Saturday, October 23, 2010

Ni Azam vs Yanga
Baada ya kulazimishwa sare na JIKT Ruvu katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania, Yanga itateremka dimbani tena Jumapili hii kupambana na Azam FC katika uwanja wa Mkwakwani huko Tanga.

Kivutio kikubwa katika mpambano huo ni mchezaji Mrisho Ngassa ambaye alihama klabu ya Yanga na kuhamia Azam kwa uhamisho uliovunja rekodi ya usajili kwa Tanzania.

Yanga inaongoza ligi hiyo kwa kujikusanyia jumla ya pointi 20 na ina rekodi ya kufungwa goli moja tu mpaka sasa wakati azam ndiyo timu iliyofunga mabao mengi katika ligi hiyo. Azam ina mabao 10.

Michezo ya ligi hiyo itakayopigwa leo ni Toto vs African Lyon, Ruvu vs Mtibwa na AFC vs Polisi Dom.

Kesho Simba itaumana na JKT Ruvu.

.

10 comments:

Anonymous said...

wanajangwani tunataka magoli na sio tuu kumuua myama, asanteni
mdau italy

Anonymous said...

wanajangwani tunataka magoli na sio tuu kumuua myama, asanteni
mdau italy

Anonymous said...

Mapumziko matoke 0 - 0. morogoro simba 2 jkt wapuuzi wanaopenda kuhongwa 0

CM said...

Kipindi cha pili dk 17 bado mambo ni 0-0

tina said...

Asante CM na update.tafadhali ondoa uchafu ndani.
Tunatake mambo ya ukweli tuu.

CM said...

full time 0-0

Anonymous said...

Asante.vipi morogoro matokeo vipi.

Anonymous said...

Simba tunamfukuza mbwa kimya kimya, mlitangulia na baiskeli ya matope sasa mvua imeanza kunyesha inaanza kukosa kasi, kabla raundi ya kwanza haijesha kuna timu itawafunga na sisi hatuna mpango wa kupoteza mechi mpaka msimu unaisha. Mtajijuuuuuuuu

Anonymous said...

habari ya asubuhi ndio kwanza umeamka?

CM said...

matokeo ya Morogoro Simba 2 JKT 1