Saturday, October 31, 2009

Tumelala 1-0

Bao pekee la mchezo liliofungwa na Musa Hassan Mgosi leo limetutoa katika Uwanja wa Taifa vichwa chini baada ya Simba kuendeleza wimbi lake la ushindi na sasa kufikisha pointi 30 katika michezo 10.
Mgosi alifunga bao hilo baada ya kupewa pasi na Danny Mrwanda katika dakika ya 26. Hata hivyo Mrwanda hakumaliza mchezo huo baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 68.
Hongera kwa walioshinda, ligi inaendelea.

15 comments:

Anonymous said...

HONGERA SIMBA,SASA TUJIFUNZE KUTOKANA NA MAKOSA YETU.

Anonymous said...

Poleni ndugu zangu wa Jangwani.

Anonymous said...

pole yeboyebo,ila msiba ni wakujitakia ,hivi hayo machezaji 10 ya nje mliyoysajiri ya kazi gani wakati viwango zero,tzn tuna wachezaji wazuri mara kumi ya hao ,kwa nn msitumie hayo mamilioni kusajiri vijana wa nyumbani wenye gharama dogo na ufanisi mkubwa kuliko hao akina mbami analipwa usd 1000 hakuna alifanyalo ,jifunzeni kutokana na makosa

Anonymous said...

wewe unatakia nini? umetoa mchango wako kwa simba au mdomo mali yako?

Anonymous said...

Poleni YaboYebo. Mliambiwa lakini mkawa wabishi. Mwaka huu ni kichapo kwa kwenda mbele tu! Aluuuuu!!!!

Tina said...

Poleni sana wana yanga, ila kwa kweli japo tumefungwa lakini kipindi cha pili nilikuwapo uwanjani tulijitahidi sema ndio hivyo makosa madigo madogo ambayo yanahitaji marekebisho,kila la kheri dar young african katika mechi ya mwisho asiekubali kushindwa si mshindani.MUNGU IBARIKI DAR YOUNG AFRICAN!

Anonymous said...

Pamoja na kuumia kwa kichapo lakini nimefurahi kwamba wametufunga na itasaidia labda kujifunza lakini pia kitendo cha wao kubamiza wakiwa 10 kimesaidia kutoa picha kwamba kupungukiwa mchezaji mmoja haina maana kwamba ndio timu itafungwa, kwa wanaokumbuka msimu uliopita mechi ya kwanza ndugu zete hawa walilalamika kwamba walifungwa kwa kuwa beki wao alioneshwa kadi nyekundu sasa je safari hii mbona wameshinda wakiwa pungufu? Tuacheni visingizio visivyokuwa na msingi pale tunaposhindwa mpira unahitaji maandalizi na seriousness vitu ambavyo viliigharimu simba msimu uliopoita na msimu huu vinaigharimu yanga. Swali lingine ambalo wa simba ningependa kuwauliza ni hili mwaka jana bao la Mwalala mlisema ni la kuotea hivi kuna tofauti gani 'kwa wale wanaofatilia mchezo huu wa kabumbu' kati ya bao la Mwalala na la Mgosi juzi, narudia tena kusema tuwe wanamichezo wa kweli tuacheni visingizio visivyokuwa na maana tunaposhindwa mara oooh wanatumia dawa za kuongeza nguvu, mara oooh wanabebwa. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.Kwa wana yanga wenzangu sio siri tunahitaji kazi ya ziada kurudi katika mstari manake inashangaza kuona mchezaji aliyewaacha wenzie mbaaali kwa magoli msimu uliopita msimu huu mechi kumi hata shuti moja la maana hakuna.

Anonymous said...

Yebo yebo hoyeeeeeeeeeeeeee! na mzee wenu Minjino! hahha mtoeni ndo mtaifunga Simba. poleni yeboyebo.

Mdau Simba

Tina said...

cm mambo ninahoja binafsi naomba niiwasilishe kwako kama inawezekana,unaweza kupata link ya sisi tuwe tunasoma yale magazeti yetu ya yanga humu ndani ili tujue nini kinaendelea kilabuni kwetu,hii itawasaidia wale wenzetu waliokuwa nje ya nchi kujua nini kinaendelea katika klabu yao ya yanga,naomba kutoa hojaCM USIWE KIMYA SANA BABAA! NAOMBA KUWASILISHA!

Anonymous said...

MISRI 4 TANAZIA 1 KIPINDI CHA KWANZA

Anonymous said...

tumelala kweli 4 kibao

Anonymous said...

timu ya maximo ati golkipa ni yule jammaa aliyefungwa na simbaaaaaaaa goli 4

Anonymous said...

Nyie mlimfunga???? wacha majungu.Mpira wetu bado kwa Misri.Maximo sio kocha wa kubadili timu .Atafutwe kocha mwingine.

Tina said...

CM mambo ninahoja binafsi naomba niiwasilishe kwako kama inawezekana,unaweza kupata link ya sisi tuwe tunasoma yale magazeti yetu ya yanga humu ndani ili tujue nini kinaendelea kilabuni kwetu,hii itawasaidia wale wenzetu waliokuwa nje ya nchi kujua nini kinaendelea katika klabu yao ya yanga,naomba kutoa hojaCM USIWE KIMYA SANA BABAA! NAOMBA KUWASILISHA!

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___