Thursday, May 20, 2010

Maftah basi tena
KLABU ya Yanga imevunja mkataba na beki wa timu hiyo Amir Maftah kwa madai ya kuonyesha kitendo cha utovu wa nidhamu wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi Simba ulifanyika Aprili 20 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa mzunguko wa pili, Maftaha alitolewa nje na mwamuzi kwa kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kichwa kwa makusudi beki wa Simba, Juma Nyoso na kuiacha timu yake ikitandikwa mabao 4-3.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Imani Madega alisema kuwa uamuzi wa kumwondoa Maftah katika timu yake umefikiwa na kamati ya utendaji ya Yanga iliyokutana na kujadili marekebisho ya katiba ya klabu hiyo pamoja na tathmini ya msimu wa ligi kuu iliyomalizika.

"Kama ambavyo wote tulishuhudia mchezo kati yetu na Simba ulivyokuwa kulikuwa na kadi nyekundu mbili ambayo ni ile ya Maftah na Wisdom Ndhlovu ambazo kimsingi ndizo zilizosababisha tupoteze mchezo ule, ukweli kutokana na matokeo yale kulizuka hisia na minong'ono iliwahusisha ama viongozi au wachezaji na kuihujumu timu.

"Kimsingi, sisi hatukuzipuuzia hisia hizo tulizifanyia kazi ingawa tulishindwa kuthibitisha kama kweli ilikuwa ni hujuma lakini kwa kuzingatia kuwa Maftah aliwahi kuonywa na kupewa nafasi ya mwisho kujirekebisha na uongozi baada ya kutoroka kambini mjini Morogoro, kamati ya utendaji amefikia uamuzi wa kuachana naye na hatutamsajili katika kikosi cha msimu ujao au kwa maana nyingine yeye ni mchezaji huru kuanzia sasa,"alisema Madega.

14 comments:

Anonymous said...

Kumfukuza bila ushahidi wa kueleweka ni kama kupoteza wachezaji bila sababu za msingi na kulea majungu.Watanzania lazima tupevuke kimchezo, tukizidiwa lazima tukubali kwamba tulizidiwa sio kusingizia watu

Anonymous said...

Tuwe makini kuongeza training facilities na mambo ya msingi, mfano usajili unaolenga kuziba mapengo katika nafasi zilizokuwa na mapungufu msimu ujao.La sivyo tutakua wasindikizaji na msimu ujao

Anonymous said...

Mshambuliaji mahiri wa zamani wa Yanga na pia Taifa stars leo amesaini kuichezea Azam FC kuanzia msimu ujao wa 2010/2011 na atakuwa akilipwa mshahara wa 1.2m kwa mwezi na ada yake ya uhamisho ni 40m. Hili ni pigo kubwa sana kwa Yanga kwa wko mbioni kumpoteza Nadir Haroub Canavaro...

Anonymous said...

kwa nini ni pigo kubwa kwa yanga? Kwani wapikuwa wauzwe nje hao wachezaji lisingekuwa pigo? Yanga tunachotakiwa kufanya ni kufanya usajili utakaoziba mapengo yao na mapengo yaliyojitokeza kwenye msimu uliopita

Anonymous said...

kama tutafuata maelekezo ya Papic kuhusu wachezaji anaowahitaji basi hakuna cha kututisha msimu ujao.Ninawaomba viongozi wasajili kama kocha alivyoagiza.

Anonymous said...

na lile gunia la msumari linalobebwa huko rwanda limekuaje?

Anonymous said...

leo tena kimewaka huko Kigali

APR 2 Simba 1

Anonymous said...

Timu bora Afrika mashariki imefungwa mechi tatu katika nne ilizocheza? Sijawahi ona timu mbovu kama hii.

Unknown said...

SIMBA WAHAPAHAPA

Anonymous said...

WAHAPAHAPA,WAHAPAHAPA HAO.

KATIKA MECHI 5 ZA KIMATAIFA WAMESHINDA 1 NA KUCHAPWA 4. WARUDI WAENDELEE KUNUNUA ZA HAPAHAPA

Anonymous said...

TIMU IMEFUZU KWA KUSHINDA MECHI MOJA KATI YA TATU,INGEWEZAJE KUSONGA MBELE.
ZAO KUCHONGA TU.
NA WALE PANYA BUKU MBONA HAPWAPO HUMU SIKU HIZI.NANI KAWAKIMBIZA

AAAAAAHHHHHHHHH ASAFALI PAKA

Anonymous said...

KUONDOKA KWA NGASA HAKUTAKUWA NA ATHARI KWA TIMU. KOCHA TULIYE NAYE ANAUWEZO WA KUIBADILI TIMU. NGASA ALIKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWENYE TIMU, LAKINI KWA FEDHA ALIZOPEWA NI SAWA AENDE,TUNAMTAKIA MAFANIKIO ZAIDI MPIGANAJI WETU.

Anonymous said...

contena la brush linakuja vyoo sasa vitang'ara msimbazi wao na mpira wapi na wapi bora wafanye usafi

Unknown said...

Wale Panyabuku wamekimbizwa na yule paka anayependa kukaa kwenye sofa. Wakajifanya kukimbia kodi, Mamlaka ya kodi ya mapato uganda ikawatia nguvuni na sasa wapo kwenye jela la wanajeshi wa APR ambako wameambiwa wakiachiwa wasionekane kabisa Rwanda. Hivyo wakati wowote watarudi kwani wale ni WAHAPAHAPA tu. Wakishaanza kununua mechi za hapa nyumbani kama kawaida yao wale PANYABUKU wataonekana tena na tambo zao.