Sunday, September 06, 2009

Kondic, Chuji kifungoni
Kondic na Chuji -Wakumbwa na rungu la TFF
Kamati ya mashindano ya Shirikisho la soka nchini (TFF) limeiangushia Yanga adhabu ya faini ya 500,000/= pamoja na kuwafungia kocha Dusan Kondic pamoja na kiungo Athuman Iddi "Chuji" kwa vipindi tofauti kwa vitendo vya utovu wa nidhamu.

Kiungo Athuman Iddi amefungiwa kutocheza soka kwa miezi mitatu kutokana na kumtukana mwamuzi wa mchezo kati ya Yanga na African Lyon. Chuji alimtukana mwamuzi huyo mara baada ya mchezo pia licha ya kuzuiwa na wenzake, alipiga teke mlango wa chumba cha waamuzi.

Hii ni mara ya tatu kwa Chuji kukumbana na rungu la TFF, mara ya kwanza ilikuwa Agosti 2007 wakati alipofungiwa mechi sita za kombe la Tusker kisha akafungiwa miezi mitatu mwezi Oktoba 2007 kwa kumtukana mwamuzi katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Coastal Union.

Rungu la TFF pia limemkuta Kocha Dusan Kondic kutojishughulisha na benchi la ufundi kwa mechi tatu zijazo za ligi za Yanga kutokana na utovu wa nidhamu. Inasemekana Kondic alimzuia mwamuzi msaidizi wa mchezo dhidi ya African Lyon asifanye kazi yake kwa kusimama katika mstari na kukataa kuondoka licha ya kuombwa kufanya hivyo.

Aidha mashabiki wa timu ya Yanga wameitia klabu hiyo matatani kutokana na vitendo vyao vya kurusha vitu uwanjani na hivyo kusababisha klabu hiyo kutozwa faini ya 500,000/=.
Shughuli imeanza.

11 comments:

Anonymous said...

mhh kazi ipo...Naona hiyo kifungo kinaweza kuongezeka and kumpata kipa Obren Circkovic maana hao walifanya vurugu songea baada ya mechi..Nasikia TFF wana subiri ripoti ya Kamisa wa mechi..

Anonymous said...

Mwaka huu ni wa shetani nini? Vijna washauriwe wapunguze jazba ligi bado sana.

Tina said...

kazi ipo msimu huu,sio mwaka wetu

Tina said...

wanayanga tusikate tamaa kufungiwa kwa kondic na chuji ni kweli kutaiathiri kisaikolojia timu ila sasa hivi kinachotakiwa ni kuwapa wachezaji wote ushauri nasaha jamani ili wasiendelee na wasijisikie vibaya kwa kufungiwa kwa wengine,binafsi imeniuma sana lakini nitafanyaje wadau,Yanga wanahitaji ushauri nasaha wa hali ya juu kwa sasa haiwezekani kufungwa hivi.nina imani tutafanya vizuri tuu soon! tuzidi kuiombea timu yetu wala huu sio mwaka wa shetani kwetu japo nahisi kama simba wakiendelea hivi hivi mh!ubingwa twaweza kuuvua,dah naumia sana.....ningekuwa mchawi ningewaloga simba lakini nitamuomba mungu

Anonymous said...

Walishasema kuwa lazima safari hii wawe mabingwa kwa gharama yoyote,tumeanza kuona dalili, huyo mnyama bwana!!!

Anonymous said...

Tusivunjike moyo..ligi safari ndefu ila inabidi tukae na tukubali kuwa nmyama wamejiandaa vizuri mwaka huu...tusubire na tuangalie ligi tutamalizaje mwaka huu..wachezaji waache kuwa na hasira wakubali matokeo tuu, ushindi, kufungwa na sare....

Anonymous said...

msijiday tim yenu mbovu zaidi ya miaka 30 mshakuwa mabigwa hamna lolote, upuuzi wenu sasa unaanza kuonekana bora mkanunuwe wachezaji rufiji ndiyo iliyobaki

Anonymous said...

huyo hapo juu mwizi wewe.

John Mwaipopo said...

jamani lakini chuji ni nunda siku zote. aliwalostisha simba tukamchukua, ametulostisha taifa stars tukamvumilia, sasa kaachia shuzi jangwani. mpira na nidhamu ndio maswahiba. lila na fila havitangamani. afundishwe kuwa mvumilivu na mpole, hayo 'anayofanyiwa' yeye hata wachezaji wakubwa wa ulaya hufanyiwa lakini hutuliza munkari.

Anonymous said...

Kwali kabisa madu John..Inabidi Chuji apunguze hasira na hizo Bangi nayo asiache..No wonder Maximo alim drop Ivory Coast

Anonymous said...

so whats nxt for us?