Monday, June 14, 2010

Uchaguzi Yanga sasa Julai 18

KAMATI ya uchaguzi ya klabu ya Yanga imetangaza kuanza mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kuwaJulai 18 huku wagombea wa nafasi ya uenyekiti na makamu wake wakilazimika kujipapasa mifukoni kwa Sh 200,000 za fomu huku wagombea wa nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji wakilazimika kutoa Sh100,000.

Awali, uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Julai27 katika mkutano mkuu uliofanyika wiki moja iliyopita ambao pamoja na mambo mengine ulipitisha marekebisho ya katiba ya klabu hiyo kulingana na maagizo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jaji John Mkwawa alisema sababu zilizosababisha kubadilika kwa tarehe hiyo ni pamoja na klabu hiyo kutokuwa na kanuni za uchaguzi, hivyo wanatakiwa kutumia kanuni za TFF za uchaguzi wakati muda huo wa kuitisha uchaguzi unatakiwa usizidi siku 40.

"Kikubwa wanachama wawe na subiri na wasilete malumbano ambayo mwisho wake ni vurugu tupu mimi napenda kuwashauri wawe watulivu ili tuweze kwenda vizuri katika hili,"alisema Jaji Mkwawa.

Aidha, Jaji Mkwawa alisema fomu zitaanza kuchukuliwa Juni14 na kurudishwa Juni18 huku siku ya uhakiki wa fomu hizo ikipangwa kuwa Juni2o na siku inayofuata majina ya walioomba nafasi za uongozi huo yatawekwa hadharani.

Alisema Juni 21 hadi26 ni wakati wa kuweka pingamizi dhidi ya wagombea kama zipo na siku inayofuata itakuwa ya kuyapitia majina hayo usaili wa wagombea ukiwa Juni28.

Alisema Julai 2- 5 wakati wa kupokea rufaa za wagombea na siku inayofuata ni kutangazwa kwa majina ya wagombea waliopita huku Julai 7 ikiwa mahsusi kwa kuanza kwa kampeni za uchaguzi huo.

Aidha, mwenyekiti huyo aliwataka wanachama wote kuachana na malumbano na badala yake wakae na kuangalia jinsi ya kupata viongozi hao wapya wenye sifa ambao wataisaidia klabu hiyo kurudisha ubingwa wake ambao umechukuliwa na watani zao, Simba.

2 comments:

Anonymous said...

INAPENDEZA, ILA MAONI YANGU NI KWAMBA TUJARIBU KUACHANA NA HAWA WALIOWAHI KUSHIKA MADARAKA NA WAKAACHA MAKOVU YA MAKUNDI NDANI YA KLABU.
CHA AJABU NASHANGAA SASA WANACHUKUA FOMU ZA KUWANIA!!!!
LAKINI KWA KUWA NI HAKI YAO KIDEMOKRASIA, TUWAACHE ILA TUWACHAMBUE KWENYE SANDUKU LA KURA.
KUTOKA KUMOYO NAPENDEKEZA MZEE KANALI KIPINGU APEWE UENYEKITI KAMA ATAGOMBEA, KWANI ANA KILA SIFA ZA MTU WA SOKA.
KUMBUKA NI WACHEZAJI WANGAPI NCHI HII KAWAIBUA PALE KWAKE KUPITIA PROGRAM YAKE YA VIJANA.
HATA KTK MASHINDANO YA VIJANA KWA TIMU ZA U 23 LIGI KUU ALILAZIMIKA KUTUPA YANGA WACHEZAJI KUTOKA KITUO CHAKE CHA BAGAMOYONA WALITUFICHIA AIBU YA AKINA MADEGA AMBAO WALIKUWA NA TIMU YENYE WACHEZAJI PUNGUFU BAADA YA VIJANA ALIOWACHAGUA JACK CHAMANGWANA KUKIMBILIA AZAM FC.
NAWATAKIA UCHAGUZI MWEMA.
WENU,
WAKILI WA SERIKALI KANDA YA MBEYA

Anonymous said...

badilisha sera ,uuza mchezaji ili tupate wacheza sio kusema mchezaji hauzwi au vunja benki kupata mchezaji yanga hii ndio tunakatisha tamaa wachezaji wengi kujiunga na klabu yetu.rejea habari zilizoandikwa kwenye habari leo.