Tuesday, October 27, 2009

Tibaigana awafungulia akina Maftah

WACHEZAJI Amir Maftah na Moses Odhiambo wa Yanga, wako huru kuichezea timu yao kwenye mpambano wa Jumamosi dhidi ya Simba baada ya kufutiwa kifungo cha kukosa mechi tatu na faini ya shilingi 500,000 baada ya kikao cha kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Kushindwa kuwasilishwa kwa aina ya matusi waliyotukanwa na wachezaji hao ni moja ya sababu za kuachiwa huru na kufutiwa faini ambayo ilitakiwa kulipwa na wachezaji hao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa kamati hiyo Kamishna wa Polisi Mstaafu, Alfred Tibaigana alisema kamati yake imeshindwa kugundua kosa na kutoa maamuzi ya kuwapa uhuru wachezaji hao kwa kushindwa kugundua sababu halisi ya makosa waliyoshitakiwa.

''Hukumu inaonyesha kuwa wachezaji hao walimtukana msaidizi wa mwamuzi wa kwanza mara baada ya mpira kumalizika na taarifa hizo zikaandikwa kwa taarifa ya kamisaa,''alisema Tibaigana.

''Hukumu ambayo bado haina uhakika kwa kuwa walishindwa kuandika aina ya matusi ambayo yalitukanwa na wachezaji hao, na sisi kama kamati hukumu za namna hiyo huwa tunazihukumu kwa kumpa haki mshatakiwa kwa kuwa zinakuwa za shaka kwa kutokamilika.

''Itakuwa bora yanapotokea matatizo kama hayo , basi waamuzi wanapoandika ripoti zao wanatakiwa kuandika aina ya matusi ambayo wanatukanwa kwa kuwa wao ni binadamu na tukio kama hilo halikuwa na ushahidi,'' alieleza Kamanda Tibaigana.

Alisema wao kama kamati ya mashindano wamewaachia huru wachezaji hao tangu kufanyika kwa kikao hicho kilipokutana na kubaini kushindwa kwa waamuzi na kamisaa kuweka bayana matusi kutambua makosa kazi ambayo wamewaachia TFF kama itakatwa rufaa nyingine.

Kutokana na uamuzi huo, Maftah na Odhiambo waliotiwa hatiani na kupewa adhabu na faini hiyo wakidaiwa kumtukana mwamuzi siku ya mchezo baina ya Yanga na Azam FC mchezo uliomaliza kwa suluhu ya bao 1-1, wameondolewa kifungoni.

8 comments:

Tina said...

asante sana CM kwa taarifa,simba kaeni chonjo lazima tuivunje vunje rekodi yenu na ninawaambia lazima tushinde tena mwaka huu,haya sasa wenye vidomo domo mseme! mpira ni dk. 90.ACHENI MANENO SIMBA.

Anonymous said...

Tina uwezo wa kuifunga Simba hatuna.Mimi ni Yanga lakini msimu huu wenzetu wanatisha kwa matayarisho mazuri.Wakati wenzetu wapo kambini sisi wachezaji wetu bado wanazunguka Dar kwa ukosefu wa pesa za kuipeleka timu kambini.

Anonymous said...

Wee Tina acha unafiki kwenye post ya kufungiwa wachezaji umedai huu ni mwaka wa shetani.Hapa unatamba kama wafanyavyo Simba.Mpira ni dakika 90 wacha hizo ngojea dakika 90 wacha kujishaua.

Anonymous said...

Wewe Tina ni Simba sana, yaani wewe unafikiria kwenda Zanzibar ndiyo kambi peke! Timu hipo kambini hapa Dar sasa wewe unataka kambi gani? yaani sababu Simba kenda Zanzibar basi na sisi twende Zanzibar? mwaka jana tumewafunga mbona kambi ilikuwa Dar, pia tulitoka nao sare wakati wenyewe wakitokea Zanzibar na sisi kambi yetu ilikuwa Dar pale Protea Hotel, sasa wewe unataka kambi gani? subiri dakika tisini ndiyo uweze kuweka conclusions zako.

Anonymous said...

Nadhani hawa tff wanakijiagenda cha kutengeneza pesa na hizi kamati zake ,kila wachezaji wakifungiwa lazima kamati ziwaachie,na kukata rufaa ni tsh 1million,wanachofanya ni kuwafungia wachezaji kwa makosa uchwara wakijua rufaa zitakatwa ili watengeneze pesa.

Tina said...

haha,anony wa 6:43 uliesema mimi ni simba nitake radhi kabisa inaelekea huwa haufungui hapa,mimi ni yanga damu toka utoto wangu na wala sitaiacha yanga tupo pamoja sana tu usijali wangu na huyo anony wa3:44,ndugu yangu kuandika mwaka wa shetani nilikuwa natafakari kuhusu yaliyopita tu na vile wachezaji wetu wanavyofungiwa haina maana kuwa mtatufunga,nahuyo anony anaekata tamaa mapema kwa kusema kuwa wachezaji wanazunguka dar,asikate tanmaa kabisa,tusubiri jumamosi,NARUDIA TENA KUMREKEBISHA YULE ANAESEMA MIMI NI SIMBA,kama amekwazika anisamehe ukweli ni kwamba NAICHUKIA SANA HIYO SIMBA.mungu ibariki dar young African! AMEN!!!

Tina said...

tunaishukiru kamati ta tff kwa kutufungulia watu wetu.lakini najiuliza ina maana wachezaji wetu tu ndio wanaowatukana marefa?au longolongo zao tu,mimi naona kama kuna ubabaishaji fulani hivi.

Anonymous said...

Hiyo kamati ya Nidhamu imejaa Simba watupu, bila Tibaigana by now zaidi wa wachezaji wetu sita wangekuwa wameishafungiwa. Haya jamani mliopo nje, Dar kwa sasa gumzo ni mechi ya kesho. Jangwani ulinzi ni mkali sana, leo mchana nilifanyikiwa kupita pale nikaona kuwa kuna ulinzi wa hali ya juu. Mtoto wa JK Ridhiwani peke aliruhusiwa kuingia ndani, na baada ya dakika kama 15 hivi Manji aliingia jengoni akiwa na wazee watatu kati ya watatu nayemfahamu ni mzee Mzimba tu. Kwa tadhimini mechi ni ngumu sana, hawa jamaa mwaka huu wamejiandaa pia wanajua hujuma sana, nadhani hicho ndicho yanga wanajipanga zaidi. Haya mambo yote kesho. Yanga mbele daima nyuma mwiko.