Monday, June 07, 2010

Ligi Kuu ya Vodacom

Pazia kufunguliwa leo
Msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom unafunguliwa leo kwa timu zote 12 zinazoshiriki ligi hiyo kuingia uwanjani.

Ligi ya msimu huu inatarjiwa kuwa ya ushindani kwa vilabu vitatu vya Yanga, Simba na Azam ambazo zinaonekana kufanya usajili makini kwa ajili ya msimu huu mpya.

Timu ya African Lyon tayari imetabiriwa na wengi kuwa haitafanya vizuri katika msimu huu kutokana na kukimbiwa na wachezaji wengi, huku klabu hiyo iliyokuwa inamilikiwa na Mohamed Dewji kuuzwa kwa mfanyabiashara anayejulikana kama Zamunda.

Timu nyingine zitakazoshiriki ligi hiyo ni Polisi Dodoma, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Majimaji, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Toto Africa na AFC.

Kituko cha aina yake mwaka huu ni usajili wa mchezaji mwanamke ambaye amesajiliwa na klabu ya Polisi ya Dodoma - Mnigeria Biku Bagayajennje.

Mechi zitakazopigwa leo ni:
Polisi Dodoma vs Yanga
African Lyon vs Simba
AFC vs Azam
Toto Africa vs Ruvu Shooting
Kagera Sugar vs JKT Ruvu
Majimaji vs Mtibwa Sugar

3 comments:

Anonymous said...

Inaonyesha wewe mpiga picha na uliyetuma hii picha sambamba na kuandika maneno haya akili zako zina walakini. kwa Lugha nyingine wanayosema akili ni nywele wewe kuna nywele zimekatika au zimenyofoka! ujumbe hauna maana! Tuache na Yanga yetu na faida zetu za kuwa Yanga! majungu peleka huko huko!

Anonymous said...

Mbona hakuna tatizo kwenye hiyo post? au mzee ulipanga foleni halafu ukakosa tiketi?

Anonymous said...

Wana yangu tufumbuke macho. hivi kizuri kwetu ni kugawiwa ticket za bure, kulipiwa ada au kuwa na timu nzuri ambayo itachukua ubingwa, kutofungwa na simba na kuwika afrika. kuliko kutulipia mapesa kununua ticket ambazo hata sisi tungeweza si tusajili basi african classic player ili tuwe na raha na amani kwa ushindi? au si angempa ngassa abaki jangwani. au ndio yale mtu anakwambia kunywa pombe tani yako lakini ukimuomba elfu moja ununue chips anakataa? natamani ningepata nafasi ya kuongea na madega. anaweza kuwa na mengi moyoni