Wednesday, April 22, 2009

Sahau Kambi afariki dunia

Kipa wa zamani wa klabu ya Yanga, Sahau Kambi amefariki dunia jana jioni baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kambi ambaye aliidakia Yanga kwenye miaka ya mwishoni ya 80 alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tumbo ambalo lilisababisha alazwe KCMC na baadaye kuhamishiwa Jijini Dar es Salaam ambako alifariki dunia huko Tandika nyumbani kwa baba yake.

Kipa huyo aliichezea Yanga kwa umahiri mkubwa hadi akafanikiwa kutwaa nafasi katika kikosi cha timu ya Taifa - Taifa Stars. Hata hivyo umahiri wa Kambi uliingia dosari mwaka 1988 katika mechi ya mwisho ya ligi kati ya Simba na Yanga ambapo wapenzi wa Yanga walimtuhumu kuiachia Simba kupata bao la ushindi lililofungwa na John Makelele. Simba ilishinda 2-1, ushindi ambao uliiokoa Simba kutoshuka daraja.

Marehemu atazikwa kesho saa 7 huko Tandika Jijini Dar es Salaam.

2 comments:

kibunango said...

Mungu amlaze mahala pema peponi...Daima utakumbukwa!

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___