Wednesday, February 17, 2010

TFF imechangia kipigo - Yanga

SIKU chache baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-2 katika mchezo wa kwanza hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Saint Eloi Lupopo, klabu ya Yanga imesema kipigo hicho kimechangiwa na TFF.

Yanga inadai kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), halikusikia maombi yao wakati ikijiandaa kwa mchezo huo, hali ambayo ilimfanya Kocha Mkuu wa Yanga, Kostadin Papic ashindwe kutekeleza baadhi ya mipango yake, hivyo kwa namna moja au nyingine kuvuruga maandalizi yao.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Yanga, Loius Sendeu alisema waliiomba TFF iahirishe baadhi ya mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara wiki mbili zilizopita hasa mchezo wao na Mtibwa, ili wapate muda wa kujiandaa na kucheza mechi za kimataifa za kirafiki, lakini TFF ilikuwa kichwa ngumu, matokeo yake ilikuwa rahisi wapinzani wao kushuhudia mechi zao za ligi na pia baadhi ya wachezaji kupata majeraha.

Kwa mujibu wa Sendeu kama TFF ingekubali kuahirisha mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar Jumatatu wiki iliyopita, ingewasaidia kupata mechi za kujipima nguvu dhidi ya timu za ama Afrika Kusini au Zambia.

Alilalamika kwamba mechi yao na Mtibwa Sugar wachezaji walichoka, lakini pia wapinzani wao walituma mashushu jambo ambalo wanaliona liliwaathiri kwa namna moja au nyingine.

Hata hivyo Sendeu alisema bado hawajakata tamaa na wameiomba TFF iwaahirishie mechi yao dhidi ya Kagera Sugar inayotarajiwa kufanyika kesho ili wapate kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya URA ya Uganda Jumamosi, ingawa hakuna dalili ya kufanikiwa ombi lao, huku pia wakitaka wasicheze mechi ya ligi mpaka watakaporudi kutoka DRC.

Papic amekaririwa na baadhi ya vyombo habari akilalamika kuwa kufungwa kwa Yanga kunatokana na kutopata maandalizi ya kutosha hasa mechi za kirafiki za kimataifa.

Yanga Jumamosi ilikubali kipigo cha mabao 3-2 katika mchezo wa kwanza hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo ili isonge mbele italazimika kushinda mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Februari 28 mwaka huu mjini Lubumbashi, DRC.

SOURCE: Habari LEO

4 comments:

Anonymous said...

tuache lawama ,kwani tunashiriki mashindano haya mara ya kwanza .hebu mara mishahara mara vingozi mara kambi .jamani tuwe wa kweli tanzania bado michano ya kuwania mbuzi.

Anonymous said...

Yanga inabidi wajipange upya kama wanataka kifika angalau nane bora za Afrika. Waache lawama za kijinga, kwa Yanga iliyopo hata wakiachiwa mwaka wajiaandae basi wakikanyaga pale DRC ni kichapo tu. Tafuteni mulipojikwaa acheni kutoa lawama za kipumbavu. Mdau nawasilisha

World of Soccer said...

Kwa jinsi mchezo ulivyokuwa Yanga tulishindwa kwa mpira tu.

Kwa wale wanaojua kutathmini mchezo wa soka watakubaliana nami kuwa wenzetu walijiandaa kwa ajili ya mchezo ule.

Mfano mmoja wapo ni ile system/mfumo walio tumia. Walikuwa wanakuwa watu watatu nyuma, sita katikati, na mmoja tu wanamuweka mbele.

Kizuri kwao ilikuwa yule mmoja aliye mbele alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kukaa na mpira, mbio, pamoja na akili ya uchezaji. Akipata mpira alikuwa na uwezo wa kukaa na mpira na kuwa subiri wenzake waongezeke mbele.

Kibaya kwetu mabeki wetu hawakujua jinsi ya kumkaba mtu huyu.

Cha pili kizuri kwao ni kuwa walikuwa wametuzidi watu wawili katikati, kwani sisi tulikuwa na wanne ilhali wao wana sita. Hali hii ilihitaji midfielder wa juu awe fighter pia, type ya Chuji. Na hapa ndipo napongeza ubora wa kocha wetu maana aliliona hili na kumuingiza Bonny.

Kwa kuwa walikuja kulinda ilitakiwa beki yetu iwe makini kwa Counter attack zao ila tukajisahau na kunogewa kushambulia ndio maana tupo hapa.

timu ni nzuri kocha ni mzuri, bado vijana wetu hawaja- mature kisoka. Hawajaweza kuusoma mchezo wakiwa uwanjani wao kama wachezaji bila kutegemea kukumbushwa na kocha. Haya yote yanarudi katika msingi wa soka hawakulelewa ipasavyo kisoka. wengi programmed soccer wameikuta Premier kama sio Yanga.

Anonymous said...

Message92, http://www.arlo.net/massacree/ online viagra, hwky0, http://www.arlo.net/fccgb/ buy viagra no prescription, xvgq3, http://www.arlo.net/fccgb/notes/ generic viagra, hnta9, http://www.arlo.net/bytes/ order cheap viagra, xacu3, http://www.arlo.net/live/ viagra