Tuesday, September 08, 2009

Yanga kuwavaa Wanajeshi leo
Baada ya kujeruhiwa huko Songea, Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Yanga leo inajitupa tena katika uwanja wa Uhuru kupambana na maafande wa JKT Ruvu katika mchezo wa ligi hiyo.

JKT hadi sasa imejikusanyia pointi 6 wakati Yanga ina pointi 4 kutokana na mechi tatu. Timu zote mbili zinaingia uwanjani baada ya kupoteza mechi zao za mwisho. JKT ilichapwa 1-0 na Mtibwa Sugar wiki iliyopita.

Tusubiri dakika 90.
FT 2-2

25 comments:

Anonymous said...

Vipi jamani mbona kimya humu leo...??CM tuwekee mambo yanaendaje huko..naona mpira half-time sasa

SP said...

yanga 1 Vs Jkt 2.
mpira kali leo..Ubabe mtupu..

CM said...

Yanga ipo nyuma kwa mabao 2-1.

Bado dakika 3 mpira kumalizika

Anonymous said...

Tumefungwa tena, hivi kwa nini tulisajili majina? kingine mimi naona kocha hatufai kabisa, lazima kufanya masahihisho mapema. Mimi nipo nje ya Tanzania, lakini nimeambiwa na mdogo wangu kuwa tulizidiwa kila idara, huyu kocha anafanya nini?

CM said...

Yanga imesawazisha kwa njia ya penalti katika dakika ya 45+3 iliyofungwa na Kiggi Makassy

CM said...

Mpira umekwisha kwa Yanga kutoka sare ya 2-2.

Kazi tunayo mwaka huu.

SP said...

ehh afadhali refa katubeba naona leo bakora zingetembea...duu afadhali pointi...CM unasemaje bwana mwaka huu basi

Anonymous said...

Mtabebwa sana mwaka huu!!! Lunyasi anawasubiri yaani ni kichapo kwa kwenda mbele

Anonymous said...

Mkubali timu yenu mbovu sana mwaka huu...hakuna cha Ambani wala Baraza..Vipigo tuu...hata hizo hela za EPA from Manji hazitawasaidia...

Anonymous said...

Mkubali timu yenu mbovu sana mwaka huu...hakuna cha Ambani wala Baraza..Vipigo tuu...hata hizo hela za EPA from Manji hazitawasaidia...

Anonymous said...

Timu haina ubovu wowote, na itafanya vizuri tuu, muda bado upo. Timu zinazoongoza zimetuzidi chini ya point 10 ambayo ni kama michezo mitatu ya kushinda. Timu ijipange upya na tunaweza kuwa kwenye nfasi 2 za juu mwisho wa msimu.

Nahisi defence haijakaa sawa baada ya kuondoka Nadir, lakini tukijipanga vizuri, sii tatizo kubwa kurekebishwa.

Simba naona mnachonga saana, lakini mnasahau ni mechi 4 kati ya 22 zimechezwa.

Anonymous said...

maneno yako mshikaji sawa kabisa ni kujipanga tu ligi bado sana ila inatosha zilizopotea zishapotea naamini matokeo yajayo watanyamaza vijana wasahau michezo iliyopita nawatazame ushindi mapema maana kila mmoja anaikamia yanga kuchukuwa ubingwa mfululizo siyo kama wanafurahi timu zote zinaikamia yanga tuwe macho nao wote hamna mdogo wala mkubwa kujikwaa si kuanguka yanga imara daima

Geoff Mwambe said...

Dear Wadau wa Jangwani,
Maendeleo ya timu si mazuri ila baadhi yetu tulitabiri akiwemo Kondic mwenyewe kuwa mwanzo unaweza usiwe nzuri.Mnakumbuka timu haijakaa kambini na kufanya mazoezi ya pamoja kama Simba.Kondic alitaka usajili ukamilike mapema na malipo kwa wachezaji na akakae nao Mwanza (Simba walienda Zanzibar) ili kuwaunganisha na kutafuta mfumo mpya.Lakini hayo yote hayakufanyika.Mazoezi yalikuwa shaghala baghala.Pia ratiba ya TFF inabana sana.Hakuna muda wa mazoezi,ni kusafiri kila siku.Hapo wataenda Mbeya na Bukoba.Then Dar, Mwanza,etc.

Kwa sasa binafsi simlaumu Kondic.Hata yeye kalalamika na tulimsikia.Mpira ni ufundi na si jina.Hivyo mazoezi ni muhimu kuliko jina la YANGA.Baada ya mechi kadhaa timu ita-stabilize na Simba hawajafika popote.Tutakuta tu.Si mnaona Man U miaka yote huanza vibaya???

Yanga Daima Mbele Nyuma .....
Mwanachama Yanga
Geoff Mwambe
Mannheim, Germany

MUGANYIZI said...

mambo yatakuwa shwari tuu nyie tulieni. wanaoshinda sasa hivi watajisahau. we acha sisi tucheze kwa machungu.

Masebe said...

Wadau hapo juu(Mwambe na Muganyizi) mmesema kweli,timu ki ukweli ndio inaanza mazoezi, tofauti na miaka ya hivi karibuni ambayo tumekuwa na tabia ya kuweka kambi mwaka huu hatukufanya hivyo, huwezi kutegemea maajabu.Naamini bado tuna uwezo mkubwa kisoka na kutwaa ubingwa inawezekana.

Anonymous said...

Kwani jamani Manji ndiyo kajitoa kabisa? Mimi nimekuwa nasikia tu mfadhili kajitoa, mara hili na lile, mliopo nyumbani naomba mtufahamishe..


Abdul

SP said...

hajajitoa kabisa ila anajiweka kando kwa sababu viongozi hawajateketesa ahadi waliyompa manji kama vile klabu kujiendesha kama kampuni na vitu vingine.nasikia anataka kununua klabu ndogo kama alivyofanya MO na mbagala utd na kuifanya iwike kuliko simba na yanga

Anonymous said...

Jamani matokeo ya mtibwa na majimaji ni ngapi ngapi?

Tujue kama kafungwa au kashinda tafazalini mnaojua.

SP said...

matokeo ya leo. Majimaji 1 vs mtibwa 0. Moro utd 2 vs Azam 3. mtibwa kazama songea. Mnyama dimbani kesho na kagera.

Tina said...

mh!poleni sana wana yanga wenzangu,mimi napenda kuuliza hivi kwanini wabongo timu ikifungwa tu mnaanza kumlaumu kocha mbona hamuangalii na matatizo mengine ,hamjui kuwa tatizo dogo tu laweza kumuathiri mtu kisaikolojia nyie mnamlaumu kocha,binafsi sioni kama kocha ana matatizo yeyote koz bado tuna kocha mzuri sana so tusimzonge kwa maneno jamani tuwe wastaarabu sana angalieni na uongozi wetu pia,pesa za wachezaji na vitu vingine ambavyo vinawaathiri kisaikolojia.na pia tumuachie kocha arekebishe pale ambapo anaona panamapungufu pengine kwa kumshauri lAKINI SIO KUMLAZIMISHA afanye tunachokitaka sie matokeo yake mliyaona katika mechi ya african lyon,mimi nina imani tutafika tu,ALIE JUU MPANDIE HUKO HUKO!.YANGA MBELE............

Tina said...

JAMANI CM HIVI KWANINI UNARUHUSU HII MIJISIMBA KOMMENT ZAKE HUMU NDANI,UMESAHAU HISTORIA YA SIMBA NDIO INAYOONGOZA KAWA KUWA NA MASHAABIKI WAKOROFI KULIKO WOTE JAMANI! MIMI NAOMBA UIPITIE TENA BLOG YAKO NA UWE UNACHUJA MSG ZA KUINGIA HUMU NDANI WNAWACHUKIA SIMBA SIPATI MFANO NDIO TIMU INAYOONGOZA KWA KUWA NA MASHABIKI WAKOROFI DAIMA! YAANI NATAMANI NIWATUKANE! KHAAA NINA HASIRA HAPA MPAKA NAANDIKA KWA KUIGONGA GONGA KEYBOARD KWA NGUVU...KHAAAAAA!

Anonymous said...

acha hizo Tina,kubali timu yetu mbovu tu.mnyama kamtafuna kagera 2 bila leo.tukubali simba wamejianda kwa hiyo tuwape hongera

Anonymous said...

Tina, huyo jamaa hapo juu achana naye, ni Simba tuu. Utaharibu keyboard yako bure kwa hasira! :)

Tina said...

dah! huyo anonymous waSep 10, 2009 7:04:00 PM
anabahati hajiamni hata jina hajaandika, msh.£$&*.........angeona.CM unayasikia hayo lakini unanichunia tu fanya mambo ya kuchuja msg bwana mtu wangu.simba mmebahatisha tu nyie mbona mmekaa miaka mingapi mfululizo bila kunyakua hata kombe sasa hivi mnajifanya mnajua kwanza sijibizani na damu mie, rangi yenu si.....anzisheni blog yenu mbona mna wivuuuuuuuuuuuuuuu

Anonymous said...

yanga imara nendeni mkapike kangara,mtakoma mwaka huu sio baraza tu hata mkinunuwa ukuta mtaipata,