Tuesday, April 27, 2010

Papic kujifunga Yanga hadi 2011
KOCHA Mserbia, Kostadin “Bill Clinton” Papic amebadilisha uamuzi wake wa kuikacha Yanga baada ya kukubali kusaini mkataba mwingine wa mwaka moja na klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani na Twiga.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jana zinasema kwamba kocha Papic amekubali kusaini mkataba wa mwaka moja utakaoanza mwezi ujao ikiwa ni wiki moja tangu alipotangaza kuikacha klabu hiyo kwa kushindwa kumlipa mshahara.

Papic alichukua uamuzi huo baada ya kukutana na viongozi wa klabu hiyo kujadili kwa undani kuhusu malipo yake.

Kiongozi mmoja wa Yanga, alisema Papic alikutana na mfadhili Yusuf Manji na kukubaliana kuyamaliza matatizo yake yote yaliyojitokeza kwenye mkataba wake wa kwanza.

Moja ya matatizo ni madai yake ya mshahara na malalamiko yake ya kutoheshimwa. Tangu alipokataa kuongeza mkataba wake mwaka jana mwezi Oktoba.

Mserbia huyo anategemea kusaini mkataba mpya mapema wiki ijayo utakaodumu hadi Mei 2011, kwa mujibu wa chanzo hicho cha habari.

Kwa habari zaidi endelea hapa.

11 comments:

Anonymous said...

Karibu Jangwani kiongozi wa ngoma na maigizo. Utatupa kila sababu ya kuendelea kuwachapa mwakani. Lazima tumle samaki pande zote yaani mzunguko wa kwanza na wa pili ni kichapo tu

Anonymous said...

kishoka njaa tupu huyo hana jipya ,sitaki nataka hana jipya ktk soka zaidi ya kijipa misifa tu,tatizo yanga mnababaika na udhungu na mwakani mtafulia sana kwa mpango huo.

Anonymous said...

shut up you sheep.huna aibu.

Anonymous said...

hivi nyie inawahusu nini?madam wenyewe tupo radhi naye nyie mnajiingiza hata ktk mambo yasiyowahusu hebu muwe na haya kidogo mnakarikibishwa mnaanza kutowa mafunzo nani anataka ushauri wenu nyie furahieni ya kwenu ktk blog yenu ambayo hamwezi kuingia

Anonymous said...

hivi nyie inawahusu nini?madam wenyewe tupo radhi naye nyie mnajiingiza hata ktk mambo yasiyowahusu hebu muwe na haya kidogo mnakarikibishwa mnaanza kutowa mafunzo nani anataka ushauri wenu nyie furahieni ya kwenu ktk blog yenu ambayo hamwezi kuingia

Anonymous said...

si unajua wanapenda kusema la wenziwe wenyewe hawana lolote.wajinga watupu.

Anonymous said...

WEWE NI SHEEP YAANI KONDOOOOOO,HILO LA YANGA LAKUUMA NINI?FUATA NJIA YAKO SAVE YOUR MONEY FOR OTHER REASON THAN TO GO TO INTERNET LOOKING ON YANGAS BLOG.

Anonymous said...

Msibishane na Simba jamani kwani ya kwao yamewashinda. Hebu angalieni walivyo wachafu kuliko hapa.. http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/klabu-ya-simba-balaa-tupu#comments

Anonymous said...

Ntajijuuuuuuuu wana wa Manji

Anonymous said...

Hao MASHOGA hapo juu wametoka wapi tena?. Mbona hii blogu si ya mipasho! Hebu kasafisheni jengo lenu kama hamna jipya la kuchangia hapa. EBO!

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___