Friday, November 20, 2009

Wanne waachwa Yanga
Hamisi Yusuf
Mike Barasa
Boniface Ambani

Klabu ya Yanga imewaacha wachezaji 4 katika dirisha dogo la usajili liliofunguliwa kuanzia Novemba mosi mwaka huu.

Wachezaji waliotangazwa kuachwa ni pamoja na mfungaji bora wa mwaka jana Boniface Ambani, beki kutoka Kenya Joseph Shikokoti, Hamis Yusuf na Mike Barasa.

Vincent Barnabas

Mchezaji mwingine Vicent Barnabas ameuzwa kwa mkopo wa miezi 6 kwa timu ya African Lyon.

8 comments:

Anonymous said...

Robert Jama Mba naye angeachwa tu.

Anonymous said...

fred mbuna achaguliwe kama kocha msaidizi

Anonymous said...

Vicent Barnabas ni mchezaji mzuri na tutammiss..wengine waliotemwa poa tuu,ila ana mpango gani na hilo jani kichwani?

Anonymous said...

Jamani ebu na tujiulize kuna tatizo gani ndani ya timu yetu linalopelekea kila mchezaji hasa washambuliaji anapokuja pale makali yake yanapotea. Kumbukumbu zangu zinanirudisha nyuma tangu kusambaratishwa kwa kile kilichokuwa kikosi cha mauaji cha kina Mohamedi Hussen, Edibili Lunyamila, Marehemu Saidi Mwamba, Akida Makunda na wengineo hapajawahi kutokea tena safu ya ushambuliaji ya uhakika tangu hapo pamoja na kusajiri washmbuliaji wenye majina makubwa kama Henry Morris,Sammy Kessy, Krume Songoro,Pichu Kongo, Laurent Kabanda nw wengineo wengi, ni msimu uliopita tu ndo tulipata bahati ya kuwa na mfungaji mahiri ambaye naye sijui amekumbwa na nini mwaka huu.
Lngine ni lazima tukiri kwamba timu yetu haina beki tatu wa asili,kwa mtazamo wangu mimi tangu astaafu Kenny Mkapa hatujampata beki tatu kama beki tatu zaidi ya kubahatisha bahatisha tu, kama ningepata nafasi ya kumshauri mwalimu basi ningemwambia afanye juhudi kumpata mlinzi wa kushoto wa kweli kweli kama ilvyo kwa watani zetu vinginevyo tutaendelea kuwa tunafurahi mara moja tunalizwa mara kumi.

Anonymous said...

sajest tumchukue yupi, nadhani hata namba mbili hatuna

Anonymous said...

WAKATI Yanga ikikumbwa na ukata wa fedha za kufanyia usajili, uongozi wa Moro United umeitaka klabu hiyo kuacha kuwapakazia kuwa wamekwamisha usajili wa mshambuliaji wao, Yona Ndabila ambaye wanajangwani hao wamedai kushindwa kumsajili kutokana na dau kubwa ambalo yeye na klabu yake wanalitaka.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa uongozi wa Yanga, kwa sasa hauna ubavu wa kupata fedha za kufanyia usajili huo, kutokana na kutokuwa na mipango yao ya kupata fedha zaidi ya kutegemea chanzo kimoja ambacho kimeripotiwa kusuasua kutoa misaada tofauti na ilivyokuwa awali.

“Tofauti na wenzetu, Simba ambao wameungana na mambo yao yanakwenda sawia, sisi hapa ni mtu mmoja tu tunamuegemea asipotoa ujue tumeumia. Ndiyo maana hakuna la maana linalofanyika kuhusu usajili sijui itakuwaje,” kilisema chanzo chetu kilicho karibu na uongozi wa Yanga.

Chanzo hicho kilionesha kukerwa na hali hiyo lakini kikautupia lawama uongozi kwa kukosa mipango ya kila siku ya kuifanya Yanga japo ifanye usajili wa dirisha dogo.

“Tunahitaji kuchagua uongozi makini utakaotuondoa katika utegemezi huu, kwani mwanzo tulikuwa tukifanyaje?” kilihoji chanzo hicho.

Kuhusu suala la Ndabila, msemaji wa Moro United, Eric Anthony alisema jana kuwa, Yanga kupitia kwa katibu wake, Lawrance Mwalusako iliwasiliana na Mwenyekiti wa Moro United, Abdul Sauko kuomba kumsajili Ndabila ambaye naye aliwasiliana na bodi yake ya wakurugenzi ambayo iliamua kumruhusu mshambuliaji huyo kusaka malisho bora zaidi kwa mabingwa hao wa soka nchini.

Alisema hata suala la ada ya uhamisho, Yanga ilipewa nafasi ya kujipangia na kutamka wenyewe dau watakalotoa ili kumnasa Ndabila na kuongeza kuwa kwa kuwa Moro United haikutaka kumgeuza 'dili' Ndabila ilikubaliana na Yanga ambayo Ijumaa iliyopita ilitoa taarifa za kushindwa kupata fedha walizotarajia.

Anonymous said...

hakuna kitu mwaka huu...tujipange tupate angalau nafasi ya pili maana Azam na Mtibwa nao wamekazana mwaka huu..

Tutafute nama ya kujitegemee maana tumezoe ufadhili wa Manji na yeye sasa amechoka na uongozi mbovo...Watani wetu tuwape hongera maana wao wameungana na Friends of Simba ndio wanafanya usajili mzima..Nasiki wamesajili wakenya wapya wawili ambao ni wakali wataungana na Mike Baraza ambae anamwaga wino msimbazi Jumapili kwenye mgahawa wa Hadees...

Anonymous said...

Hivi kundi la Yanga family linafanya kazi gani kuisaidia timu?
maana kazi ya kundi la friends of simba inaonekana ni pale tu kundi hili linapokuwa katika msukosuko kama katika duru la kwanza msimu uliopita ndio timu inafanya vibaya,kumbu kumbu zangu zinanipeleka nyuma kidogo pale aliyekuwa Katibu mkuu wa simba Priva Mtema alipomtuka Abdallah Majura kwenye mahojiano baada ya timu waliyosajili wakati huo wakiwemo wakina Machupa, Machepe n.k ambayo wao waliamini kuwa ndio suluhisho la wao kufungwa mara kwa mara na Yanga kuonekana si lolote kwa Yanga ya kina Mmachinga,Lunyamila n.k. Kutoka hapo ndipo friends of Simba ikaundwa ikiwa na jukumu la kurudisha heshima ya Simba mbele ya Yanga, kilichofuatia nafikiri tunajua mkakati wa kwanza ulikuwa ni kudhoofisha kikosi cha Yanga kwa kujifanya kuwatafutia timu Uarabuni na kwingineko, kupandikiza wanachama na wachezaji mamluki. Kwa kweli binafsi kundi hili nalikubali kwa kuwa lina watu serious na wana mbinu za kimafia kuhakikisha timu yao inafanya vizuri hasa inapokutana na Yanga.
Sijaona wakati wowote kundi la Yanga Family ambalo liliundwa baada ya lile la Friends of Simba limechangia timu kufanya vizuri.
Suala la kumtegemea Manji nalo ni tatizo kubwa kwani ikitokea siku huyu bwana akaamua kubwaga manyanga manake ni kwamba hatuna timu.