Saturday, August 01, 2009

Yanga kulikoni?

Kuna baadhi ya mambo ambayo naweza kuyaita tetesi ambazo zimekuwa zikichanganya katika siku za hivi karibuni kuhusu hali ya mambo katika klabu yetu labda nikiyaweka hapa kuna wadau/mdau atakayesaidia kuondoa huu utata:

  1. Yanga ilipanga kuweka kambi huko Mwanza lakini ghafla safari ya kwenda Mwanza ikafutwa na miongoni mwa mambo yanayotajwa kama sababu ni kwamba mfadhili Yusuf Manji amekataa timu kupelekwa Mwanza kwa vile tayari amegharamia ukarabati wa makao makuu ya klabu hiyo. Hata hivyo inasemekana Manji ameingizwa mjini katika ununuzi wa fenicha (vitanda) kwani vipo katika hali ya chini.
  2. Kocha Dusan Kondic na baadhi ya wachezaji wamelalamikia kutolipwa mishahara na fedha za usajili. Katibu Mkuu Lucas Kisasa amewahi kukaririwa na vyombo vya habari kwamba hakuna klabu inayolipa vizuri nchini kama Yanga na kilichotokea ni kubadilika tu kwa utaratibu kwa vile kuna wachezaji wengi wapya kwenye mfumo wa malipo.
  3. Yanga imeshindwa kumalizana na SC Villa ya Uganda kuhusu uhamisho wa mchezaji Steven Bengo. Shirikisho la soka la Uganda FUFA limeijibu TFF kwamba haiwezi kutoa hati ya uhamisho wa kimataifa mpaka hapo Yanga itakapomalizana na Bengo.
  4. Yanga ilishindwa kuwasilisha majina ya wachezaji itakaowaacha kwenye ofisi za TFF lakini baada ya siku chache ikasema haitaacha wachezaji ambao bado wana mkataba. Hivi majuzi Yanga iliibuka na kusema itamwacha beki George Owino wakati mchezaji huyo bado hajamaliza mkataba. Hali hiyo iliifanya Simba kumwekea pingamizi kwamba hawezi kuachwa kwa vile muda wa kuacha wachezaji umeshapita.
  5. Uuzaji wa hisa za klabu ya Yanga umekwama kuanza kutokana na malengo ya kukusanya idadi kubwa ya wanachama kushindwa kufikiwa. Yanga ina mashabiki wengi ambao hawajahamasishwa kuchukua uanachama na hata suala la mashabiki wa Yanga walio nje ya nchi na wanataka uanachama bado halijapatiwa ufumbuzi.
  6. Yanga haijaweka wazi sifa za nafasi ya kazi ya Katibu pamoja msemaji wa klabu hiyo na matokeo yake wengi tunayajua.

Naomba kutoa hoja.

4 comments:

gray said...

nashangazwa na Uongozi huu wa Mwenyekiti kuhusu Taarifa za Club. Timu inafanya vizuri ni vema wanachama wakaitwa na kupewa taarifa kamili.
pamoja na hilo ni vema tukajua wanachama wangapi wamelipia fedha za uanachama na kiasi gani kimepatikana. nasikitishwa na hali hii.

gray said...

nashangazwa na Uongozi huu wa Mwenyekiti kuhusu Taarifa za Club. Timu inafanya vizuri ni vema wanachama wakaitwa na kupewa taarifa kamili.
pamoja na hilo ni vema tukajua wanachama wangapi wamelipia fedha za uanachama na kiasi gani kimepatikana. nasikitishwa na hali hii.

Masebe said...

Kwanza nakushukuru kwa kutuhabarisha tena wana Yanga kile kinachoendelea katika klabu yetu.
Mimi ninavyo ona kwa mtazamo wangu tuna tatizo kwa mwenyekiti wetu na timu yake ya uongozi.Swala la kushindwa kupata wanachama wakutosha halina maana kabisa kwa sababu hakuna hatua zozote zilizochukuliwa ili kupata wanachama hao 1000. Wao wanahangaika hapo Dar tu ili kupata wanachama, huku mikoani kuna watu tele wenye mapenzi na Yanga lakini hakuna juhudi zozote zinazo fanyika ilikuwapata. Kusema kweli ndugu zetu bado wanaongoza kama zamani tu (business as usual).Lakini pia ninacho ona ni kuwa hawa ndugu zetu hasa mwenyekiti hawapendi swala la Kampuni kwa hiyo wanatumia kila hila kuhakikisha halifanikiwi kabisa.Kwa watu makini walitaiwa kutumia nafasi hii ya ufadhili kuijenga Yanga kwa kuwekeza, lakini kinachoonekana jamaa wamelala hata hawana habari na kinacho endelea. Kwa mtindo huu hata huo ukarabati wa mamilioni hauna maana kabisa kwa sababu baada ya muda kutabaki magofu tena.Wamejaa hofu,hawataki kuajiri watendaji, ni hofu tupu.Jamani Manji naye ni binadamu anauchungu na fedha zake,hebu tumuonee huruma.Alipe mishahara yote,ukarabati wa jengo,uwanja.FOR SURE THIS IS THE FIRST AND LAST CHANCE OPPORTUNITY FOR THE CLUB IT WILL NOT HAPPEN AGAIN.Kwa nini tunaipoteza fursa hii?

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___