Monday, February 22, 2010

Yanga vs Toto Africa

Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea tena leo katika uwanja wa Uhuru wakati mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga watakapowakaribisha Toto Africa ya Mwanza.

Yanga inatarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa Toto Africa kwani vijana hao wa Mwanza maarufu kama Wana-Kishamapanda wapo katika kampeni nzito ya kuhakikisha wanabaki katika ligi kuu msimu ujao. Katika mchezo wao wa mwisho, timu hiyo iliifunga Majimaji huko Songea 2-1 na hivyo kujiweka vizuri katika kampeni yake.

Yanga nayo leo itautumia mchezo huo kujipima kabla ya kukwea pipa kuelekea Lubumbashi DRC kurudiana na Lupopo FC mwishoni mwa wiki.

Tusubiri dk. 90.

24 comments:

CM said...

1.Berko
2.Mbuna
3.Maftah
4.Owino
5.Nadir
6. Chuji
7.Nurdin
8.Bonny
9.Ambani
10.Tegete
11.Abdi

CM said...

Dk 5, 1-0 Boniface Ambani

CM said...

2-0 Jerry Tegete dk 21

CM said...

HT 3-0

Ambani dk.5 na 45, Tegete dk.21

CM said...

4-0 dk.48 Shamte Ally

Anonymous said...

Leo mambo poa nafasi ya pili lazma.

Anonymous said...

Aingie Ngassa aongeze mabao mpige bao mgosi ufungaji bora.

CM said...

5-0 Shamte Ally dk 52

CM said...

Ngassa hatashiriki game ya leo.

Yanga wamemaliza sub zote tatu:
Bonny/Shamte
Abdi/Bengo
Tegete/Odhiambo

Anonymous said...

inshaallah iwe mazoezi tosha kwa kuwakabili wacongo nategemea mambo yatakuwa mazuri yakifanywa mashambulizi ya nguvu tutarudi na ushindi si chini ya magoli matatu nawaamini forward wetu

CM said...

6-0 Shamte hat-trick dk 77

CM said...

full time

Yanga 6 Toto 0

Yanga sasa imefikisha pointi 42.

Anonymous said...

hata mngefunga 100 bado nyie zero tu! Mnakumbuka shuka asubuhi? ngoja WaCongo wajilie vitu vyao kiulaini. Nyie zenu kuwabwenga viwete then mnajiona mnajua!!!

Anonymous said...

Hata mufunge elfu 1000 hazitawasaidia, musubiri tu kichapo kwa Lupopo weekend hii. kazi yenu kuchapa vipofu halafu majisifu kwy magazeti, mpira ni uwanjani sio magazeteni subiri kichapo kwa DRC tu.

Anonymous said...

huyo mbwa katoka wapi?shut up u dog

Anonymous said...

hii blog juu kabisa imaandikwa ni ya wapenzi wa yanga pote ulimwenguni sasa huyo bundi anayelia hapo juu katoka wapi asituletee uchuro

Anonymous said...

mnajiona mmeshinda wapumbavu nyie na timu yenu,nendeni kongo tunawangoja namtafungwa sio chini ya 4 au zadi

Anonymous said...

hii ni 606 ya Yanga. ukijisikia vibaya kaanzishe blogu yako siyo kuleta matusi hapa. sawa sie wapumbavu sasa wewe kinakuuma nini mpaka ulete pua yako hapa? ukiona wapumbavu wawili na wewe ukajitia katikati yao, sasa tofauti iko wapi? maana matokeo yake utaona wapumbavu watatu!!

anywa acha watu wafurahie ushindi, bao 6 bila teh teh teh

Anonymous said...

huyu malaya wa simba anajiingiza hapa wewe umelipa ada ya uanachama au ni mpiga debe stendi ?shut up u dog.

Anonymous said...

hao wazambia vipi wamekuja?

CM said...

Yanga 1 ZESCO 1

Yanga imechezesha wachezaji wengi wa akiba akiwemo Jama Mba, Msigwa, Odhiambo, Njoroge etc

Anonymous said...

Hata mungechezesha wachezaji gani uwezo wenu mwisho ni kufunga hao TOTO na tutaona huko DRC! tayarisheni tu kapu la kubebea magoli, kwa uchache mutakula 3-0

Anonymous said...

Mtabaki kutukana tu mpira hamuwezi

Anonymous said...

Mtabaki kutukana tu mpira hamuwezi