Thursday, April 23, 2009

Mrisho Ngassa

Amefuzu au la?


Kumekuwa na habari za kuchanganya kuhusu majaliwa ya mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngassa aliyekwenda kufanya majaribio katika klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza ya West Ham United.Hapo awali kulikuwa na habari kwamba Ngassa alikuta kundi kubwa la wachezaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakitafuta nafasi ya kufuzu kuchezea "Wagonga nyundo" hao wa London, hivyo nafasi yake ilikuwa na ushindani mkubwa.Baada ya hapo kumekuwa na habari kwamba amefuzu hatua ya kwanza ambayo itaamuliwa kesho Ijumaa huku wengine wakisema ameshindwa kwenye majaribio hayo.Mlio na habari za uhakika tunaomba msaada tafadhali. Je, Ngassa amefuzu au la?

12 comments:

Anonymous said...

Hapana Ngasa ameshindwa, nadhani labda nchi za Belgium Ngasa anaweza kufuzu, lakini Ligi ya hapa hapana

Anonymous said...

Geof na wengine,ishu ya website ya klabu yetu imeishia wapi?,maana imekuwa kimya sana.Kama vp tupeni maendeleo.Kazi njema

Anonymous said...

ligi ya u.k sio kama inatisha kama,ngasa uwezo unaokabisa,ufupiwake ni kama shaun right philips,au jamein de foe,kasi na stamina uwezo huo anaokabisa kama wataamua kweli kumsajili,musiwe na mawazo kuwa ligi ya hapau.k hawazi kucheza,sometimes nchi anayotoka mchezaji pia inakuwa inaleta utata ktk kumchukua mchzaji,ngasa uwezo wa kucheza ligi popote anao musidanganyike ila kunakuwa na mambo fulani fulani ambayo wachezaji wetu huko hawatayarishwi tokea wadogo,hayo ndio baadhi ya wataalam wanayoyaangalia,sio chenga na kwenda mbio tu bila mpangilio ambapo huko nyumbani ndio big deal,hata akikosa west ham uwezo kama atapatiwa timu nyingine hata akina sunderland na za juu yake akina portsmouth uwezo anao

Anonymous said...

Geoff tunaomba ututafutie habari za uhakika kuhusu Ngasa. Kwa sasa hakuna habari ya kueleweka, awali nilisikia mchambuzi wa masuala ya michezo wa BBC Israel Salia akieleza kwa uhakika kwamba Ngasa ameshindwa majaribio, lakini tena ikasikika kwamba bado anaendelea na inaonekana hivyo kwa sababu wiki imeisha,jamani ukweli uko wapi? Geof nakuamini sana huna habari zozote?

MASEBE

Anonymous said...

ukweli ni kwamba Ngasa ameshindwa majaribio, atafika bongo leo mchana

Anonymous said...

hapa iliombwa kwa wale wenye habari za uhakika lakini wote mmeishia kutoa maoni yenu tu.
sasa mwenye habari za uhakika atuambie na atoe ushahidi wa anayosema, kwa mfano atuoneshe habari hizo kazipata wapi ili wenye nia ya kufuatilia zaidi wafanye hivo,

Anonymous said...

OK. Ya Ngasa yameisha, kwa bahati mbaya mimi siwezi kuwa kama mtu ambaye alikuwa anachukua habari kwa michuzi wakati mechi yetu na watani inaendelea na kujifanya yuko uwanjani... ahahaha
Turudi sasa kwenye mradi wa DECI aka website ya klabu. Mimi binafsi ningependa kujua ni mbeguy ngapi tunatakiwa tupande...

Anonymous said...

mshindi wa pili ni nani? tupeni matokeo ya mechi za leo

Anonymous said...

mnyama kachukua nafasi ya pili.kashinda 2-0
mechi yetu haikuchezwa kwa sababu mvua kali imenyesha.
mechi kuchezwa jumatatu

Anonymous said...

Leo hakuna updates kwa michuzi na hapa hatujamuona akibandika kitu chochote. Ahsante sana mdau hapo juu kwa kutujulisha matokea ila ningependa kujua kama website yetu itakuwa inategemea uopdates toka kwa michuzi au la...

Mliakuvana said...

Someni Michuzi blogspot kwa zaidi kuhusu Ngassa. Ukweli ni kwamba hakufanikiwa kuchukuliwa na West ham ila watamualika afanye nao mazoezi during the off season na pre-season wakienda huko Italia. I think thats good maybe watampachika katika affiliate timu yao moja madaraja ya chini kwa kumsubiria - agewise bado advantage ipo kwake.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___