiyo wanashikilia usukani wa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 42.

18 comments:

CM said...

mpira umekwisha kwa ushindi wa 1-0 lililofungwa na Boniface Ambani kwa penati.

Kwa ushindi huu Yanga sasa inahitaji pointi moja tu ili kuweza kutetea ubingwa wake.

Anonymous said...

hayo magoli ya ligi ndiyo mnayoweza wangojeni wamisri wakutunguweni, tena sio 3 zitakuwa nyingi mtakuona mayanga mnadhani pesa zinacheza mpira panya nyie

Anonymous said...

hilo linalia nafasi ya pili, hupati panya wewe unaona yanga watapata mamilioni ,wewe ujitapetape tuu fukara wa kutupwa jalalani.

Anonymous said...

hivi uyo msenge wa simba anatoka wapi kwani wao wanashindwa kutengeneza blog yakwao mpaka waingilie ya kwetu?

Anonymous said...

Jamani nauliza:
Uwanja wa Uhuru ndio ule wa Taifa wa Zamani???

Anonymous said...

huo ndo uwanja wa taifa wa zamani aka shamba la bibi...

Anonymous said...

acheni maringo wachezaji wenu wanaondoka ligi ikisha.kaseja anarudi simba kupitia african lyon.yanga mtabomolewa sasa.hahaha

Anonymous said...

na waende kwani wameleta maendeleo gani ?,na wewe mbumbumbu tuu huna hela.

Anonymous said...

mbumbumbu mama yako.kwani wewe mwenyewe hela unayo?kuingia uwanjani unaruka ukuta.mkekwisha ndo maana hasira hizo.

Anonymous said...

Haya habari ndiyo hiyo, Mnyama kapigwa....kwa mahesabu ya haraka tayari tumekuwa mabingwa, kingine mnyama hata nafasi ya pili anaweza kuikosa....bado anakutana na Azam, Kagera Sugar....halafu anakutana na wanaume (Yanga)

Anonymous said...

habari hiyo ni ya kweli naona kipanya kametulia sasa

Anonymous said...

haya jamaa karudi kichwa kichwa hata hana aibu.sasa simba vipi? jee ile nafasi muhimu atapata ?

Anonymous said...

Mnjama kaliwa moja moro apo kazi ipo msimbazi

Anonymous said...

wazee msikae kujipotezea wakati tanzania mpira hamna tusijidanganye,si yanga wala simba hamna hata tim moja ya maana

Anonymous said...

kweli kabaisa kaka uliyasema hapo...mpira Tanzania ni wa kujidanganya na ubabaishaji tuu...hakuna kitu....mepoa tuuuuuuuuuuu

Anonymous said...

sasa nyie mnaosema Tanzania hamna mpira mnakuja kufanya nini kwenye blog inayoongelea mpira wa tanzania? Semeni tuu ukweli kuwa hakuna mpira msimbazi, msitake ku-generalise mambo hapa, ebo!

Anonymous said...

Simba ikifanya vibaya hakuna mpira..., Jamani mpira ni burudani na sisi wapenzi tunafurahia timu zetu zikifanya vizuri katika level tuliyonayo..., hivi wewe kama unaishi mjini unafedha na una magari ya kifahari.., je wale wakulima vijijini una haki gani ya kusema hawaishi wewe tu ndio unaishi?.., yote maisha.., walio Uingereza wacha wafurahie Kabumbu yao na sisi huku kwetu tujifariji na tulichonacho. kama ni Mpenzi wa mpira utafurahia tu hata mpira wa mchangani amboa nao una washabiki wake.
Ikipangwa mipango mizuri with time nasisi tutapanda panda. kwani Africa nzima bado hakuna Mpira sio Tanzania tu.

Anonymous said...

huyo mwehu anayesema mpira hakuna ni baada ya kuona mipira mingine aache watu wafurahie soka lao hata kama ni chandimu...au hujui kama watu wa mwanza walikua wakiamini hakuna jengo refu zaidi ya Bugando sasa wewe kama ulienda Dar ukaona kitega uchumi usiende kuwaambia watu wa mwanza eti mwanza hakuna ghorofa huo ni ujinga na na ufinyu wa fikra zinazoongozwa na ulimbukeni. Ujinga mtupuu. Hebu waachaneni watanzania wafurahie mpira wao bwana...tusiwe watu wa kuponda kila kitu kama wanasiasa wanaoahidi kuhamishia bahari mlimani na kujenga madaraja pasipo na mito wala korongo.
Nakuunga mkono mdau hapo juu, hawa ndio watu wanaokwenda Ulaya, akimpata mzungu anaanza ooh Africa hakuna wanawake, na mama ako ni nani, NYANI? Eboooooo!