Friday, August 07, 2009

Yanga, Mtibwa katika Ngao ya Hisani
Shirikisho la soka nchini TFF limerejesha utaratibu wa kuwa na mechi ya ufunguzi wa msimu ya kuwania Ngao ya Jamii/Hisani kwa kuzikutanisha Yanga na Mtibwa Sugar katika mechi itakayopigwa Agost 16 kwenye Uwanja wa Uhuru.
..........................................................................................................................................................................
Hata hivyo kwa mwaka huu timu hizo mbili zimeteuliwa tu lakini utaratibu kamili utaanza kuanzia msimu ujao ambapo Bingwa wa ligi atakutana na mshindi wa Kombe la Shirikisho au kama kombe hilo halitakuwepo basi atakutana na mshindi wa pili wa ligi.
..........................................................................................................................................................................
Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 23.

4 comments:

Masebe said...

Tunaomba kujua vigezo vilivyo tumika katika uteuzi wa timu za kushiriki Ngao hiyo. Kuna vigezo vyovyote au ni kutaja tu.

Anonymous said...

Kwa msimu huu umefanyika uteuzi tu wa timu.

Inawezekana TFF imeamua kuchukua mshindi wa ligi na wa Kombe la Tusker......labda

Hata hivyo kwa kuanzia mwakani kutakuwa na utaratibu maalum.

MUGANYIZI said...

KWA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA KAIJAGE JUMAPILI ILIYOPITA KIPINDI CHA MICHEZO MCHANA REDIO TANZANIA NI KUWA: WALIJADILIANA NA TIMU ZOTE NA KWA UPANDE WA YANGA HAIKUWA NA UBISHI SABABU WAO NDO MABINGWA LAKINI KUHUSU SIMBA ALISEMA ASINGEWEZA KULAZIMISHA, IKAONEKANA MWAKA HUU WAMCHUKUE MSHINDI WA TATU, LAKINI KI UKWELI NI KWAMBA SIMBA WALIGOMA NA KUKIMBIA MAANA TUKIWAFUNGA SASA MGOGORO UTAKUWA MKUBWA AJABU KIASI KWAMBA HATA LIGI WANAWEZA KUCHEZA KWA TABU.AKASEMA MWAKA UJAO KUTAKUWA NI MSHINDI KATI YA BINGWA WA BARA NA MSHINDI WA KOMBE LA FA YAANI LA LIGI. SASA NAJIULIZA BINGWA HUYU AKITWAA YOTE ITAKUWAJE. LAKINI LAZIMA KUNA UTARATIBU MZURI UNAANDALIWA. VODACOM WAMEKUBALI KUUDHAMINI MCHEZO WA NGAO YA HISANI MWAKA UJAO IWAPO TFF ITAPANGA TARATIBU ZINAZOELEWEKA.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___