Saturday, April 18, 2009

Yanga vs Simba

Huku ikiwa tayari imetwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu huu, Yanga itaingia uwanjani Jumapili kupambana na watani wao wa jadi Simba katika mchezo wa ligi hiyo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Simba inahitaji ushindi katika mechi hiyo ili ijiweke katika mazingira mazuri ya kutwaa nafasi ya pili ambayo itaiwezesha kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na kombe la Kagame.

Yanga itacheza mchezo huo bila wachezaji wake wawili ambao walishiriki katika mchezo wa kwanza baina ya vilabu hivyo. Wachezaji ambao hawatakuwepo ni Mrisho Ngassa aliyekwenda Uingereza na Obren Circkovic aliyekwenda Austria. Adiha kwa upande wa Simba Musa Hassan Mgosi alitarajiwa kuondoka jana kuelekea India na Victor Costa ambaye yupo Msumbiji.

Tayari zengwe limeanza kuhusu pambano hilo ambapo Simba wameonyesha wasiwasi wao baada ya TFF kubadilisha mwamuzi mwanzoni mwa wiki hii. Pambano hil sasa litachezeshwa na Israel Nkongo badala ya Oden Mmbaga ambaye amepangiwa majukumu mengine na CAF mwishoni mwa wiki hii.

Kivutio kikubwa katika mechi hiyo ni uwezekano wa Juma Kaseja kuidakia Yanga dhidi ya timu yake ya zamani ya Simba. Kaseja alihamia Yanga akitokea Simba kwa uhamisho unaoaminika kugharimu shilingi milioni 60.

Mara ya mwisho vilabu hivi vilipokutana, Yanga iliibuka na ushindi wa 1 - 0 lililofungwa na Ben Mwalala.

Tusubiri filimbi ya mwamuzi tuone.

35 comments:

Anonymous said...

Mchezo utakuwa mgumu sana, nadhani sale itakuwa nzuri sana kwetu, majamaa yamebadilika sana, pia yamejiandaa kwa mchezo huu. Tuombe Mungu, Chelsea tumefanya vizuri, nategemea Yanga tutafanya vizuri pia,

Anonymous said...

Ngassa amefeli majaribio West ham jana

Anonymous said...

Yeah walikuwa wengi sana, haya tungoje matokeo ya leo, naungana na mdau wa kwanza, majamaa yatakuwa yamejiandaa sana, halafu yamekamilika, sale kwetu itakuwa nzuri tu

Anonymous said...

Jamani msiwa waoga kiasi cha kuombea sare, yaani hamna imani na timu yenu kiasi hiki!!!!!!!

Anonymous said...

tupe matokeo jamani

Anonymous said...

ha! ha! ha! Kumbe mlishachungulia TV ya Babu!!Lunyasi 1, Yeboyebo 0. Rodondo keshafanya mambo huko. Msife moyo lakini mpira ni dk 90

Anonymous said...

hawo ni mashabiki wa simba mimi nasema simba mmeumia tuu,

Anonymous said...

Sema tu kaka mdomo mali yako! wenzako uwanjani wanaomba mpira uishe na wengine wanaomba suluhu,angalia wenzako hapo juu wamesemaje!!!!

Anonymous said...

wewe mdomo mali yako ,ngoja dkk 90.

Anonymous said...

Punguza munkari kaka!!!

Anonymous said...

Du! amakweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza, Chuji maji shingoni ametoka na nafasi yake inachukuliwa na Nurdin. N bado mpakawote waombe kutoka

Anonymous said...

Msife moyo maana naona timu imeanza kuamka na kumshambulia mnyama

Anonymous said...

jamaa vipi matokeo naona blog imevamiwa na nyani

Anonymous said...

Yanga wamesawazisha kwa bao la Mwalala. Hadi sasa ni 1-1. Mpira unaenda vizuri tu.

Geoff Mwambe
Mannheim, Germany

Anonymous said...

sasa hivi yanga wanashambulia ki roho mbaya mnyama akipona basi ujue Dalali kaingia uwanjani na mguu wa albino

Anonymous said...

Yanga inatawala kwa kiasi kikubwa mchezo.Ni nusu uwanja tu wanavyowachezea Simba. Ni kipindi cha pili sasa. Vijana wakijitahidi kuwa makini wataibuka na ushindi kwa ajili ya kuboresha rekodi tu.

Geoff Mwambe

Anonymous said...

simba wamepata goli la pili, yanga wana matatizo na safu ya ulinzi ni dhaifu saana

Anonymous said...

bado matokeo ni hayo hayo au kuna mabadiliko yeyote

Anonymous said...

Makosa ya defence na Kaseja kutoa upande mapema imempa nafasi Boban Haruna Moshi (Maximo) kufunga la pili kwa Simba.

Geoff Mwambe
Manheim

Anonymous said...

kwa maana hiyo tushalala 2-1

Anonymous said...

Tegete kaisawazishia Yanga. Mpira unakaribia kwisha. Hadi sasa ni 2-2.

Geoff Mwambe
Mannheim

Anonymous said...

jamaa mliopo nyumbani matokeo vipi? mpira bado unaendelea

Anonymous said...

geoff asante ndugu yangu kwa muda wako.

Anonymous said...

ahsante geoff tutaarifu matokeo ya mwisho

Anonymous said...

Mpira umekwisha na matokeo ni 2-2. Hakuna mbabe.

Goeff Mwambe
Mannheim, Germany

Anonymous said...

Haya mimi ni mdau wa kwanza niliyesema kwamba sale inatosha sana kwetu, mimi nawajua hawa waarabu wanajua sana kafili hasa huyou babu yao Dalali, haya kazi kwao sasa

Anonymous said...

ndiyo mkubali mkimfunga simba inakuwa kama ndoto kwenu hiyo sare kwa yanga mmeshinda wapuuzi nyie mnadhani pesa zinacheza mpira?

Anonymous said...

Wewe Anon wa juu, mmezidiwa kila kitu, acheni imani ya uchawi, waarabu watawafila nyinyi

CM said...

Shukrani sana kwako mdau G. Mwambe kwa update zako hapa katika blog.

Anonymous said...

simba nyinyi ndio mlikuwa mkitaka mshinde,msijifanye kama ndio hio draw sisi tumeshinda,kama mnao uwezo basi leo ilikuwa ndio mshinde kwani sisi ilikuwa ni kulinda heshima tu,

Anonymous said...

Tuko pamoja Mzee CM na wadau wengine. Yanga Daima Mbele, Nyuma Mwiko.

Kwa wale WADAU wa YANGA waliotaka kushiriki kwenye ujenzi wa WEBSITE ya Club kokote waliko, waniandikie geoffrey.mwambe@gmail.com. Process imeshaanza na tunawakaribisha wadau ambao wako na nia ya kufanikisha.

Geoff Mwambe
Mannheim, Germany

Anonymous said...

website ya club au ya mashabiki wa club ya yanga? nadhani tofauti iko wazi, hasa masuala juu ya nini website itakuwa na uwezo wa kusema/kutosema lolote.

Anonymous said...

Hiyo wala isikupe shida mdau wa hapo juu. Kama nilivyoeleza awali ni website ya Club - links za mashabiki (fan zones) zitakuwa humo humo. Na wala usitie shaka, tunashirikiana na Uongozi wa Yanga. Na Phase 1 is almost over. Kama kuna wadau wengine wako interested wajiunge tu. Lakini tu, ni kwa wale wenye mtizamo wa maendeleo na wanaofahamu maana ya majukumu kwenye Community kama Club yetu, wenye malengo na wenye team-work spirit ya kujengana. Hii ni kutaka wadau tushirikiane na kujengana kwenye kuiimarisha Club yetu.

Geoff Mwambe
Mannheim, Germany

Anonymous said...

Geoff Mwambe,nitakuandikia bwana, wazo zuri sana hilo.

Anonymous said...

Haya delete na hii msg..... wizi mtupu. Kama hoja leteni hoja siyo ku-delete msg zinazosema ukweli.