Thursday, October 22, 2009

Odhiambo, Maftah kuikosa Simba
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limewafungia wachezaji wake Amir Maftah na Moses Odhiambo wasicheze mechi tatu za Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.

Wachezaji hao 'wamekwenda jela' zikiwa zimebaki siku kumi kabla ya mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga.

Timu za Yanga na Simba zinatarajiwa kumenyana Oktoba 31 katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ofisa Habari wa TF, Florian Kaijage, amewaeleza waandishi wa habari jana kuwa,kikao cha Kamati ya Mashindano ya shirikisho hilo kimetoa uamuzi huo Jumatatu wiki hii.

wachezaji hao wamepatikana na hatia ya kumshambulia kwa maneno mwamuzi msaidizi namba moja aliyechezesha mechi ya Yanga na Azam Oktoba 17 na kutaka kuingia chumba cha waamuzi kufanya fujo.

Wachezaji hao pia wametozwa faini ya sh.500,000 kila mmoja,Yanga imetozwa kiasi hicho hicho baada ya mashabiki wake kumrushia mwamuzi msaidizi namba moja chupa za maji, mawe na kusababisha mchezo kusimama kwa dakika moja.

Msemaji wa Yanga, Loius Sendeu alisema jana kuwa watakutana kujadili cha kufanya.

“Inashangaza sana uamuzi huu, lakini tutakutana haraka iwezekanavyo na kuamua tuchukue hatua gani,” alisema Sendeu.

...........Cirkovic mgonjwa
Sendeu pia alisema, kipa wao wa kutumainiwa,Obrein Cirkovic,juzi aliugua ghafla, akalazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, amepata nafuu, na ameruhusiwa jana.

“Hatujajua hali yake itakuwaje, lakini tunaomba apate nafuu ili aweze kuitumikia Yanga kama kawaida,” alisema Sendeu.

6 comments:

Tina said...

dah kweli huu ni mwaka wa shetani,sijui tufanye nini?

muganyizi said...

tupe matokeo ya simba na moro

muganyizi said...

jamani kuna mtu au hakuna

Anonymous said...

Wadau, mbona mnauliza matokeo wakati inajulikana kabla mpira haujaanza..mnyama hakamatiki..Azam kaondoka 1-0..Bado Yebo Yebo..Lol..!!

Anonymous said...

Angalieni mwananchi.co.tz kupata matokeo ya leo

Anonymous said...

kweli kuna jamaa hana la kufanya ila anaangali ya wenzake ,duh kweli binadamu haoni mkudu wake lakini ya mwenziwe anaona bila shida.