Thursday, February 25, 2010

Yanga yatua Lubumbashi

Kikosi cha wachezaji 18 na viongozi 8 cha Yanga kimetua jijini Lumbumbashi tayari kwa mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya FC Lupopo.

Yanga imewasili nchini humo huku wachezaji wake wanne wakipatwa na balaa la kupotelewa na mabegi yao. Wachezaji waliopotelewa na mabegi yao ni Jerry Tegete, Boniface Ambani, Godfrey Bonny na Obren Circkovic.

Hali ya hewa huko Lubumbashi ambayo ilikuwa ikiripotiwa kwamba ni ya mvua kubwa imebadilika na kwa siku tatu sasa mvua haijanyesha jijini humo.

Kikosi kilichotua nchini humo ni makipa- Yaw Berko, Obren Curkovic, mabeki- Shadrack Nsajigwa, Amir Maftah,George Owino, Fred Mbuna, Nadir Haroub Cannavaro, Wisdom Ndhlovu.
Viungo ni - Athuman Idd 'Chuji', Kiggi Makassi, Godfrey Bonny. Washambuliaji ni, Mrisho Ngassa, Jerry Tegete, Shamte Ally, Steven Bengo na Boniface Ambani.

8 comments:

Anonymous said...

tuko nanyie,hamna hofu, mchezo ni burudani,kila la kheri .kwasababu tuna imani na timu nzima.

Anonymous said...

tutazidi kuwaombea tu, ushindi safari hii ni lazima. Mungu awabariki!

Anonymous said...

inshaallah mungu aibariki iwe safari ya ushindi yanga daima mbele

tina said...

na hizo mabegi za wachezaji zilizopotea nairobi zimeshawafikia wachezaji au ndio basi tena?

Anonymous said...

leo nileo yanga kuonyesha maajabu haya matokeo ya mabegi kupotea na kufanyiwa fujo hotelini itakuwa nguvu ya ziada kwa wachezaji yanga waingia raundi pili kila la khei wana yanga wote

Anonymous said...

Subirini KICHAPO WANA WA JANGWANI

Excomta said...

The problem is hawa jamaa hawana sehemu ya kuongelea mambo yao, hivyo wanahangaika kudandia hapa na pale. Tuwasamehe tuu. Ila tunawaomba wawe makini katika kudandia kwao kwani ni hatari kudandia gari lenye mwendokasi kwa mbele.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___