Thursday, July 02, 2009

Wapya wa Jangwani

Klabu ya Yanga imewasilisha kwa Shirikisho la soka nchini (TFF) majina ya wachezaji wake wapya itakaowasjili kwa msimu ujao wa ligi. Wachezaji hao ni hawa wafuatao:

Kabongo Honore
Raia wa Rwanda aliyekuwa anachezea klabu ya Samut Songkram ya Thailand

Moses Odhiambo
Mkenya ambaye alikuwa akisakata soka APR ya Rwanda.

John Njoroge
Mkenya ambaye alikuwa Tusker ya Kenya

Joseph Shikokoti
Mkenya ambaye alikuwa Tusker ya Kenya

Steven Bengo
Mgnda ambaye alikuwa
SC Villa ya Uganda

Robert Jama Mba
Mcameroon ambaye alikuwa Canon Yaounde

Nelson Kimati
Mtanzania - Prisons ya Mbeya

Bakari Mohamed Mbegu
Mtanzania - Sifapolitan ya Temeke

10 comments:

MASEBE said...

TUNASHUKURU SANA KWA KUTUHABARISHA KWA WAKATI. TUNAOMBA UENDELEE KU UPDATE HABARI, KAMA NILIVYOSEMA AWALI HABARI ZIKICHELEWA KUPATIKANA KIJIWE KINAPOA SANA.
ASANTE SANA.
NAFIKIRI PROF.AMESAJILI VIZURI SANA

Anonymous said...

alafu ukifahamu wageni hao wanacheza nafasi gani tuhabarishe.
alafu ukipata muda hebu tembelea mazoezi yao utupatie na viwango vyao kama vinaridhisha.

naelewa kwamba unafanya blog hii kwa hisani zako mwenyewe wala siyo jukumu langu kukupangia utaratibu wa mambo yako. lakini mzee uwaga unatufaa sana kwa blogu yako hii ndio maana hamu haiishi

Anonymous said...

e bwana mimi pia nakushukuru kwa yote unayo fanya,kweli muda wako ni wa dhahabu,asante .mwanza

Anonymous said...

Mzee CM,
Natumai unaendelea ku-roll na blog yetu wadau wa Jangwani/Twiga. Ni siku nyingi sijasalimia wadau wenzetu ila karibu kila siku najipa nafasi ya kupata some up-dates za blog hii. The project that we're undertaking regarding the Yanga's website is going well. Tumeshalipia domain registration and the first layout is ready. Tuko kwenye technical aspects za layout na tunajitahidi kila tuwezalo ili by the end of the year Wana-Yanga wawe na official website yao. Thanks wadau wote kwa mshikamano. Tuendeleze Club yetu na tui-transform kuwa the real international and professional.

Yanga Daima Mbele, Nyuma Mwiko.
Geoff Mwambe
Mwanachama wa Yanga
Card No. 000661
Mannheim, Germany

Anonymous said...

Jamani wapenzi wa mnyama nao wametua na site yao ni hii
http://simbasc.ning.com/

Kazi kwetu nasi hii inahitaji kuboreshwa maana inasikitisha hni ya amature kweli kweli au sijui ndo kandambili?

Anonymous said...

Waungwana mratibu wa hii site yuko hai au alishavuta boksi lake siku nyingi? inasikitisha mno maana haina maendeleo kabisaa.

Anonymous said...

Ha ha ha ha , hii ni kijiwe cha Yanga kandambili, wewe ulikuwa hujui?

Anonymous said...

jamaa vipi? kimya au mishughuliko tupashane mapya

Anonymous said...

Sasa mzee maana ya blog ni kuwa na habari mpya at least moja kwa wiki, sasa unatuweka kimya, najua unashughuli zako, lakini wote waliofungua blogs wana shughuli zao too, jitahidi basi walau utuwekee news mara kwa wiki.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___