Saturday, November 07, 2009

Mshahara wa Kondic aulizwe Manji

UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema hauhusiki na ulipaji wa mshahara wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Dusan Kondic na anayewajibika na suala ni mfadhili mkuu, Yusuph Manji kama ilivyokuwa katika makubaliano yao.

Kondic ambaye yupo nje ya nchi kwao mara baada ya kuachia ngazi ya kuendelea kukifua kikosi cha Jangwani bado anaidai klabu hiyo mshahara wake wa miezi mitatu ambao hakulipwa.

Afisa habari wa klabu ya Yanga, Louis Sendeu alisema wao kama uongozi hawawajibiki na ulipaji mshahara kwa kocha huyo na hiyo ni jukumu la mfadhili wao ambaye katika mkataba wake ulionyesha yeye mlipa wake atakuwa mfadhili wa klabu hiyo.

Alisema ni kweli kocha huyo anadai kiasi cha shilingi milioni 30 ambazo ni za miezi mitatu, lakini wao hawahusiki katika hilo na hivyo kumwachia mfadhili , Manji kama ilivyokuwa awali.

"Katika jukumu la kumlipa kocha sisi kama uongozi hatuhusiki kwani kocha alipokuja kusaini mkataba ilisaini kuwa analipwa na mfadhili na sisi katika hilo hatuhusiki hivyo hiyo si kazi yetu sisi na endepo atarejea kwa ajili ya kuchukua malipo yake anatakiwa kwenda kwa muhusika na si uongozi,"alisema Sendeu.

Klabu ya Yanga kwa sasa inanolewa kocha Kostadin Papic ambaye amechukua nafasi ya Kondic aliyeiacha klabu hiyo

MWANANCHI

3 comments:

Anonymous said...

huyo manji atawachoka amewafundisha kula samaki pia kuvua samaki sasa mnataka aache kazi zake ashinde akiwalisha. haa haa kazi kweli kweli!!!!!!!!!!! yanga oyeeeeeee!!!!!! nina machungu. msingetoa hii habari kwa ushauri.

Anonymous said...

mimi yanga lakini hii ni ajabu,mtu kawasaidia lakini leo mnamruka kweli binadamu hana fadhila.

Tina said...

mh!