Tuesday, September 28, 2010

Laurent Kabanda hatunaye


Mchezaji wa zamani wa Yanga Laurent Kabanda amefariki dunia.

Kwa mujibu wa habari ambazo zimethibitishwa na Afisa Habari wa klabu hiyo Louis Sendeu, Kabanda amafariki jana asubuhi mara baada ya kutoka katika mazoezi huko Lubumbashi DRC.

Kabanda aliichezea Yanga msimu wa mwaka 2007/8 wakati huo Yanga ikiwa chini ya kocha Dusan Kondic. Hata hivyo Kabanda licha ya kusajiliwa kwa fedha nyingi kutoka APR ya Rwanda, aliitoroka Yanga baada ya kutofautiana na kocha huyo.

2 comments:

Anonymous said...

Rest in Peace Kabanda.

Shein Rangers Sports Club said...

Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu peponi, amen!