Vita vya Kagera
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Yanga leo wanajitupa katika Uwanja wa Kaitaba huko Kagera kupambana na Kagera Sugar ya huko katika mchezo wa ligi hiyo.
Yanga inabidi iingie kwa umakini katika mchezo huo, kwani katika misimu miwili iliyopita ilitoka kapa katika uwanja huo.
Michezo mingine inayopigwa leo ni:
Simba vs Moro United
Mtibwa Sugar vs Prisons
Toto Africa vs Majimaji
19 comments:
cm lete raha kaka mdau buruda hapa
bado hamna matokeo ndugu?
Dar Simba wanaongoza kwa goli 1
Bukoba, mambo bado...Kagera Sugar wamekosa penati.
Yanga wamepata bao katika dakika ya 26 kupitia kwa Mrisho Ngassa.
Kagera 0 Yanga 1
Dakika ya 55 bado tunaongoza 1-0.
Katika Uwanja wa Uhuru Simba 1 Moro United 1
Yanga imepata bao la pili kupitia kwa Jerson Tegete.
Kagera 0 Yanga 2
Asante cm mwendo mdondo kaka !!!!!!!!! MYAMA LAZIMA ALIWE LEO
? Mpira bado haujaisha
mnyama kapata bao la 2
Mpira umekwisha Dar:
Simba 2 Moro Utd 1
pointi 18 safi kwa mnyama.
Hakuna wa kumzuia MNYAMA mwaka huu, ote lazim walie tu!!!
Tusiangalie mnyama, sisi tuendelee kushinda tu...mnyama lazima atapoteza points huko mbeleni sisi tuendelee kushinda ndiyo dawa. Tuwe kama Man U, jamaa wenyewe wanachoangalia ni ushindi tu mpaka mwisho wa Ligi, huu ni mpira wa miguu, ligi bado sana.
Judy,
Denmark
Mpira umekwisha huko Kaitaba kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.
Kwa ushindi huo Yanga sasa imefikisha pointi 11.
Jioni njema
Tusiangalie mnyama, sisi tuendelee kushinda tu...mnyama lazima atapoteza points huko mbeleni sisi tuendelee kushinda ndiyo dawa. Tuwe kama Man U, jamaa wenyewe wanachoangalia ni ushindi tu mpaka mwisho wa Ligi, huu ni mpira wa miguu, ligi bado sana.
Judy,
Denmark
Kwi! Kwi! Kwi! Dua la kuku halimpati mwewe!!! eti yeboyebo kama Man u!! Subirini kichapo tu mtakapokutana na Mnyama
Mwalala
NY
wee judy mjinga sana ,man yuu ni wakubebwa tuu,unamaana nanyi yeboyebo mnabebwa sio? check leo match yao na sunderland utapata jibu, mnyela mkubwa weeee
Mdau hapo juu naona umechoka kubeba maboxi unamalizia hasira kwa Judy....nenda kapumzike bwana. Majuu kuzuri kama umesoma...
hahaha mnanifurahisha sana wana simba midomo juuu kazi mnayo.hata mseme sana ligi bado sna tu angalia msije kulia!yanga oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
cm na wanayanga wenzangu hivi ule mpango wa ngasa kwenda tena ktk majaribio westham umeishia wapi?wakati ule tuliambiwa ataludi tena kwa majaribio mengine ,lini ataludi tena westham?
Post a Comment