Saturday, August 21, 2010

Ligi Kuu Ya Vodacom

Pazia kufunguliwa leo
Msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom unafunguliwa leo kwa timu zote 12 zinazoshiriki ligi hiyo kuingia uwanjani.

Ligi ya msimu huu inatarjiwa kuwa ya ushindani kwa vilabu vitatu vya Yanga, Simba na Azam ambazo zinaonekana kufanya usajili makini kwa ajili ya msimu huu mpya.

Timu ya African Lyon tayari imetabiriwa na wengi kuwa haitafanya vizuri katika msimu huu kutokana na kukimbiwa na wachezaji wengi, huku klabu hiyo iliyokuwa inamilikiwa na Mohamed Dewji kuuzwa kwa mfanyabiashara anayejulikana kama Zamunda.

Timu nyingine zitakazoshiriki ligi hiyo ni Polisi Dodoma, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Majimaji, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Toto Africa na AFC.

Kituko cha aina yake mwaka huu ni usajili wa mchezaji mwanamke ambaye amesajiliwa na klabu ya Polisi ya Dodoma - Mnigeria Biku Bagayajennje.

Mechi zitakazopigwa leo ni:
Polisi Dodoma vs Yanga
African Lyon vs Simba
AFC vs Azam
Toto Africa vs Ruvu Shooting
Kagera Sugar vs JKT Ruvu
Majimaji vs Mtibwa Sugar

5 comments:

CM said...

Halftime
Yanga 1 Polisi 0 (Tegete)
Simba 1 Lyon 0 (Maftah)

Anonymous said...

Asante CM

CM said...

Simba 2 Lyon 0 (result)
Yanga 1 Polisi 0
Azam 2 AFC 0

Anonymous said...

Vipi mambo Dodoma kaka CM

CM said...

Matokeo ya leo:
Simba 2 Lyon 0
Polisi 0 Yanga 1
AFC 0 Azam 2
Majimaji 0 Mtibwa 1
Toto 2 Ruvu 0
Kagera 0 JKT 1