Saturday, April 04, 2009

Pasipo 4-0, kwaheri


Mabingwa wa soka wa Tanzania bara Yanga leo wanarudiana na mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika Al Ahly katika mchezo wa pili wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Yanga inahitaji ushindi wa mabao 4 -0 au zaidi ili kuwavua ubingwa magwiji hao wa Afrika, kwani wiki 3 zilizopita Yanga ilifungwa 3-0 Jijini Cairo.

Katika kikosi cha Yanga cha Yanga leo hii mchezaji pekee ambaye hatacheza ni Kiggi Makassy ambaye ana malaria lakini wachezaji wengine wapo fit kukabiliana na Al Ahly. Wadau wengi wamekuwa wakipiga debe mlinda mlango Juma Kaseja akae langoni leo ili kama timu hiyo itailazimisha Al Ahly kwenda kwenye matuta basi watatumia uhodari wa Kaseja katika uokoaji wa penati.

Kwa upande wa Al Ahly wao watawategemea sana akina Mohamed Barakat, Flavio na Aboutrika katika kuhakikisha wanasonga mbele.

Timu itakayosonga mbele leo itakutana na mshindi kati ya AS Douanes ya Senegal au Kano Pillars ya Nigeria.

Majibu ya mambo yote haya tutayapata baada ya saa 11 leo jioni. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Yanga.

17 comments:

Anonymous said...

lengo la kuwachezesha kwenye jua kali la saa 9 limekwama. Mvua inanyesha Dar leo

Anonymous said...

LOLOTE LINAWEZEKANA KTK SOKA, HAKUNA ALIEDHANIA AGENTINA ATAKULA BAO 6-1 KWA BOLIVIA,PAMOJA NA KUUJUA MPIRA LAKINI UNATEGEMEA PIA NA BAHATI IMEANGUKIA KWA NANI KIUPANDE MWINGINE KWAHIO TUNATARAJIA VIJANA LEO WATAKUWA FITI NA TUTAWEZA KUWAFUNGA HAWA WA MISRI

Anonymous said...

kikosi cha leo
1. Kaseja
2. Nsajigwa
3. Nurdin
4. Ndhlovu
5. Haroub
6. Owino
7. Ngassa
8. Abdi
9. Ambani
10. Baraza
11. Chuji

Anonymous said...

Mzee hapo juu nakubaliana na wewe, lakini siyo timu yetu. Nilifanyikiwa kuona mechi mbili za timu nilipokuwa Tanzania, uwezo wetu bado, unajua tunacheza na timu bora, jamaa wanafahamu sana mbinu za mpira na sisi tunaingia kichwa, kichwa tu. wewe angalia jamaa walifanya booking ya hotel hata kabla ya mechi yetu ya kwanza tuliocheza huko kwao... mimi naipenda sana Yanga na nitaendelea kuipenda, lakini kwa timu yetu kuwafunga waarabu goli nne....ni kitu ambacho hakiwezekani...napenda tu kuwa mkweli kwenye hili

Anonymous said...

tumelambwa goli moja tayari

Anonymous said...

Kwa mpira watu wa Tanzania Yanga hawachomoi leo pamoja na kwamba wapo nyumbani. Ushindi kwa Yangani kishapo cha mabao chini ya 3. Mpaka sasa mmeshabonyezwa kimoja nabado.....

Anonymous said...

kazi kweli kweli, tuanzishe ligi yetu ya mabraiwe nchi hizi Comoro, Zanzibar na Somalia ha ha ha maana hata Burundi na Rwanda hatuwawezi, si timu ya Taifa si vilabu uchafu mtupu. Maneno mengi kama mwanamke mwenye bikira

Anonymous said...

Wazee waliahidi Al Ahly itajuta kutujua.Mpira bado huenda ahadi za wazee zikatimia.Wizi mtupu kuamini uchawi wakati mpira unatupiga chenga.Tukubali tumezidiwa full stop tuache mpira wa magazetini na kwenye redio.

Anonymous said...

mpira umekwisha tumefungwa 1-0

Anonymous said...

tena kufungwa 1 bora maana walijuwa wanakuja tembea sio kucheza mpira poleni ma yanga ngojeni ligi yenu muwe club bingwa wa tanzania hapo ndiyo mwisho wenu. bado mna mipira yakina kitwana manara ama kweli mmelala,

Anonymous said...

kodik kocha wenu alishawaambia kuwafunga waarabu haiwezekani ,mkaanzaa kumtukana ,YANGA MABINGWA WA KUBORONGA HAHAHAHA,MMEKULA KIDUDE CHA MKWEZI KIMYAAA.

Anonymous said...

wewe hujui mpira,ktk mpira kuna kufungwa,al ahly ni timu ambayo kiwango chake umekiona miaka miwili iliyopita wanacheza ligi ndogo ya mabara ya dunia kule japani, akina manchester bingwa wa europer na wengine, kama yanga wakiwatoa al ahli inamaanisha kiwango cha yanga watakuwa wapo tayari kucheza na timu kubwa kama manchester ,au barcelona kama kiwango cha ahli wanavyowakilisha africa, ukweli ni kuwa kiwango cha jamaa ni kikubwa, lakini hakuna timu hata moja wanaosema tunakwenda uwanjani kufungwa,nilazima uwe na moyo wa kushindwa, real madrid timu tajiri duniani kapigwa nyumbani 1-0, na ugenini liverpool 4-0, kwajio ndio soka, mwakani Yanga watajipanga tena, na watakuwa wachezaji wamesoma vya kutosha kutokana na hizi game zao,na watazidi kuelewana na wanaweza kuendelea vizuri siku za mbeleni,

Anonymous said...

unajidai miaka ya mbele utafanya vizuri hebu tukumbushe siku gani yanga ilfika japo robo fainal kama simba? bora simba inarecodi nzuri toka miaka hiyo kila anaepangwa na simba anajuwa anacheza na nani sio yanga, ukweli yanga ni mbovu tena sana, tunalia wakubwa wanaiba pesa za wa tanzania wanapeleka yanga kukuza majina yao kwa hesabu ya wanyonge,

Anonymous said...

Yanga ilifika robo fainali mwaka 1998

Anonymous said...

Mkatiaaibu kwa kufungwa sita na Raja Casablanca .

Anonymous said...

hao yanga ni sawa nawauza nyanya hawachoki kupiga kelele bado hawajakubali kama tim yao ni mbovu pia nashauri viongozi wa soka tanzania jaribuni kutafuta wazalendo hao wachezaji wakulipwa hawana mpango ama kweli vichekesho eti mchezaaji wakulipwa anatoka kenya huo kama si usenge ni kitu gani?

Anonymous said...

wewe mjinga hapo juu,tunaongelea miaka ya mbele wewe unaulizia miaka ya nyuma,hakuna mtu anaeishi kwa iliyopita,ww unaishi hivi sasa kwa leo na kesho,iliyopita haifutiki tena,unaangalia yanayokuja,