Saturday, September 05, 2009

Kazi ipo Songea leo

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Yanga leo wanaingia kwenye Uwanja wa Majimaji huko Songea kupambana na timu ya Majimaji katika mchezo wa ligi hiyo.

Mchezo huo unatarjiwa kuwa mgumu kwani Majimaji tayari imepoteza mechi zake mbili za kwanza za ligi hiyo zote zikiwa katika uwanja wake wa nyumbani.

Yanga kwa upande wake itakuwa bila Wisdom Ndhlovu aliyeitwa kwenye kikosi cha timu ya tatifa ya Malawi, Boniface Ambani, Mrisho Ngassa na Shamte Ally ambao wamebaki Dar kutokana na kuwa majeruhi.

Mchezo mwingine utakapigwa leo utakuwa kati ya Simba na Toto Africa utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

24 comments:

Anonymous said...

Songea mambo yameiva, Maji Maji 1, Yanga 0, nitawapa habari zaidi, Maji Maji wamepata bao dakikia 20 Kipindi cha kwanza.

Anonymous said...

ahsante mdau muda bado ipo goli litarudi?vipi mnyama nae anateswa au la?

Anonymous said...

Mnayama anaongoza kwa goli moja, tungoje game bado sana.

Anonymous said...

Dar sasa Mnyama 1 and Toto 1, nadhani mdau umekosea, Songea bado ni 0 kwa wote

Anonymous said...

matokeo bado kama yalivyo au kuna mabadiliko

john, manchester said...

vipi mbona matokeo yanatafautiana.tuweke ukweli hapa

Anonymous said...

cm tupe usafi naona vipanya washaanza kupotosha humu

Anonymous said...

Tumuamini nani sasa??,mbona kila mtu anaripoti kivake.Tafazali nyie msio mashabiki wa yanga acheni kujipendekeza kwenye kijiwe kisicho chenu,km simba hamna glob sii mfungue yenu mkaposti huko?
Tafazali CM au mwanayanga yeyote atupe za kwelikweli!

john, manchester said...

vipi mbona matokeo yanatafautiana.tuweke ukweli hapa

Anonymous said...

vipi mpira bado haijaisha?

Anonymous said...

Haya Simba kashinda 3 - 1, Yanga kishafungwa 2 -0 mpira bado haujaisha, nitawapa matokeo.

Anonymous said...

jamani wekeni ukweli humu

Anonymous said...

wewe acha fitina

Anonymous said...

Huo ndiyo ukweli, mpira Dar umeisha Simba kashinda 3 na Yanga tayari ameishafungwa 2, mpira bado haujaisha

Anonymous said...

Dar: Simba 3 Toto 0
Songea: Majimaji 2 Yanga 0 Mpira umekwisha sasa hivi

CM said...

wadau mpira umekwisha.simba 3 toto 1 na majimaji 2 yanga 1.

Anonymous said...

Majimaji 1 Yanga 0
Simba 3 Toto 1

CM said...

Matokeo ya mechi za leo:

Majimaji 1 Yanga 0
Simba 3 Toto 1
Prisons 1 African Lyon 0

Kuna mdau amejipachika jina la CM ametoa matokeo ya uongo.

CM halisi ni hii yenye rangi ya blue.

CM said...

Inasikitisha kuona watu wazima wanapost matokeo ya uongo sijui hasa nia yao ni nini.

Na mbaya zaidi wanatumia jina la CM kufanya hivyo.(mdau aliyepost comment Sep 5, 2009 6:31:00 PM)

Naomba msituharibie blog yetu.

Anonymous said...

Nyinyi mlisajili kwa majina, sasa ngojeni hakuna timu hapo. Tunawangoja kwa hama, ngojeni tu.

Masebe said...

Blog hii kwa sasa imeingiliwa na kila mtu anaona. Kinachotakiwa kufanya kwa sasa bwana CM unatakiwa kuchuja habari za kuchapisha, sioni kwa nini uchapishe kila takataka inayo ingia.Other wise hii hiki si kijiwe cha wanayanga tena. Tunapenda tupate habari za kweli zinazo husu klabu yetu. Tumewakimbia mitaani na kashifa zao bado wanatufuata hata hapa. CM huna haja ya kulalamika wewe una rungu kwa nini unaruhusu upuuzi huu. Bila kuchukua hatua watu wataacha kufungua blog hii.Awali hatukuwa na shida hizi,ONDOA TAKATAKA ZAO NA WATAONDOKA WAO WENYEWE,kuendelea kuchapisha huo utumbo wao ni kuwakaribisha.

Anonymous said...

Eti CM ni kweli Manji ametaka timu irudi Dar haraka kabla ya mechi ya pili? hizi habari nimezisikia leo pale mgahawa wa Falcon.

Anonymous said...

Mimi sijasikia hilo la Manji, lakini nilichosikia ni kuwa Yanga wametozwa faini ya 500,000. Chuji kafungiwa pamoja na kocha Kondochi..., labda CM anaweza kutupa habari kamili.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___