Wednesday, August 18, 2010

Ngao ya Hisani

Kenaaaakooooo!!
Ule msemo maarufu wakati wa Kombe la Dunia 2010 - Ke Nako (its time)umewadia tena safari hii ikiwa ni katika mchezo wa kuwania ngao ya hisani kati ya Simba na Yanga itakayopigwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa.

Mechi hiyo inazikutanisha timu hizo baada ya kuwa timu zilizoshika nafasi ya juu msimu uliopita wa Ligi Kuu ambapo Simba ilishika nafasi ya kwanza na Yanga nafasi ya pili.

Katika kujiandaa na pambano hilo, Yanga iliweka kambi huko Bagamoyo wakati Simba ikijificha huko Zanzibar.

LIcha ya kujiandaa huko, hakuna timu iliyo na uhakika wa ushindi kwani baadhi ya wachezaji walikuwa wanakabiliwa na malaria na kwa upande wa Simba itamkosa kipa wake tegemeo Juma Kaseja ambaye ameumia kidole.

Endapo pambano hilo litamalizika kwa sare, timu hizo zitawenda moja kwa moja kwenye matuta.

Kivutio kingine katika pambano hilo ni kuwa mechi hii itakuwa ya kwanza kwa uongozi mpya ya vilabu hivi viwili ambavyo hivi karibuni walifanya uchaguzi ambao uliwaweka madarakani Wenyeviti Lloyd Nchunga wa Yanga na Ismail Aden Rage wa Simba.

Tusubiri tuone pambano.

19 comments:

CM said...

Game limeanza dk 5 bado 0-0 line up:
1. Berko
2. Nsajigwa
3. Mwasika
4. Nadir
5. Isaac Baokye
6. Ernest Boakye
7. Nurdin
8. Chuji
9. Asamoah
10. Abdi
11. Nsa Job

Anonymous said...

Asante sana.tupatia update yuweze kujua mambo yanakwendaje

CM said...

dakika 21 bado ni 0-0

CM said...

dakika 32 bado 0-0

Anonymous said...

Kaka CM vipi mechi tumekaribia kupata goli na vipi mashambulizi yanaendaje?

CM said...

halftime 0-0

Mashambulizi mengi yalikuwa langoni mwa Simba. Kipa wa Simba amekuwa kikwazo.

CM said...

mpira ni mkali, bado 0-0

CM said...

dk 80 mambo bado 0-0

CM said...

dakika 90 zimemalizika kwa sare ya 0-0. Tunakwenda kwenye matuta

Anonymous said...

Naona matuta yatatoa mshindi

CM said...

Simba wamelala

CM said...

Simba wamelala kwa penati 3-1

Anonymous said...

Tumepoteza penati yoyote?

CM said...

mambo yalikuwa hivi;
Okwi - alikosa
E. Boakye- alikosa
Uhuru - alikosa
Bonny-alifunga
Kiemba - alikosa
Mwasika-alifunga
Banka-alifunga
I Boakye - alifunga

Tumeshinda 3-1

Anonymous said...

asante mkubwa! naamini kosa kosa za simba ni kwa sababu ya uimara wa kipa wetu na si kwamba walipiga nje, au? yote na yoye, tumewashika!

Anonymous said...

Ahsante Mkubwa kwa ktuletea uhondo huu. Naomber wapenzi wa blog hii tuanze ktathmini game lilivyokuwa mnaonaje?

Anonymous said...

Kumbe Simba bila Kaseja ni bure kabisa!

Anonymous said...

CM nakukubali sana kwa update zako

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___