Tuesday, October 26, 2010

Asamoah mpaka raundi ya pili

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana limetoa tamko rasmi kuhusu sakata la mshambuliaji Kenneth Asamoah kuwa hataweza kuichezea timu hiyo katika kipindi cha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, labda asubiri dirisha dogo la usajili.

Hatua hiyo imekuja baada ya klabu ya Yanga kulishutumu shirikisho hilo kwamba ndio wamesababisha mchezaji huyo kutoichezea klabu hiyo hadi sasa.

Akizungumza na Jijini jana, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni alisema tatizo lililokuwepo ni malipo ya uhamisho wa mchezaji huyo ambayo Yanga ilipaswa kuyafanya mapema zaidi kwa klabu ya Serbia.

"Sisi hatuhusiki kabisa juu ya suala la Asamoah, Yanga wenyewe ndiyo wakuwa wakijichangaya kwa sababu mpaka wakati tunafunga usajili mwezi Julai walikuwa wajifika makubaliano ya uhamisho wake.

"Kutokana na hali hiyo Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) lilikataa kutoa kibali cha kumruhusu mchezaji huyo kwa sababu tayari muda wa usajili ulikuwa umemalizika labda wasubiri katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari," alisema Kayuni.

2 comments:

Anonymous said...

Yanga mnatuzingua sana mashabiki,ile raha ya kuifunga simba yote imeshaisha,tushaanza kuona kumbe simba tuliwabahatisha tu, droo ya 3 mfululizo inaonyesha timu yetu ishajifia,mashabiki tushapoteza matumaini hata ligi yenyewe sitaki kuifatilia tena maana naona naumia moyo tu

Anonymous said...

Hata ile ushindi dhidi ya simba tulibahatisha.tulizidiwa mechi nzima watani walitengeneza magoli mengi lakini bahati haikuwa yao.timu yetu hamna lolote.tumesha droo mechi 4 sasa.tukubali mwaka huu hakuna ubingwa tena.ahh