Tuesday, August 03, 2010

Ngao ya Hisani 2010

Yanga vs Simba sasa Agosti 18
Shirikisho la soka nchini TFF imesogeza mbele pambano la Ngao ya hisni kati ya Yanga na Simba lililokuwa lipigwe tarehe 14 Agosti hadi 18 Agosti mwaka huu.

Kusogezwa huko kunatokana na timu hizo mbili kuwa na wachezaji wengi katika timu ya taifa ambayo itakuwa na mchezo wa kirafiki huko Misri. Pambano kati ya Taifa Stars na Mafarao wa Misri linatarajiwa kupigwa Agosti 11 Jijini Cairo.

Kikosi cha Taifa Stars kilichotangazwa jana ni:Kikosi kamili cha Stars kinaundwa na:-
Makipa: Juma Kaseja (Simba), Jackson Chove (Azam), Shaban Hassan Kado wa Mtibwa Sugar.

Mabeki: Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasika, Nadir Haroub 'Cannavaro' (Yanga), Salum Kanoni, Juma Jabu, Kevin Yondan, (Simba), Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam) na Idrisa Rajabu wa Sofapaka ya Kenya.

Viungo: Nurdin Bakari, Athuman Idd, Kigi Makasi, Abdi Kassim, (Yanga), Abdulhaim Humoud, Uhuru Selemani (Simba), Henry Joseph (Kongsvinger, Norway), Nizar Khalfan(Vancouver Whitecaps, Canada), Jabir Aziz na Selemani Kassim wa Azam.

Washambuliaji: Mrisho Ngasa, John Bocco (Azam), Mussa Mgosi (Simba), Jerryson Tegete (Yanga) na Danny Mrwanda anayekipiga klabu ya DT Long An ya Vietnam.

4 comments:

Anonymous said...

Hivi wajemeni tarehe 18/8/2010 tucheze na mnyama Dar na kisha ndani ya siku 2 tusafiri na kucheza Dodoma na Polisi, wakati mnyama atabaki dar na kucheza na Lyon ambayo haina wachezaji wa ligi kuu/ waliokata tamaa, hizi siyo mbinu za mnyama kuwekeza katika uongozi wa TFF Taifa?

Anonymous said...

acha hizo ,zimepitwa na wakati sasa hivi ni kazi moja tuu.tandaza kandanda.

Anonymous said...

Wazee facebook ya wapenzi iko hapa;

http://www.facebook.com/pages/edit/?id=144971678852174#!/pages/I-am-a-FAN-of-YOUNG-AFRICANS-SC/144971678852174

Anonymous said...

Wadau vp matokeo ya yanga na expres?