Monday, August 24, 2009

Hatujampangia Kondic timu - Madega

Siku moja baada ya kocha mkuu wa Yanga Dusan Kondic kutoa lawama kwamba anaingiliwa katika upangaji wa timu, Mwenyekiti wa klabu hiyo Imani Madega amekanusha kufanya hivyo.

Mara baada ya mchezo wa jana, Kondic aliulaumu uongozi wa Yanga kwa kumwingilia kazi ya upangaji wa kikosi kilichoshuka jana kwenye Uwanja wa Uhuru kupambana na African Lyon na hivyo kusababisha timu hiyo kushindwa kuibuka na ushindi katika mechi hiyo.

Akitoa ufafanuzi wa kilichotokea, Madega alisema Kondic alikuwa ameorodhesha jumla ya wachezaji 7 wa kigeni katika mchezo wa jana na kuona hivyo uongozi kupitia kwa mratibu wa kamati ya mashindano ya klabu Emmanuel Mpangala ulimwarifu Kondic kwamba jambo hilo ni kinyume na kanuni za ligi kwani kanuni hizo zinazuia timu kutumia zaidi ya wachezaji 5 wa kigeni katika mchezo mmoja.

Hali hiyo ilisababisha Kondic apunguze wachezaji 2 wa kigeni kwa shingo upande ili kuendana na kanuni za ligi. Endapo Yanga ingewaweka wachezaji hao 7 katika kikosi cha wachezaji 16 (walioanza na wa akiba), African Lyon ingepewa ushindi wa mezani.

Kwa hali hii, Kondic atamaliza msimu?

13 comments:

Anonymous said...

Hali ngumu, Manji kaingia mitini, kocha anaona daa..jamani tujipange, tushukuru jamaa katuachia Jengo zuri la kisasa.

Anonymous said...

Uongozi yanga ni dhaifu mno

SJ said...

naona tutasambaritika mwaka huu...ni wakati tujitegemee wenyewe na kuacha kutegemea ufadhili kutoka watu binafsi....Tupokee usaidizi kutoka wadau waliyo na mapenzi na timu...

Anonymous said...

Hivi tatizo ni Manji? hapa kafanya nini mpaka alaumiwe amjitahidi kuwa mawazo kidogo tu ili time ije ijiendeshe lakini wapi sasa mnamlaumu nini? katoa pesa kukarabati jengo na ununuzi wa vitanda, lkn ubadhilifu umefanywa. Nia yake alitaka Yanga isiingie gharama kuweka kambi sasa bado kweli tunamlaumu?

Anonymous said...

vipi wazee leo manji kawa mbaya ?kwanini?mzazi kamwambia mtoto hebu kua iliujitegemee kwani ni ubaya gani?tuwe na mawazo ya kisasa ,manji you are great we will always remember you,nobody can do what have you done in yanga for decades asante.

Anonymous said...

Manji hakutoa msaada wa samaki tu, amejaribu kufundisha watu kuvua. Kama watu wataamua kubaki wameshikilia ndoano itakuwa kumtafuta Manji ubaya.

Anonymous said...

yes hiyo ni ukweli kabisa ,hebu tujifunze sasa.

Anonymous said...

Inasikitisha mno kuwa na uongozi mbovu wa kifisadi kama huu. Yanga haijawahi kupata mfadhili kama huyu. Hili siyo siri kafanya mengi mno

barazani said...

matokeo ya leo vipi wadau mlioko Bongo?

Anonymous said...

SAWA ,MANJI JIKATAE HUMO HAMNA KITU YANGA ALIKUWEPO MAREHE, GULAMALI ALIAMBULIA MITUSI OHH TEJA WE BADO MDOGO FUATA NYAYO ZA DEWJ MBUNGE: WEKEZA KTK TIMU ZISIZO NA MAJINA: UNA HERAAAA WEWE...!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! hii ndio yanga khakha!!!!!

Anonymous said...

SAWA ,MANJI JIKATAE HUMO HAMNA KITU YANGA ALIKUWEPO MAREHE, GULAMALI ALIAMBULIA MITUSI OHH TEJA WE BADO MDOGO FUATA NYAYO ZA DEWJ MBUNGE: WEKEZA KTK TIMU ZISIZO NA MAJINA: UNA HERAAAA WEWE...!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! hii ndio yanga khakha!!!!!

Anonymous said...

SAWA ,MANJI JIKATAE HUMO HAMNA KITU YANGA ALIKUWEPO MAREHE, GULAMALI ALIAMBULIA MITUSI OHH TEJA WE BADO MDOGO FUATA NYAYO ZA DEWJ MBUNGE: WEKEZA KTK TIMU ZISIZO NA MAJINA: UNA HERAAAA WEWE...!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! hii ndio yanga khakha!!!!!

Anonymous said...

hivi hizo khabari ya manji kajitowa mumezipata wapi?wapo watu wanalaumu nawapo wanapongeza naye yupo kimya mbona mna pupa kilichofanywa kutizama jee yanga bila msaada kutoka nje inaweza kujiendesha au !!!!