Saturday, October 31, 2009

Yanga vs Simba

Macho na masikio ya maelfu ya mashabiki wa soka nchini leo yataelekezwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya soka ya Tanzania Bara kati ya vigogo vya soka hapa nchini Simba na Yanga.

Huo utakuwa ni mchezo wa pili kwa vigogo hivyo kukutana ndani ya mwaka huu, ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni Aprili 19 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja huo na timu hizo kwenda sare ya 2-2, ambapo Yanga ilikuwa na jukumu la kusawazisha.

Mchezo wa leo utakuwa na umuhimu mkubwa kwa Yanga kutokana na ukweli ina changamoto kadhaa za kukabiliana nazo.

Kocha mpya, Kostadin Papic aliyechukua mikoba kutoka kwa Dusan Kondic atakuwa anakalia benchi la timu hiyo kwa mara ya kwanza wiki tatu zilizopita.

Pia Yanga yenye pointi 18 itakuwa na kibarua cha kupunguza kasi ya Simba, ambayo inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 27 baada ya kushinda mechi zake tisa za mwanzo.

Kutokana na ukweli kuwa ikipoteza mchezo huo ina maana itazidi kutoa mwanya kwa Simba kuzidi kupaa katika msimamo wa ligi hiyo. Yanga itakuwa fursa kwao kuendeleza ubabe wa kuifunga Simba kwa mara ya pili kwenye uwanja huo kama ilivyofanya katika raundi ya kwanza ya Ligi Kuu msimu uliopita, ambako Yanga ilishinda bao 1-0, Oktoba 26,2008.

Katika mchezo huo, Simba itakuwa na kazi moja tu ya kuhakikisha wanaendeleza wimbi la ushindi kwenye michezo yake ya ligi pamoja na kutaka kuweka rekodi mpya ya kushinda michezo 10 mfululizo.

Akizungumzia mchezo huo, kocha wa Yanga, Kostadin Papic alisema kuwa mara baada ya kukirekebisha kikosi chake ana matumaini ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

Kwa upande wake, kocha wa Simba, Patrick Phiri aliweka wazi kuwa anachohitaji ni pointi tatu kutoka kwa Yanga na uhakika wa kuzipata pointi hizo anao.

16 comments:

Anonymous said...

kila la kheri dar young africa daima mbele nyuma mwiko

Anonymous said...

Mpira ni mapumziko, Msimbazi wanaongoza

Anonymous said...

cm toa rada kaka

mdau italy

Anonymous said...

cm toa rada kaka

mdau italy

Anonymous said...

Mpira ni mapumziko, Simba wapo mbele kwa goli moja. Haya wadau habari ndiyo hiyo, tungoje kipindi cha pili.

muganyizi said...

tumechapwa tuombe mungu

muganyizi said...

mdau italy pole tumelambwa moja na mgosi

Anonymous said...

kipindi cha pili mnakula lingine yanakuwa 2- lakini mtapata 1 lazima mfungwe leo

Anonymous said...

we mchawi wa 2-1 leo lazima tung"oe mnyama
italy

Anonymous said...

utanambia baada ya mpira kwisha
kuwait

Anonymous said...

eti krosi ya benny mwalala...gazeti la mwanaspoti hamjui kuwa mwalala hachezi tena ligi kuu baada ya kuachwa na Yanga???
Anyway...naitakia timu yetu Yanga ushindi japo tupo nyuma kwa goli moja.

Anonymous said...

KKAKA CMMMMMMM UKO? NIPE UKWELI

CM said...

Mpira umekwisha tumefungwa 1-0

Anonymous said...

mtajiju ,ila mmejitaiidi ,na hole wenu tungekua 11 tungewapiga thalatha[3]kaaaaziii kwelikweli hahahahahah

Anonymous said...

ngojeni bakora nyingine mzunguko wapili,jeuri imekwisha mjuwe simba ni baba yenu ndiyo alokuwekeni mjini poleeeeeeeeeeeeni ama leo kweli jeuri imekwisha
bang bang

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___