Tuesday, June 30, 2009

Yanga kutangaza usajili
Mabingwa wa soka nchini Yanga leo wanatarajiwa kutangaza wachezaji wake wapya iliowasajili kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo kwenye michuano mbalimbali ya kimataifa ikiwa ni pamoja na michuano ya Ligi Kuu.

Mbali na kuvitangaza vifaa vipya, itawasilisha baru aza maombi ya vibali vya uhamisho vya kimataifa vya baadhi ya wachezaji wake kutoka nje ambao wamemkuna kocha wa timu hiyo Dusan Kondic na kukubali kuwasajili.

Akiongea jijini Dar jana Mwenyekiti wa klabu hiyo jana Mwenyekiti wa klabu hiyo Imani Madega alisema kuwa zoezi la usajili wamelikamilisha na kesho watawasilisha kwenye Shirikisho la soka nchini (TFF) majina yote ya wachezaji wao wapya.

Madega amewataka wapenzi wa Yanga wategemee mambo makubwa kutoka kwa timu yao kwani usajili wao wa msimu huu wameufanya kwa umakini mkubwa lengo likiwa ni kupata wachezaji wenye viwango vya juu vitakavyoiwezesha Yanga kufikia katika hatua za juu za michuano ya kimataifa na utetezi wa ubingwa wa nyumbani.

AIdha mbali ya wachezaji wapya kutoka nje, pia Madega amedai wameshakamilisha mazungumzo na baadhi ya wachezaji wao waliomaliza mikataba yao.

Baadhi ya wachezaji kutoka nje ambao Kondic amevutiwa nao ni wachezaji kutoka Rwanda Abulkarim Kamanzi na Kabonge Honore, Stephen Bengo kutoka Uganda, Frankline Teme kutoka Cameroon na Moses Odhiambo kutoka Kenya.